Fahamu jinsi mwanadamu anavyoweza kuwa mabaki ya kale

Mabaki yoyote yamekuwepo kwa asilimia 0.1 ya mabaki yote ambayo yamewahi kuishi duniani. Lakini ikiwa utaepuka kuzikwa ndani ya jeneza au sanduku, unaweza kuchangia pakubwa kuongeza uwezekano wa upatikanaji wa mabaki ya kale.

Kila mabaki yanayotambulika ni miujiza huwa ni miujiza. Kama Bill Bryson anavyosema katika kitabu chake cha "Historia kidogo ya Karibu kila kitu Duniani," ni mfupa mmoja tu kati ya bilioni utakaopitia mchakato wa kuoza.

Na hiyo ina maanisha kuwa idadi yote ya watu Marekani ambayo ni milioni 320, itakayosalia sio zaidi ya mifupa 60 - takriban robo ya mifupa ya binadamu.

Hata hivyo, ikiwa tutafikiria kuwa mifupa hiyo kidogo inaweza kuzikwa popote pale katika kipande cha ukubwa wa milioni 9.8 kilomita za mraba, uwezekano wa kuwa itapatikana tena ni sifuri.

Hata hivyo sisi wanadamu kuna mengi yanayoweza kutusaidia: tuna mifupa migumu na miili mikubwa na hilo linaongeza fursa ya mwanadamu kuwa mabaki ya kale.

Hilo linawezekana kupitia mchakato wa kuzika, kuoza na kuhifadhi mabaki ya viumbe na yote hayo yanafanyika kiumbe kufariki dunia na hatimaye kuwa mabaki ya kale.

Kujibu maswali kuhusu mchakato wa kuwa mabaki ya kale, BBC Future imezungumza na wataalam kadhaa.

1. Unastahili kuzikwa kwa haraka

"Kwa mabaki kubadilika na kuwa ya kale, mabadiliko ya kimwili na kikemikali yatafanyika chini ya ardhi," anaelezea Sue Birdmore, mtaalamu wa vitu ya kale na msaidizi wa makumbusho ya Kihistoria chuo kikuu cha Oxford.

"Kuwepo kwa miaka milioni lazima mabaki yako yapitie mchakato unaofanyika mtu akishazikwa ambapo hakuna mtu wala chochote kitakacho wasumbua tena," ameongeza Susan Kidwell, Profesa wa chuo kikuu cha Chicago.

Kuzikwa kwa haraka wakati mwingine kunatokana na janga la asili kama vile mafuriko na mlipuko wa volkeno ambako kunafunika mwili wa kiumbe na majivu.

2. Unahitaji maji

Bila shaka hatua ya kwanza ni kufariki dunia lakini cha msingi zaidi ni kuchagua sehemu stahiki. Wataalam wanasema ni vyema kufariki dunia katika sehemu ambayo vifusi vinaweza kuingia kwa haraka chini ya ardhi hadi kwenye miamba. Mfano kwenye ziwa, mto, na chini ya sakafu ya bahari.

Pia inakuwa vizuri zaidi ikiwa eneo lenyewe litakuwa na kiwango cha chini cha oksijeni ambapo wanyama na viumbe vinavyokula mabaki haviwezi kuishi.

"Kwa hiyo, inatakiwa kuwa sehemu tambarare ambayo uchafu unaweza kufyonzwa kwa haraka, hasa penye maji yaliyosimama, pasipo na oksijeni," Profesa Kidwell amesema.

3. Pia utahitajika kutozikwa kwenye jeneza au sanduku

Kawaida, mabaki yote ambayo yamekuwepo kwa takriban miaka 50,000 yanahesabika kuwa yamefikia nusu ya hatua kuitwa ya kale. Tishu za mwili za mabaki kama hayo bado hazijabadilika kabisa.

Hata hivyo kwa mabaki kuendelea kuwepo kwa miaka milioni, lazima madini yaingie hadi kwenye mifupa na kuibadilisha na vitu vizito. Na mchakato huo unaweza kuchukua miaka milioni kadhaa.

