fahamu kwanini magari ya kutumia umeme yatautawala ulimwengu wetu hivi karibuni

Chanzo cha picha, Getty Images
Najua huenda hujaendesha gari la umeme au hata hujawazia kununua gari hilo, utabiri wangu unaweza kuonekana kuwa na ujasiri, lakini nivumilie.
Tuko katikati ya mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa utengenezaji wa magari tangu Henry Ford alipoanza kutengeza magari ya kwanza mnamo mwaka 1913.
Na huenda yakafanyika hataka zaidi ya unavyodhania.
Wadadisi wengi wa tasnia ya utengezaji magari wanaamini tayari tumepita mahali ambapo mauzo ya magari ya umeme (EVs) yatazidi magari ya petroli na dizeli kwa haraka sana.
Bila shaka huenda watengenezaji wakuu wa magari wanatilia wazo hilo maanani.
Jaguar inapanga kuuza magari ya umeme pekee kuanzia mwaka 2025, Volvo kuanzia 2030 na wiki iliyopita kampuni ya Uingereza ya utengenezaji magari ya Lotus ilisema itafuata mkondo huo kwa kuuza magari ya umeme pekee kuanzia 2028.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na sio kampuni hizo za magari ya kifahari pekee.
General Motors imesema itatengeza magari ya umeme pekee kufikia mwaka 2035, Ford imesema magari yote yatakayouzwa Ulaya yatakua ya umeme kufikia mwaka 2030 na VW inasema 70% ya mauzo yake yatakuwa ya magari ya umeme kufikia mwaka 2030.
Huu sio utani, huu ndio ukweli wa mambo.
Ukweli ni kwamba, serikali kote duniani zinaweka azimio la kupiga marufuku uuzaji wa magari yanayoendeshwa kwa petrol na dizeli kwa kupatia kipaumbele mchakato huo.
Lakini kinachofanya mwisho wa injini ya mwako wa ndani isiepukike ni mapinduzi ya kiteknolojia.
Na mapinduzi ya kiteknolojia huwa yanatokea haraka sana.
Mageuzi hayo yatakuwa ya umeme
Hebu angalia intaneti.
Ukitaka kupata taswira kamili ya soko la magari ya umeme tafakari hali ya huduma za intaneti ilivyokuwa miaka ya 1990 au mwanzo wa miaka ya 2000.
Wakati huo kulikua na gumzo kubwa kuhusu hiki kitu kipya kilichokuwa na uwezo wa kufanya kompyuta kuwasiliana.
Jeff Bezos alikua ameanzisha Amazon, na Google ilikuwa imeanza kuchua usukani kutoka kwa makampuni kama vile Altavista, Ask Jeeves na Yahoo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wazo ni kwamba ubunifu huanza polepole, kwa kuwavutia tu wale wanaopenda mambo mapya.
Kwa ntaneti, jedwali linaanza 22:30 tarehe 29 Octoba mwaka 1969. Huo ndio wakati kompyuta katika Chuo Kikuu cha California huko Los Angeles iliwasiliana na kompyuta nyingine katika Chuo Kukuu cha Stanford University maili 100 kutoka hapo.
Wachunguzi waliandika herufi L, kisha O, ikafuatiwa na G. Mtambo ulikwama kabla wakamilishe kuandika neno "login".
Kama nilivyosema ni watu wachache waliovutiwa na ubunifu ndio waliojaribu.
Muongo mmoja baadaye bado kulikuwa na kompyuta chache kwenye mtandao lakini kasi ya mabadiliko ilikuwa inaongezeka kwa kiwango kikubwa.
Miaka ya 1990 wale waliokuwa na ujuzi wa kiteknolojia walianza kununua kompyuta zao binafsi.
Soko lilipoendelea kuwa kubwa, bei ikashuka na utenda kazi ukaimarika pole pole - kuwavutia watu wengi kujiunga na intanet.
S ilianzia hapa kupanda, ukuaji ukawa mkuwa zaidi. Kufikia mwaka 1995 kulikuwa na watu milioni 16 mtandaoni. Kufikia mwaka 2001, walikuwa wameongezeka hadi watu milioni 513 .
Sasa kuna zaidi ya watu bilioni tatu mtandaoni. Kitakachofanyika kwa S yetu baadaye inaanza kuchuka kuelekea kulia (usawa) .
Kiwango cha ukuaji kinashuka kwasababu kila mtu hatimaye anataka kuwa mtandaoni.
