Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda atiwa nguvuni Rwanda baada ya kurejeshwa kutoka Marekani

Chanzo cha picha, RBA/Twitter
- Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili, Kigali
- Muda wa kusoma: Dakika 2
Idara ya Upelelezi wa makosa ya jinai nchini Rwanda imemkamata na kumshikilia Bi Béatrice Munyenyezi mara tu baada ya kusafirishwa hadi mjini Kigali na nchi ya Marekani Ijumaa usiku.
Mume wake Bwana Arsène Shalom Ntahobali na mama mkwe Nyiramasuhuko pia wanazuliwa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na mahakama ya Arusha Tanzania. Mamlaka nchini Rwanda zinasema Bi Munyenyezi anashtakiwa makosa ya mauaji ya kimbari yakiwemo kupanga na kutekeleza mauaji hayo,kuangamiza kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na ubakaji, makosa ambayo anatuhumiwa kufanyia katika mji wa Huye mkoa wa kusini mwa Rwanda.
Shirka la habari la taifa la Rwanda (RBA) limeshirikisha umma picha za tukio la kukamatwa kwa Bi Munyenyezi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kigali:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Munyenyezi, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani na mahakama nchini Marekani kwa kumpata na hatia ya udanganyifu wa kwamba hakuhusika katika mauaji ya kimbari na alipelekwa Rwanda mara tu baada ya kukamilisha hukumu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai Thierry Murangira amesema '' serikali ya Amerika haikupendelea kumbakiza kwenye ardhi yake, ikaona a heri kumrudisha Rwanda, huo ni ujumbe mkubwa''
Alisema ''kumrudisha Rwanda ni kwa manufaa ya sheria kwani tayari alikuwa amefunguliwa mashtaka kutokana na makosa anayotuhumiwa kufanya yenye uhusiano na mauaji ya kimbari''

Chanzo cha picha, RWANDA INVESTIGATION BUREAU
Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 51 na watoto watatu, ambaye alikuwa anaishi Manchester huko New Hampshire, alikamatwa mnamo 2010 kwa madai ya udanganyifu.
Mume wa Munyenyezi Bwana Arsène Shalom Ntahobali na mama mkwe Pauline Nyiramasuhuko, tayari walipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya Arusha.












