Vifo vya Waafrika mashuhuri 2020: Kutoka rais wa zamani wa Kenya hadi wachezaji soka maarufu

Kutoka kushoto juu hadi kulia: Papa Bouba Diop, Zindzi Mandela, Manu Dibango, Nikita Pearl Waligwa. Chini kutoka kulia: Gita Ramjee, Daniel arap Moi, Hawa Abdi, Richard Maponya, Lina Ben Mhenni,

Chanzo cha picha, Various

Huku mwaka 2020 ukikaribia kukamilika , ni wakati kuwakumbuka baahi ya watu muhimu kutoka barani Afrika waliofariki mwaka huu.

Hapa tunawaangazia watu 10 miongoni mwao ambao tuliwapungia mkono burihani kutoka wachezaji wa kandanda , Wanasayansi, wanamuziki, maafisa wa matibabu , wanasiasa , wanaharakati na wasanii.

Short presentational grey line

Kandanda: Papa Bouba Diop, 42

Mchezaji soka wa Senegalese aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu alituzwa kwa mchezo wake mzuri katika kombe la duniani la 2002 World Cup ambapo alifunga bao lililoipatia ushindi timu yake dhidi ya Ufaransa sula lililosukuma mbele Senegal na kufika robo fainali .

Hakuna timu nyengine ya Afrika ambayo imesonga zaidi ya hapo.

Kilele cha miaka ya mchezo wake ni kushinda kombe la FA akiichezea Portsmouth . Pia aliichezea Fulham , West Ham United , Birmingham City na klabu ya Ufaransa ya Lens.

Papa Bouba Diop

Chanzo cha picha, Getty Images

Pia tuliwapoteza: Leon Mokuna, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mchezaji wa Gambia Alhaji Momodu Njie (maarufu "Biri Biri"), ambao wote walikuwa wachezaji wapya wa Afrika barani Ulaya , kabla ya kumsahau mchezaji wa zamani wa Cameroon Stephen Tataw, ambaye pia aligonga vichwa vya habari katika kombe la dunia.

Sayansi: Gita Ramjee, 63

Mwanasayansi maarufu kote duniani kutoka Uganda alifariki mwezi Machi kutokana na matatizo ya maradhi ya corona.

Alijulikana sana kwa utafiti kuhusu kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa makahaba.

Miaka miwili iliopita alikabidhiwa tuzo ya mwanasayansi bora na shirika la Ulaya la European Development Clinical Trials Partnerships.

Gita Ramjee

Chanzo cha picha, Aurum Institute

Pia tulimpoteza : Simon Mallam, Kiongozi wa tume ya atomiki nchini Nigeria ambaye alifarilki katika mlipuko wa gesi mjini Kaduna.

Mwanamuziki: Manu Dibango, 86

Mpiga Saxafoni huyo kutoka Cameroon alifariki mwezi Machi kutokana na Covid Covid-19.

Alichanganya muziki wa Jazz na ule wa Funk pamoja na sauti ya kitamaduni na alijulikana sana kwa wimbo wake Makosa.

Wakati mmoja aliwasilisha kesi mahakamani 2009 akisema kwamba Michael Jackson alikuwa ameiba mishororo miwili kutoka kwa wimbo huo katika albamu ya Thriller iliouza sana . wawili hao walitatua kesi hiyo nje ya mahakama.

Emmanuel N"Djoke Dibango, maarufu kama Manu Dibango akicheza saxafoni katika hoteli ya Ivory mjini Abidjan 2018

Chanzo cha picha, AFP

Pia tuliwapoteza: Mwanzilishi wa muziki wa Afrobeat Tony Allen, Wanamuziki wakongwe wa DRC wanaopiga muziki wa Lingala Aurlus Mabele na Kasongo wa Kanema, Balla Sidibé, mwanachama mwanzilishi wa kundi la muziki la Senegal Orchestra Baoba, Mfalme wa muziki wa Oud nchini Somalia Ahmed Ismail Hussein Hudeidi, Mkenya John Nzenze, Mwanzilishi wa Ladysmith Black Mambazo Joseph Shabalala, Mwanamuziki wa muziki wa Gospel Kizito Mihigo, Mwanamuziki wa Algeria Hamid Cheriet, ,maarufu kama Idir, mwanamuziki wa Nigerian Majek Fashek na Hachalu Hundessa .

Biashara: Richard Maponya, 99

Mfanyabiashara huyo aliyefariki mwezi Januari , alijulikana kama baba wa black retail nchini Afrika Kusini , akikaidi masharti ya ubaguzi wa rangi na kujenga biashara yake.

Richard Maponya akiwa katikahospitali ya Milpark Hospital mjini Johannesburg, South Afrika tarehe 27 Januari 2011.

Chanzo cha picha, Getty Images

Daktari: Hawa Abdi, 73

Daktari Msomali na mwanaharakati za haki za binadamu , aliyefariki mwezi Agosti alijulikana kama Mama Teresa wa Somalia.

Wakati hospitali yake iliposhambulia 2011 katika eneo la chini la Shabelle na wapiganaji wa Islamic State , alisimama kidete na wapiganaji hao wakajiondoa kufuatia maandamano na mamia ya wanawake .

