Mapinduzi ya Myanmar:Jeshi latanda mitaani, intaneti yazimwa

Armoured vehicles on the streets of Yangon, 14 Feb

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Magari ya kivita yakiwa katika mitaa kadhaa

Magari ya kivita yametanda katika mitaa ya miji kadhaa nchini Myanmar huku kukiwa na ishara kwamba wanajeshi wanaandaa msako dhidi ya wale wanaopinga mapinduzi yaliyofanywa Februari 1.

Mtandao wa interneti umezimwa nchi nzima licha ya juhudi za kimataifa kupinga hatua hiyo.

Katika jimbo la kaskazini la Kachin, vikosi vya usalama vimefyatua risasi katika siku ya tisa ya maandamano ya kupinga mapinduzi nchini kote.

Afisa wa maalum wa umoja wa mataifa nchini humo amewashutumu wanajeshi kwa kile walichokiita kutangaza vita dhidi ya raia wasio na hatia.

Tom Andrews, mwandishi maalum wa umoja wa mataifa kuhusu Myanmar inayojulikana pia kama Burma, amesema majenerali walikuwa wakionesha dalili za kukata tamaa na kuwajibika.

Balozi mbalimbali za nchi za Magharibi zimehimiza jeshi kuonesha weledi wake wakati huu ambapo nchi hiyo ipo katika wakati mgumu.

Kote nchini humo, mamia ya maelfu ya waandamanaji wameendelea kujikusanya katika miji kadhaa ikiwa ni siku ya tisa mfululizo kupinga mapinduzi hayo.

Katika mji wa Myitkyina, katika jimbo la Kachin, risasi zilisikika wakati vikosi vya usalama vikipambana na waandamanaji.

Haikufahamika ikiwa ni risasi za mpira au ama moto zilizotumika kuwatawanyisha waandamanaji hao.

Waandishi wa tano ni miongoni mwa waliokamatwa.

Mapinduzi nchini Myanmar yaliondoa serikali ya raia iliyoongozwa na Aung San Suu Kyi.

Chama chake kilishinda kwa kishindo katika uchaguzi huo mnamo Novemba, lakini wanajeshi walisema ulikua uchaguzi uliojaa ulaghai

Maelezo ya video, Apiga picha akifanya mazoezi bila kujua serikali yake inapinduliwa

Huko Yangon, magari ya jeshi yalionekana kwa mara ya kwanza tangu mapinduzi yaanze.

Jumuiya za kidini na waandisi waliongoza maandamano maeneo hayo , wakati waendesha pikipiki wakiwa wakiendesha katika mitaa ya mji mkuu wa Nay Pyi Taw.

Kampuni za simu nchini humo zimesema mawasiliano ya intaneti yamezimwa kuanzia saa saba mpaka saa tatu majira ya saa za huko.

Daktari mmoja katika hospitali ya Nay Pyi Taw ameiambia BBC kuwa vyombo vya usalama vilikuwa vinawavamia watu nyumbani kwao majira ya usiku.

"Bado nina wasiwasi kwasababu marufuku ya kutotoka nje yapo kuanzia saa mbili mpaka saa kumi alfajiri na ndio muda ambao polisi wanatumia mwanya wa kukamata watu kama sisi," alisema daktari, ambaye jina lake limehifadhiwa kwasababu za usalama.

"Jana waliiba nyumbani kwangu, waliwavamia watu kinyume na sheria, Ndio maana nina wasiwasi."

Afisa wa ubalozi wa Marekani mjini Yangon amewataka raia wa Marekani kutotoka nje wakati huo wa marufuku ya kutoka nje.

Siku ya Jumamosi, jeshi liliwakamata wanaharakati saba wa kampeni za upinzani na kuonya umma kutowasaidia wanaharakati kutoroka ili wasikamatwe.

Picha za Video zikionesha watu wakipiga kelele na kugonga masufuria wakiwaonya jirani zao kuhusu uvamizi wa jeshi majira ya usiku.

Jeshi lilisitisha sheria inayokataza kuzuia mtu zaidi ya saa 24 na kumchunguza maliza zake.

2px presentational grey line

Myanmar -

  • Myanmar, inajulikana pia kama Burma, ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi kuanzia mwaka 1962 mpaka 2011
  • Harakati za ukombozi zilianza mwaka 2010, na kulifanya taifa hilo kuwa na uchaguzi huru mwaka 2015 na mwaka uliofuata serikali ya taifa hilo kuanza kuongozwa na kiongozi nguli wa upinzani Aung San Suu Kyi
  • Mwaka 2017, mgogoro mkubwa uliibuliwa na jeshi la Myanmar katika eneo la waislamu wa Rohingya ambapo mamilioni ya watu walikimbilia mpakani mwa Bangladesh, jambo ambalo baadaye Umoja wa Mataifa UN iliita kuwa "mfano wa kitabu cha utakaso wa ukabila"
  • Aung San Suu Kyi na serikali yake ilipinduliwa na jeshi Februari 1 February kufuatia matokeo ya uchaguzi wa Novemba.