Titanic: Utafutaji wa manusura wa China wa ajali ya meli ya Titanic

Ah Lam, Fang Lang and Ling Hee

Chanzo cha picha, LP Films

Maelezo ya picha, Manusura walijumuisha Ah Lam, Fang Lang na Ling Hee

Wakati meli ya kifahari ya Uingereza ya Titanic ilipozama katika Bahari ya Atlantic April 1912, maelfu ya watu walifariki majini.

Moja ya boti za kuokoa maisha ndio pekee iliyofanikiwa kunusurika kwa ajili hiyo na ikarejea kuanza kutafuta manusura. Wakiwa gizani, waokoaji hao walimkuta mwanamume mmoja raia wa China akiwa ameshikilia mlango wa mbao, anatetemeka lakini bado yuko hai.

Mwanamume huyo alikuwa Fang Lang, mmoja wa manusura raia wa China katika meli ya Titanic, na shughuli ya kumuokoa ikachochea pakubwa filamu maarufu mwaka 1997 ya Hollywood.

Lakini kunusurika kwao ambako bado ni miujiza hakukuwa mwisho wao kupitia mitihani ya maisha.

Ndani ya saa 24 baada ya kuwasili kituo cha ukaguzi cha wahamiaji huko kisiwa cha Ellis New York, walifukuzwa nchini humo kwasababu sheria ya China, sheria tata ambayo ilipiga marufuku wahamiaji wa China kuingia Marekani.

Wanaume hao sita wakatoweka katika historia ya dunia hadi sasa. Filamu ambayo ilikuwa ndio imekuwa maarufu China, 'The Six', iliangazia wao ni kina nani na maisha yao, miaka 109 baada ya kutokea kwa ajali ile.

Iliweka wazi simulizi zaidi ya alaji ya Titanic, simulizi iliyoangazia ubaguzi wa rangi na sera ya kupinga uhamiaji ambayo bado inaweza kuakisiwa hadi hii leo kufuatia unyanyasaji wa hivi karibuni wa ubaguzi wa raia wa Asia nchini Marekani.

Je raia sita wa China walionusirika ni kina nani?

Wanaume hao walikuwa Lee Bing, Fang Lang, Chang Chip, Ah Lam, Chung Foo na Ling Hee. Waliaminika kuwa mabaharia ambao walikuwa wanaelekea Caribbean kufanyakazi kazi.

"Kama kundi la watu, hawakuwa wanatambulika," Arthur Jones, mtengezaji wa filamu wa Uingereza na mwelekezi wa filamu ya 'The Six', ameiambia BBC.

Photo shows the ill-fated luxury liner, the Titanic, sailing the ocean

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, The ill-fated Titanic sank in 1912

Majina ya manusura wa China yalikuwa kwenye orodha ya abiria wa meli hiyo, na makala iliyoangazia taarifa za meli ya Titanic mufa mfupi baada ya kuzama.

Lakini tofauti na manusura wengine wa meli ya Titanic ambao walisifiwa na vyombo vya habari, wanaume wa China walikosolewa kwa kauli za kupinga raia wa China Magharibi mapema karne ya 20, kulingana na wanahistoria na watafiti.

Katika taarifa iliyotolewa siku kadhaa baada ya meli hiyo kuzama, kwa mfano, ya 'The Brooklyn Daily Eagle' iliwaita manusura wa China "viumbe" waliorukia boti la kunusuru maisha "baada tu ya kuona ishara ya hatari" na kujificha chini ya viti.

Lakini timu ya utafiti ya makala ile ya 'The Six' ilibaini kuwa madai hayo yalikuwa ya uwongo.

Walijenga mfano wa boti ya kuokoa maisha na kubaini kuwa haingewezekana kwa raia hao wa China kujificha eneo hilo. "Nafikiri ni kitu kile kile tunachokiona leo. Tulibaini kuwa wahamiaji hao walionewa na vyombo vya habari," Bwana Jones amesema.

