Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jamuhuri ya Muungano wa Afrika - Wanaigeria wapendekeza jina jipya la nchi yao
Je mtu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Afrika ataitwaje? Uranium or Urea?
Jibu ni kuwafanya Wanaigeria wengi kuwa na uelewa kuhusu pendekezo la kubadili jina la nchi.
Wiki mbili mfululizo, wabunge wamekuwa wakikusanya maoni ya wananchi kuhusu kufanya marekebisho katika katiba.
Wazo lilikuwa ni kupata maoni ya kufanya marekebisho kama kwenye uchaguzi na mfumo wa serikali.
Lakini mwananchi kama Adeleye Jokotoye, mshauri wa masuala ya kodi, aliacha jambo moja ambalo liliwashtua wengi mjini Lagos.
Anataka jina la nchi libadilike kutoka kuwa Nigeria akisema ni jina ambalo liliwekwa na wakoloni.
Jina la Nigeria, lilipendekezwa karne ya 19 na mwandishi wa habari wa Uingereza Flora Shaw, ambaye baadaye aliolewa na kiongozi wa utawala wa kikoloni Frederick Lugard.
Limetokea kwenye jina la ziwa Niger ambalo linaingia nchi hiyo kutoka Kaskazini Magharibi na ikitiririka katika maporomoko ya Niger yanayotoka katika bahari ya Atlantic ingawa kuna mikondo mingi.
Lakini bwana Jokotoye anataka kubadili jina la Nigeria ili kuwa Muungano wa Jamhuri ya Afrika - kuwakilisha mamia ya jamii ya kundi la watu wa taifa hili.
Watumiaji wa Twitter wana nadharia ya eneo ambalo wazo la Muungano wa Jamhuri ya Afrika, au UAR, limetokea wapi:
Tayari kuna wimbo wa taifa, ambao si mpya kabisa bali ni marejeo ya wimbo wa zamani wa Nigeria:
Jina jipya la nchi linahitaji fedha mpya:
Na kulikuwa na kumbusho la masuala madogo ya mkopo ambao Nigeria inadaiwa na benki ya dunia, IMF na China.
Wengine walifikiri kwamba jina jipya linamaanisha mwanzo mzuri:
Lakini kila mtu anaona kuwa pendekezo la bwana Jokotoye ni la utani kwa kuwa taifa lina mambo mengi muhimu ya kuzingatia kwanza:
Lakini mtu kutoka UAR anaitwaje? Wazo la jina la madini ya Uranium - ambalo Nigeria halina -linaonekana linatoka kwa mchekeshaji:
Na masuala madogo yanajumuishwa na Uranium:
Ni kama alijua kuwa baadhi ya wenzake hawatakubaliana na chaguo lake.
Bwana Jokotoye alikuja na mbadala - the United Alkebulan Republic (maana yake ikiwa : United Mother of Mankind Republic), ambalo kwanza halionekani kama la watu wa Afrika, lakini lina herufi hizo hizo.
Pia alitoa mapendekezo kuhusu katiba, kama vile kupendekeza marekebisho katika mfumo wa serikali , udhibiti wa kodi - lakini pia kwa sababu kadhaa hayo hayakuweza kutoa hamasa ya wengi kwa namna ile ile.
Katika wiki zijazo wabunge wataweza kupitia mapendekezo waliopokea kutoka kwa raia wa Nigeria , ingawa hakuna anayejua ni yapi yatashangaza watu au kupitishwa.
Lakini ni kama hatutaweza kuiona Jamuhuri ya Muungano wa Afrika katika uelekeo huo.
Ni jambo la aibu, kama nikiachana na wazo la kuitwa Uranium - lina nguvu sana.