Guinea yarekodi vifo vinavyotokana na Ebola tangu mwaka 2016

Mhudumu wa afya Guinea

Chanzo cha picha, AFP

Takribani watu watatu wamekufa kwa Ebola nchini Guinea, na wengine watano wakipima virusi vya HIV, maafisa wa afya wanasema.

Waliugua kuhara, kutapika na kutokwa na damu baada ya kuhudhuria mazishi.

Kati ya 2013 na 2016 zaidi ya watu 11,000 walifariki kutokana na janga la Ebola Afrika Magharibi, ambayo ilianza Guinea.

Lakini katika kukabiliana na janga hilo chanjo kadhaa zilitengenezwa, ambazo zimetumika kupambana na milipuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ebola huambukiza binadamu kupitia kula wanyama walioambukizwa, kama vile sokwe, popo wa matunda na swala wa msituni.

Halafu huenea kati ya binadamu kwa kupitia damu iliyo na maambukizi, maji ya mwili au viungo, au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia mazingira machafu.

Mazishi ya jumuia, ambapo watu husaidia kuosha mwili wa mtu aliyekufa, inaweza kuwa njia kuu ya kueneza Ebola katika hatua za mwanzo za mlipuko.

Dkt Sakoba Keita, mkuu wa Shirika la Afya la Guinea, amesema majaribio zaidi yanafanywa ili kuthibitisha hali ilivyo katika eneo la Kusini-Mashariki karibu na jiji la Nzérékoré, na wafanyakazi wa afya walikuwa wakifanya kazi kutafuta na kuwatenga wenye maambukizi

Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la Afya Ulimwenguni, Matshidiso Moeti, alituma tweet kuwa shirika hilo "linazidisha juhudi kushughulikia suala hilo" la kuibuka kwa Ebola nchini Guinea.

Map

Chanjo ya Ebola ilijaribiwa kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miezi minne mwaka 2015 huko Guinea - ilianzishwa na Wakala wa Afya ya Umma ya Canada na kisha ikatengenezwa na kampuni ya dawa ya Marekani Merck Sharp & Dohme (MSD).

Wagonjwa 100 waligunduliwa na kisha walikuwa nao karibu walipewa chanjo mara moja, au wiki tatu baadaye. Mwaka 2,014 watu wa karibu walipatiwa chanjo mara moja hakukuwa na maambukizi ya Ebola.

2px presentational grey line

Ebola ni nini?

  • Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
  • Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu.
  • Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola
  • Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukiwa maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.