Sasa basi, jeneza au sanduku vinaweza kutatiza mchakato huu kwasababu mifupa inaoza haraka maji yenye madini yanapoingia kwa uhuru zaidi ndani yake na kuijaza madini ya chuma na kalisiamu. Kwa upande mwingine, majeneza yanasaidia kuhifadhi mabaki ya mifupa.

Mtaalamu wa mabaki ya vitu vya kale Mike Archer wa chuo kikuu cha New South Wales anatoa suluhisho. Kulingana na yeye, mwili unastahili kuzikwa katika sanduku lililojazwa michanga, huku mamia ya mashimo ya ukubwa wa milimita 5 yalitobolewa kwenye kuta za sanduku.

Na kuzikwa ndani ya kina cha chini zaidi ili maji ya chini ya ardhi yasifike.

Pia kunyunyiza mwili na madini kama vile chokaa ya mawe au chaki kunaweza kuongeza kasi ya mchakato wa uozeshaji.

Michanga ya silikati pia inasemenekana kuwa madini mazuri.

Archer pia anapendekeza kuweka vipande vya shaba na nikeli kando ya mwili. Kisha mifupa na meno iliyo kwenye mchakato wa kuoza itakuwa na rangi nzuri ya buluu na kijani.

4. Epuka kuwa mwisho wa miamba mikuu

Ikiwa umefanikiwa kuendelea kuwepo kwa miaka elfu kadhaa na madini yameanza kuchukua nafasi ya mifupa, hongera, sasa umekuwa mabaki ya kale. Mabaki yataendelea kuingia chini zaidi katika tabaka la juu la dunia, joto na shinikizo vitaongeza kasi ya mchakato wa kuozesha.

Hata hivyo, ni muhimu kutoingia sana ambako kiwango cha joto na shinikizo ni vya juu kwasababu vitafanya mifupa iyeyuke. Na kuepuka hilo, unahitaji kukwepa kuwa mwisho wa miamba mikuu ambako tabaka la juu la dunia hatimaye hufyonzwa.

5. Pia unahitaji kutambuliwa

Pia unastahili kufikiria namna utakavyoweza kubainika siku za usoni.

Kufanikiwa katika hili, unahitajika kutafuta mahali ambako ni tambarare kuweza kuvutia miamba laini itakayozikwa chini zaidi.

Lakini pia, unahitajika kuwa sehemu ambayo inaathirika na mmomonyoko wa udongo ambao hatimaye utasukuma mifupa yako juu ya ardhi.

6. Njia zingine

Kuna njia zingine zinazoweza kusaidia katika mchakato wa kuwa vitu vya kale.

Kwanza ni madini ya kaharabu, jiwe hili linalotokana na utomvu wa mbao ulisaidia kubainika kwa mabaki mengi ya ndege, mijusi na pia mkia wa dinosaria huko Myanmar.

"Ukipata utomvu wa mbao wa kutosha na kuufunika na madini ya kaharabu, hii ndio njia muafaka kabisa ya kuhifadhi mifupa na tishu laini," amesema Caitlin Syme.

Tatizo ni kwamba binadamu ni mkubwa sana kupakwa utomvu wa kwenye mbao na kaharabu.

Njia nyengine ni kutumia mashimo yenye lami ingawa njia hii, mifupa yako inachanganywa na mabaki ya wanyama wengine.

Pia unaweza kuingia kwenye theluji kama ilivyokuwa kwa Etzi, maiti ya kale ya barafu ya mwanamume aliyegunduliwa katika milima ya alps mwaka 1991.

Njia asili za kuhifadhi miili ya waliofariki dunia pia itasaidia ikiwa mwili wako utakuwa kwenye mapango.

"Mabaki mengi ya kale yamepatikana kwenye mapango ambayo hufunikwa kwa kalsiamu ya maji ya chini ya ardhi na kutengeneza mawe ya chokaa ya stalaktiti na stalagmiti," amesema Syme.