Mwanafunzi aliyeshuhudia mauaji wakati wa ukoloni Nigeria

Malalamiko kuhusu ukatili wa polisi nchini Nigeria leo yanarejea majibu ya mauaji yaliyotekelezwa na polisi wa kikoloni dhidi ya wafanyakazi waliokuwa kwenye mgomo mnamo 1949 na, kama Nduka Orjinmo wa BBC anavyoripoti, kuna wengine ambao wanaamini kuna uhusiano wa moja kwa moja.
Ikoro iliposikika alasiri ya tarehe 18 Novemba mwaka 1949, mtoto wa shule Godwin Aniagbo alijua kuna kitu kibaya.
Katika jamii ya kitamaduni ya Waigbo, ikoro, ngoma kubwa ya mbao iliyochongwa haswa iliyochongwa kutokana na mti mgumu na mnene wa iroko, ilikaa kabisa katika uwanja wa mji na ilisikika tu wakati wa shida kubwa au kuwaita watu kwenye mkutano muhimu.
Saa kadhaa kabla, wakati alikuwa akirudi kutoka shuleni na marafiki wengine, Bwana Aniagbo alikutana na polisi wa kikoloni wakionekana kama wanatarajia shida.
Kulikuwa na siku kadhaa za mvutano baada ya maandamano katika mgodi wa makaa ya mawe.
''Niliwaona watu wa Magharibi, ( karibu sita) wakiwa wameketi kwenye reli.. wakiwa na silaha.
''Walituita twende kwao lakini tulikuwa tunaogopa kukimbia,'' aliiambia BBC, akikumbuka miaka alipokuwa kijana mdogo.
Muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwake, Bonde la Iva, mjini Enugu, alisikia sauti za risasi kisha ngoma ya Ikoro ikalia.
Polisi wa kikoloni, walioundwa na raia wa Nigeria na wale wa Ulaya, waliwafyatulia risasi wafanyakazi waliokuwa wakidai mazingira mazuri ya kazi katika mgodi wa makaa ya mawe huko bonde la Iva Kusini-Mashariki, ambapo wachimbaji takribani 21 walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa.
''Watu walikuwa wakikimbia kila mahali...wengi ( wa wale waliokuwa wakirejea kutoka kwenye mgodi) walijeruhiwa,'' alisema Bwana Aniagbo, ambaye sasa ana miaka 80.
Shauku kufahamu kilichotokea,

Chanzo cha picha, Joliba Heritage & Culture
Tukio hilo lilisababisha migomo zaidi hasa Kusini mwa Nigeria na baadhi walidai kuwa ilisaidia kuhimili uungwaji mkono wa harakati zinazoendelea za kupinga ukoloni ambazo zilizaa uhuru miaka 11 baadaye.
Wakati wa uchunguzi rasmi , polisi walitetea kitendo hicho kwa kusema kuwa walihofia kuzidiwa.
Lakini miongoni mwa wale walioshutumiwa katika uchunguzi huo walikuwa wakoloni ambao walidaiwa kuchochea hali hiyo. Waliopoteza maisha hivi sasa wanakumbukwa kama mashujaa katika mji huo.

Chanzo cha picha, Centre for Memories
Kile ambacho sasa kinaweza kuwa tukio la kukumbukwa na bado linaangaziwa nchini Nigeria leo.
Licha ya miongo saba, na miaka 60 ya uhuru, kupita tangu mauaji hayo, wengine wanasema kwamba polisi huhifadhi mambo kutoka zamani za kikoloni.
Wimbi la maandamano ya mwaka jana dhidi ya ukatili wa polisi nchini Nigeria chini ya bendera ya #EndSars lilimalizika kwa upigaji risasi mjini Lekki huko Lagos mnamo Oktoba 20, ambayo imesababisha kulinganisha na kile kilichotokea mwaka 1949.
Katika matukio yote mawili waandamanaji wa amani walikabiliana na na nguvu kali, ingawa mamlaka zinaendelea kukana kwamba waandamanaji waliuawa huko Lekki. Amnesty International inasema zaidi ya watu 10 walifariki.
Maandamano yaliongozwa na vijana ambao walifanikiwa kutoa wito wa kuvunjwa kwa kikosi cha Sars, ambacho walikishutumu kutumia vibaya mamlaka yao kwa kuwakamata watu kiholela, kuwadhalilisha na wakati mwingine kuua.
Operesheni ya kukomesha kikosi hicho imedhihirisha kuwepo kwa hali ya kukosa uaminifu kati ya raia na polisi.
Ripoti ya 2004 katika Jarida la Polisi, chapisho la kitaaluma la kimataifa, ilisema taswira ya Umma kwa polisi wa Nigeria wakati huo haikuwa bora kutoka ilivyokuwa wakati na baada ya kipindi cha ukoloni, ikiielezea kuwa bado inafanya kazi "kwa jeuri ileile, ukatili , uharibifu, kutokujali, uwajibikaji mdogo kwa umma na ufisadi ".
Watu wengine, kama Okechukwu Nwanguma wa Noprin, shirika lisilo la kiserikali lililojitolea kufanya mageuzi ya polisi nchini Nigeria, wanaamini kuwa kutokuaminiana kati ya watu na polisi katika nchi nyingi za Afrika ni kwa sababu ya namna vikosi vilivyoanzishwa.
"Jeshi la Polisi la Nigeria, kwa mfano, liliundwa na Waingereza ili kukidhi matakwa ya tabaka tawala na hiyo inaelezea kwanini licha ya Wanigeria kuisimamia tangu mwaka 1964, polisi nchini Nigeria haijawa bora," alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wabunge wanasema sheria mpya inafanya "polisi kuwa bora na inayofaa ambayo inategemea kanuni za uwajibikaji na uwazi, ulinzi wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi; na ushirikiano na taasisi zingine za usalama".
Lakini kitendo cha 2020 kina wakosoaji wake, pamoja na Bw Nwanguma.
Alisema serikali zinazofuatana zimeunda kamati za kuangalia mageuzi ya polisi lakini mapendekezo yao hayajawahi kutekelezwa.
"Kati ya Marais wa zamani Olusegun Obasanjo na Goodluck Jonathan tulikuwa na kamati tatu tofauti - chini ya utawala huu wa Buhari pia tumekuwa nazo lakini hakukuwa na nia ya kisiasa kutekeleza mageuzi makubwa," alisema.
Aliongeza kuwa utashi wa kisiasa unakosa kutekeleza mageuzi kwa sababu wanasiasa wanapendelea polisi jinsi ilivyo ili waweze kuwatumia maafisa kwa malengo yao, "moja ambayo ni kudanganya katika uchaguzi".

Chanzo cha picha, Getty Images
Msemaji wa polisi hakujibu chochote kuhusu suala hilo lakini msemaji wa zamani ambaye sasa anakiongoza chuo cha polisi cha mahusiano ya Umma alikiri kuwa kuna masuala ya kuangaziwa
"Usisahau kwamba polisi wa mwanzo iliyoundwa na mabwana wa kikoloni haikuwa ya kutekeleza haki, nia yao haikuwa kututendea mema, lakini kutufanya mabaya," Emmanuel Ojukwu aliiambia BBC.
Lakini ana imani kwamba mageuzi ya kisheria yatabadilisha kikosi hicho.