Hawa Abdi

Chanzo cha picha, Getty Images

Siasa: Daniel arap Moi, 95

Mtu aliyetawala siasa za Kenya kwa zaidi ya robo karne alifariki mwezi Februari .

Alikuwa kiongozi wa Afrika mashariki aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi akiwa rais kutoka 1978 hadi 2002.

Wandanai wake walimsifu kwa kuweka udhabiti nchini humo , lakini wakosoaji wake walisema kwamba aliwakandamiza wapinzani wake na mwaka 2004 aliwaomba msamaha wale aliowakosea.

Daniel arap Moi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Daniel arap Moi served as president from 1978 to 2002

Pia tuliwapoteza : Waziri mkuu wa Ivory Coast Amadou Gon Coulibaly, Ambrose Dlamini, waziri mkuu wa Eswatini, na kiongozi wa Burundi Pierre Nkurunziza . Marais wengine wa zamani waliofariki ni pamoja na Jerry Rawlings wa Ghana, Hosni Mubarak wa Misri, Benjamin Mkapa wa Tanzania, Moussa Traoré wa Mali na Amadou Toumani Touré, Mamadou Tandja Niger, Pierre Buyoya wa Burundi, Jacques Joaquim Yhombi-Opango wa Congo-Brazzaville na aliyekuwa rais wa Mauritania Sidi Ould Cheikh Abdallah. .

Mwanaharakati wa uhaguzi wa rangi : Zindzi Mandela 59

Mwana wa mwisho wa kike wa rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela, alikuwa akihudumu kama balozi wa Denmark wakati alipofariki kutokana na Covid 19 mwezi Julai.

Alikulia wakati wa makabiliano dhidi ya ubaguzi wa rangi na babake alifungwa jela na kuvumilia mateso mengi katika jela la Robben Island na utawala wa ubaguzi.

Mwezi Februari 1985, alisoma pingamizi ya babake baada ya rais wa wakati huo PW Botha kuwasilisha ombi la kumuachilia huru katika mkutano wa hadhara.

Aliendelea na kuwa mwanaharakati akipigania mabadiliko muhimu na hususan yale ya ardhi.

Zindzi Mandela akivalia glavu za ndondi alizopewa na bingwa wa ndondi wakati huo uzani mzito zaidi Mike Tyson kama zawadi akisherehekea miaka 70tarehe 16 Julai 1988 mjini Soweto

Chanzo cha picha, AFP

Sanaa: Nikita Pearl Waligwa, 15

Msanii huyo wa Uganda alifariki mwezi Februari kutokana na uvimbe wa ubongo.

Nyota huyo wa filamu ya Disney ya Queen of Katwe na mchezaji maarufu wa Chess alipatikana na uvimbe huo 2016 na mkurugenzi wa filamu alidaiwa kuwakusanya watu na kuwaomba kumsaidia kupata matibabu nchini India..

Mwaka mmoja baadaye aliambiwa kwamba hana saratani lakini mwaka 2019 alielezewa kwamba alikuwa na uvimbe mwengine.

Picha ya Nikita Pearl Waligwa katika mazishi

Pia tuliwapoteza: Waandishi wawili wa vitabu Nigeria Chukwuemeka Ike na mshairi John Pepper Clark; Mwandishi wa Vitabu vya kiswahili nchini Kenya Ken Walibora, muigizaji maarufu wa Misri Mahmoud Yassine na mpiga picha wa Afrika Kusini Santu Mofokeng.

Mwanaharakati: Lina Ben Mhenni, 36

Mwanablogu huyo wa Tunisian na mwanaharakati wa haki za kibinadamu alifariki mwezi Januari baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kinga wa lupus.

Alikuwa maarufu mapema 2011 kupitia blogu yake Tunsian Girl . Alikuwa miongoni mwa watu wachache kuandika kuhusu maandamano katika eneo la Sidi Bouzid - ambapo maandamano yaliomuangusha rais dikteta Zine el-Abidine Ben Ali began, na kuzua mapinduzi katika eneo lote la Uarabuni .

Mtetezi wa haki za kibinadamu , mwanaharakati wa intaneti na mwanablogu Lina Ben Mhenni

Chanzo cha picha, Getty Images

Athari kubwa : Hachalu Hundessa, 34

Mauaji ya mwanamuziki wa Ethiopia mwezi Juni yalisababisha msururu wa maandamano ya raia , yaliowawacha zaidi ya watu 160 wakiwa wamefariki ikiwemo viongozi maarufu wa upinzani Jawar Mohammed, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Nyimbo za Hechalu ziliangazia haki za watu wa kabila la Oromo , kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia na zilikuwa zikiimbwa sana katika maandamano yaliosababisha kuondoka kwa waziri mkuu aliyeondoka 2018.

Hachalu Hundessa

Pia tuliwapoteza: Rais wa Burundi President Pierre Nkurunziza, ambaye alikuwa madarakani kwa takriban miaka 15 .

Wakati kiongozi huyo wa zamani wa waasi alipochukua madaraka alionekana kupenda kuleta amani , lakini kampeni yake ya kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu 2015 ilizua ghasia .

Alikuwa anajianda kuondoka madarakani ili kuwa kiongozi mkuu .