Vyombo vyengine vya habari wakati huo vilishutumu wanaume wa China kwa kuvaa kama wanawake ili kupewa kipaumbele katika boti za kuokoa maisha.

A single ticket lists the names of the Titanic’s eight Chinese passengers.

Chanzo cha picha, LP Films

Maelezo ya picha, Tiketi moja inaorodhesha majina ya wasafiri wanane wa meli ya Titanic waliokuwa raia wa China - sita kati yao waliponea kifo

Mwanahistoria wa suala la Titanic Tim Maltin amesema hakuna ushahidi kuwa manusura wa China walikuwa ni wahamiaji haramu waliojificha au waliojifanya kuwa ni wanawake.

"Hayo ni baadhi ya yaliyotungwa na vyombo vya habari na umma baada ya kutokea kwa ajali hiyo," alizungumza na BBC.

Uvumi huo huenda chimbuko lake ni unyanyapaa uliotokea kwa manusura wengi wanaume waliokuwa kwenye meli ya Titanic kwasababu wakati huo watu walihisi kuwa wanawake na watoto ndiyo wangepewa kipaumbele katika operesheni ya uokozi.

Meli ya Titanic

Kulingana na Bwana Maltin, wanaume wa China walijitahidi kusaidia manusura.

Fang Lang, mwanamume ambaye alijipiga mijeledi katika mlango uliokuwa unaelea, baadaye alijitokeza katika boti ya uokozi ambayo ilimuokoa yeye na kusaidia kila mmoja aliyekuwepo hadi eneo salama.

Kipi kiliwatokea baada ya ajali?

Baada ya kufukuzwa Marekani, wanaume wale sita walikwenda Cuba. Na kwa haraka wakapata njia ya kufika Uingereza ambako kulikuwa na upungufu wa mabaharia kwasababu mabaharia wengi wa Uingereza walikuwa kwenye jeshi wakati wa Vita vya Kwanza Vya Dunia.

Changa Chip akawa mgonjwa baada ya usiku ule ambao hauwezi kusahaulika na baadaye akafariki dunia mwaka 1914. Alizikwa katika kaburi ambalo halikuwekwa maelezo yake katika makaburi ya London.

Wengine walifanyakazi pamoja huko Uingereza hadi mwaka 1920, nchi hiyo ilipokumbwa na poromoko kubwa la kiuchumi baada ya vita na wahamiaji wakahisi kuwa hali imekuwa ngumu.

Arthur Jones (second from left) leads teams to trace the descendants of these survivors
Maelezo ya picha, Arthur Jones (wa pili kutoka kushoto) aliongoza kundi la kutafuta jamaa wa walionusurika

Wengine wakaoa wanawake wa Uingereza na kuwa na familia. Lakini sera ya kupinga uhamiaji ikawalazimisha kuondoka nchini humo bila kutoa taarifa na kulazimika kuacha nyuma wapendwa wao.

Ah Lam alihamishwa Hong Kong kwa lazima huku Ling Hee akipanda boti hadi Kolkata (Calcutta) nchini India.

Lee Bing alihamia Canada, huku Fang Lang, baada ya kuwa baharia kati ya Uingereza na Hong Kong kwa miaka mingi akawa raia wa nchi ambayo iliwahi kumkataa - Marekani.

Tom Fong knows nothing about his father's experience
Maelezo ya picha, Tom Fong hajui lolote kuhusu kile kilichomfika baba yake

Wakati timu ya utafiti ya filamu ya 'The Six' ilikuwa inafuatilia kujua taarifa za watu hao sita, ikabaini kuwa familia nyingi hazikuwa tayari kuzungumzia ambayo wanaume hao waliyapitia kwasababu ya unyanyapaa wa karne moja iliyopita.

Zaidi ya miaka 100 iliyopita, ukatili waliopitia raia sita wa China manusura wa ajali ya meli ya Titanic bado unashuhudiwa hadi hii leo.