Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

mzozo

Chanzo cha picha, Getty Images

Serikali ya Israel imeapa kulipa kisasi kwa shambulio la kushtukiza la kundi la wanamgambo wa Hamas ambalo ni baya zaidi katika historia ya miongo ya hivi karibuni.

Tayari mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza ambao upo chini ya utawala wa Hamas yamechachamaa. Wakati baadhi ya mataifa yakitaka vita vikomeshwe, Marekani chini ya Rais Joe Biden imekuwa mstari wa mbele kulilaani kundi la Hamas na kuitetea Israel.

Marekani pia kupitia rais wake, pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu ikiwemo waziri wa mambo ya nje na waziri na waziri wa ulinzi imeahidi kuipa Israeli msaada wa aina yoyote katika makabiliano dhidi ya wanamgambo wa Hamas ambao wanawatambua kama kikundi cha kigaidi.

Wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini Marekani katika mzozo huu ama katika machafuko mengine ya nyuma imekuwa ikiegemea zaidi kwa upande wa Israeli.

Katika mzozo wa sasa rais Biden anatumia kauli ambayo marais kadhaa waliomtangulia wa taifa hilo pia walikuwa wakiitumia, nayo ni: "Israel ina haki ya kujilinda". Watetezi wa Palestina na Hamas wanaona kuwa uungwaji huu mkono wa Israeli na taifa la Marekani ndio unaolipa nguvu taifa hilo hata wakati mwengine kukiuka maagizo ya Umoja wa Mataifa. Lakini je, chimbuko la usuhuba baina ya Israeli na Marekani limetoka wapi?

Majibu yapo katika sababu hizi sita:

1.Uhusiano wa karibu wa marais wa Marekani na Israel

Uhusiano kati ya Marekani na Israel ulianza kitambo ,enzi za rais wa zamani Harry Truman ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza duniani kuitambua Israel kama nchi huru mwaka wa 1948 . Truman alikuwa na uhusiano wa karibu na pia mshirika wa kibiashara wa Edward Jacobson ambaye alichangia pakubwa kuisaidia Israel itambuliwe na Marekani.

Tangu Israel ijipe uthabiti wa kijeshi kupitia ushindi wake wa vita vya 1967 dhidi ya nchi za kiarabu kama vile Misri, Syria na Jordan na kuchukua udhibiti wa ardhi kubwa za nchi hizo pamoja na Palestine,Marekani iliboresha kabisa uhusiano wake na nchi hiyo na kuanza kuipa misaada ya kila aina .

2.Misaada ya kifedha na kijeshi kwa Israel

Israel imekuwa ikipewa misaada ya kifedha na Marekania kwa muda mrefu na hilo limekuwa likifanyika tangua vita vya pili vya dunia . kwa mfano mnamo mwaka wa 2016 rais wa Marekani wakati huo Baraack Obama alisaini mkataba wa ulinzi wa Dola bilioni 386 kuisaidia Israel pamoja na ufadhili wa miaka 10 wa mfumo wao wa kulinda dhidi ya makombora wa Irone Dome

mzozo

Chanzo cha picha, Reuters

Licha ya kuwa Israel ni nchi yenye uwezo wa kiuchumi wengi hushangaa mbona Marekani inawapa misaada mikubwa kama huo wa ulinzi . Tayari teknolojia ya Israel imestawi vizuri sana katika sekta zote lakini inazidi kupata usadizi wa kila aina kutoka kwa Marekani .

3.Maoni ya umma

Maoni ya raia wengi nchini Marekani yamekuwa ya kupendelea Israel na hilo ni kwa sababu ya huduma za kampuni za kuboresha uhusiano wa Israel na umma . Israel pia imeweza kupata huruma kutoka kwa Wamarekani kutoka kwa visa kama shambulizi la Munich mwaka wa 1972 ambapo wanaspoti 11 wa Israel waliuawa na makundi ya kipalestina na tukio kama la kutekwa kwa Waisraeli katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda mwaka wa 1976 .

Hata hivyo kulingana na kura mbali mbali za maoni kutoka kwa kampuni ya Gallup,Wamareani pia wameanza kuwahurumia Wapalestina na kufahamu mateso wanayopitia chini ya utawala wa kijeshi wa Israeli . Idadi ya raia ambao bado wanaiunga mkono Israel hata hivyo bado ni kubwa

4.Mashirika yenye ushawishi

Kuna mashirika mbali mbali nchini Marekani ambayo hutetea maslahi ya Israel kwa kila njia na mojawapo ya kundi hilo ni American Israel Public Affairs Committee (AIPAC).

Wanachama wa kundi hilo wanaripotiwa kuwa na ushawishi mkubwa san ahata kisiasa na hupata na kupokea kila aina ya misaada kwa Wayahudi wa kimarekani na makanisa ya kiebanjelisti .

Netanyahu

Chanzo cha picha, Reuters

AIPAC huandaa mkutano wa kila mwaka jijini Washington DC ambao washiriki zaidi ya 20,000 huhudhria n ahata wanasiasa wa Marekani hujitoikeza katika mikutano yake wakiweo marais . Rais wa sasa Joe Biden na rais wa zamani Donald Trump wamewahi kwenda katika mikutano na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni mgeni wa kila mwaka atika kongamano hilo.

5. Ufadhili wa kisiasa

Makundi yanayounga mkono maslahi ya Israeli hutoa mamilioni kwa wagombea wa kisiasa nchini Marekani. Wakati wa kampeni ya 2020, vikundi vinavyounga mkono Israeli vilitoa $ 30.95m, na asilimia 63 ikienda kwa Democrats nayo , asilimia 36 kwa wanachama wa Republican. Hiyo ni karibu mara mbili ya walivyotoa wakati wa kampeni ya 2016, kulingana na OpenSecrets.org.

Wanasiasa wengi katika bunge la Marekani kutoka vyama vya democrat na Republican wanaiunga mkono Israeli.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, Kiongozi wa walio wengi katika Bunge Steny Hoyer na Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer - wote wa Demokrat - wana rekodi ndefu za kuunga mkono Israeli na wanaweza kuhesabiwa kutoa msaada mkubwa kwa haki ya Israeli ya kujilinda wakati wa mizozo.

6. Kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Wayahudi

Hatua ya Marekani chini ya utawala wa rais wa zamani Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel iliwakera sana Wapalestina waliochukulia hatua hiyo kama ushahidi wa wazi kuhusu msimamo wa Marekani kuhusu mateso waliokuwa waipitia chini ya Israel.Mji wa Jerusalem ni muhimu kwa makundi yote mawili yanayozozana na Marekani kujitokezazi kusema kwamba mji huo ni wa Israel ni ishara iliyokuwa ya wazi kwamba Israel walikuwa na mshirika mkubwa sana katika upande wao kwenye mzozo kati yao na Wapalestina .