Maiti yazuiliwa hospitali kisa 'Hitilafu ya pasipoti'

David Donoghue

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, David Donoghue alikuwa ameishi nchini Thailand kwa miaka 15

Mwanamke ambaye baba yake wa kambo alifariki Thailand wiki mbili zilizopita anasema hospitali imekataa kuachilia maiti yake kutokana na mchanganyiko wa nambari katika pasipoti yake.

Mwili wa David Donoghue, 75, ambaye alihamia Mkoa wa Phuket miaka 15 iliyopita, utachomwa pamoja na miili mingine katika hospitali hiyo siku ya Jumatano ikiwa dosari hiyo haitarekebishwa.

Gemma Swift amesema kuwa "anawasihi" wafanyakazi wa ubalozi nchini Thailand kushughulikia dosari hiyo anayosema ni "suala la kiutawala"

Ofisi ya mambo ya nje imesema maafisa wake wanajaribu kushughulikia suala hilo ili nyaraka sahihi zipatikane.

Bw. Donoghue, ambaye alikuwa akiishi Bury eneo la Manchester kabla ya kuhamia Thailand, aliugua maradhi ya mapafu.

Alipelekwa hospitali nchini humo kwa ambulensi lakini alikuwa na pasipoti ambayo muda wake wa matumizi umemalizika.

Bi Swift, mkazi wa Abergele, kaunti wa Conwy, anasema Bw. Donoghue alifariki hospitali Februari 15.

Gemma Swift
Maelezo ya picha, Gemma Swift anasema hali hiyo imekua ya "kutisha" fkwa familia yake

Hatahivyo, nyaraka sahihi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini humo zinahitajika ili hospitali iachile mwili wake. Maelezo waliyo nayo wahudumu wa hosptali inaonesha pasipoti yake ya sasa.

Kwa kuwa maelezo hayo hayaendani, mwili wake umesalia katika hospitali hiyo kwa siku kadhaa sasa.

Swift,alie na umbri wa miaka 37, anasema hilo ni suala ambalo linaweza kusuluhishwa kwa urahisi akiongeza kuwa familia yake "imetishwa" na hali hiyo.

"Ubalozi wa Uingereza njini Bangkok, unasema kwa sababu [nambari] ilikuwa ya pasipoti ya sasa, haiwezi kubadilisha barua hiyo," aliambia BBC.

"Wamesema hawatatoa barua nyingine kwa kutumia nambari ya pasipoti aliyo nayo hospitalini."

Anasema mpango ulikuwa mwili wake uchomwe Thailand, na sehemu ya majivu yake kurupelekwa Uingereza kisha familia yake irudi Thailand kutawanya majivu yaliosalia kama alivyoelekeza mwenyewe wakati wa uhai wake.

Hakuna hata mmoja wa familia yake aliyefanikiwa kusafiri Thailand kuwa na Bw, Donoghue siku zake za mwisho, na wameshindwa kutatua suala la urasimu kwa sababu ya muda wa siku 14 wa karantini ya Covid nchini Thailand.

'Haki ya kimsingi ya kibinadamu'

Bi Swift anasema eye na familia yake wameshindwa kutatua hali inayowakabili umbali wa maili 6,000.

"Nilidhani ni haki ya kimsingi ya kibinadamu kupewa mwili wa mpendwa wako ukauzike. Nakubali kuna mipaka hatustahili kuvuka…lakini tafadhali naomba mtupatie barua ya kutuwezesha kumleta nyumbani."

Anasema kabla ya jana la Covid-19, familia yake ilikuwa ikimtembelea Bw.Donoghue, ambaye zamani aliwahi kuhudumu kama askari wa Thailand katika kitengo cha watalii.

"Inasikitisha kwamba hakuna hata mmoja wetu alikuwa kando ya kitanda chake wakati alituhitaji," Bi Swift alisema.

David Donoghue with family

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Familia ya David Donoghue wamekua wakimtembelea mara kwa mara nchini Thailand

Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya nje, Jumuiya ya Madola alisema: "Tuanasaidi familia ya Muingereza aliyefariki Thailand na tunawaombea faraja wakati huu mgumu.

"Maafisa wetu wanawasiliana na hospitali hiyo kusiadia familia yake kupata nyaraka zinazohitajika ili iweze kuhifadhi mwili wa mpendwa wao."