Dharau ya Jeremy Clarkson
Tuliona mfano huo wa kuanza polepole, ukuaji wa kielelezo na kisha kupungua kwa soko kulikomaa na simu aina ya smartphone, picha, hata dawa za antibiotiki.
Injini ya mwako ndani mwanzoni mwa karne iliyopita ilifuata njia hiyo hiyo.
Vile vile injini za mvuke na mashine za kuchapa. Na magari ya umeme yatafanya vivyo hivyo.
Gari la kwanza la umeme lililosafirishwa lilitengenezwa na mvumbuzi wa Scotland Robert Anderson mnamo miaka ya 1830.
Lakini ni katika miaka michache iliyopita tu ambapo teknolojia imeiwezesha kupatikana kwa bei nafuu sasa inaifanya kuwa na ushindani.
Mtangazaji wa zamani wa Top Gear na muuzaji wa magari yaliyotumika Quentin Willson anapaswa kujua.
Amekuwa akiendesha magari ya umeme kwa zaidi ya muongo mmoja.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alijaribu kuendesha gari laa General Motors aina ya EV1 20 miaka kadhaa iliyopita. Iligharimu dola bilioni kadhaa kuitengeneza lakini haikuvutia GM, ambayo iliharibu magari yote iliyokuwa imetengeza .
Kasibya EV1 ilikua ya kuogopesha - karibu maili 50 kwa dereva wa kawaida- lakini bwana Willson alivutiwa sana. "Nakumbuka nikidhani hii ndio maisha ya siku za usoni" .
Anasema hatawahi kusahau kauli ya mtangazaji mwenzake wa Top Gear Jeremy Clarkson alipomuonesha gari lake la kwanza la umeme, aina ya Citroen C-Zero, mwongo mmoja baadaye.
"Alisema kwa mshangao: 'umefanya kitu cha ajabu sana na umetuaibisha sisi wote. Ondoka!'," anasema. Ijapokuwa sasa anakiri hangeweza kuwasha sehemu ya kuongeza joto ndani ya gari kwasababu ilipunguza masafa.
Jinsi mambo yalivyobadilika
Bwana Willson anasema anasema hana wasiwasi wowote na gari lake la hivi karibuni la umeme, Model 3 ya Tesla.
Anasema Inaweza kwenda karibu maili 300 kwa betri iliyochajiwa mara moja na intend kasi kwa kati ya 0-60 ndani ya sekunde 3.1.
"Ina starehehesha sana, hewa inaingia vizuri, na ni angavu. Ni raha tu. Naweza kukwambia bila shaka bila shaka kwamba sitawahi kurudi nyuma."
Tumeona maboresho makubwa katika Kigali yanayoendeshwa kwa nguvu za umeme, kompuyuta zinazozielekeza , mfumo wa kuchaji na muundo wa gari.
Lakini mabadiliko ya makubwa yaliyoshuhudiwa na bwana Wilson katika utenda kazi yamewezeshwa pakubwa kwasababu ya maboresho yaliyofanywa katika sauti ya gari na betri.

Chanzo cha picha, Tesla
Mabadiliko makubwa yako kwenye bei.
Muongo mmoja uliopita, iligharimu dola 1,000 kuchaji betri kwa saa moja anasema Madeline Tyson, kutoka shirika la utafiti la kawi safi, RMI lenye makao yake nchini Marekari. Sasa bei imepungua hadi dola 100 (£71).
Hii inaashiria mwanza mpya uliofanya kuwa rahisi kununua magari hayo ukilinganisha na aina nyingine ya magari.
Lakini Bi Tyson anasema, ukizingatia gharama ya mafuta na kuihudumia - EVs hazihitaji vyote hivyo - Tayari magari ya EVs ni bei rahisi ukilinganisha na zile zinazotumia petrol au dizeli.
Huku hayo yakijiri , kuwango cha nguvu inayoweza kupakiwa kwenye kila betri - inaendelea kuongezeka.0
Pia yanadumu kwa muda mrefu.
Mwaka jana gari la kwanza linaloo
Mwaka jana betri ya kwanza duniani inayoweza kuendesha gari kwa maili milioni ilizinduliwwa na mtengenezaji wa betri wa China, CATL.
Makampuni yanayoendesha magari kama Uber na Lyft zinaongoza katika mpango huo, kwasababu gharama yake ni nafuu hasa kwa magari yaliyoendeshwa kwa muda mrefu.
Lakini Bi Tyson anasema, kadri bei inavyoendelea kushuka ndivyo watesha wa reja reja watakavyofuata mkondo hivi karibuni.












