Shambulio Nigeria: Je utekaji wa wanafunzi wa shule Nigeria ulifanywa na Boko Haram?

A man in Nigeria protesting against Boko Haram

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wananchi wa kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakitoa wito kwa mamlaka zichukue hatua dhidi ya wanamgambo

Tulio la kutekwa wa wanafunzi wa shule katika jimbo la Katsina, Nigeria limefikia kikomo baada ya mamia ya wavulana waliyokuwa wametekwa kuachiwa huru, lakini maswali yanaendelea kuibuliwa kuhusu hatari inayochangiwa na wanamgambo hao katika eneo hilo.

Kundi la kigaidi la Boko Haram limedai kuhusika na shambulio hilo hivi karibuni lililofanyika eneo la kaskazini - magharibi mwa nchi, eneo ambalo halijawahi kuhusishwa na kundi hilo na kuzua hofu huenda ushwishi wao unaendelea kuongezeka.

Hata hivyo, kuna makundi kadhaa yanayohudumu katika eneo hilo, baadhi yametangaza kuwa tiifu kwa uongozi wa Boko Haram.

Katika kipindi cha mwongo mmoja uliyopita, wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha watu katika eneo la kaskazini -mashariki mwa Nigeria hususan katika jimbo la Borno na majimbo jirani.

Ni katika shule ya Chibok, katika jimbo la Borno, ambako mamia ya wasichana walitekwa na wanamgambo wa Boko Haram mwaka 2014 na baadi yao mpaka leo baadhi yao hawajulikani waliko. Utekaji mwingine dhidi ya watoto wa shule ulifanyika mwaka 2018 katika eneo la Yobe, jimbo lingine kaskazini -mashariki.

Hali ya usalama katika eneo la kaskazini -magharibi umekuwa shwari, licha ya visa vya uhalifu vinavyohusishw ana magenge yaliyojihami yanayofahamika kama majambazi, ambo wamekuwa wakiiba mifugo, kufanya bishara ya silaha na kuchungza vijiji.

The rescued boys being returned to Katsina

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wavulana waliotekwa wakirudishwa Katsina

Sasa kuna hofu kwamba Boko Haram inaimarisha ushawishi wake.

"Kitu kinachoshangaza ni kiwango cha oparesheni hii, kwasababu ilizidi kile ambacho kinafanywa na majambazi,"alisema Jacob Zenn, Mhariri wa wakfu wa Jamestownunaofuatilia masuala ya ugaidi.

"Inaonekana kama sehemu ambayo inatumiwa na majambazi kufanya oparesheni zao, mbinu za majambazi [lakini] na kiwango cha Boko Haram na itikadi ya kiongozi wake Abubakar Shekau, "alisema Bw Zenn

Gavana wa Katsina alisisitiza majambazi walihusika na shambulio hilo la hivi karibuni. Ingawa Boko Haram ilichapisha video kwenye mtandao wake ikionyesha wavulana wakiwa wameshikwa mateka.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la AFP iliyonukuu maafisa wa usalama, Boko Haram wamewapa mafunzo makundi ya majambazi katika eneo hilo kuwateka wanafunzi wa shule.

Map

Wakati lilipokuwa hatari zaidi mwaka 2012, kundi hilo lilipanua ushawishi wake katika eneo zima la kaskazini - mashariki mwa Nigeria na kuingi ahadi nchi jirani za Niger na Chad.

Japo sasa kundi hilo linashikilia eno dogo, mashambulio yameendelea kushuhudiwa licha ya madai ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwamba kundi hilo "limesa,baratishwa".

school boys in uniform

Chanzo cha picha, Getty Images

Eneo la kaskazini mashariki kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha ghasia kaskazini mwa nchi. Hali haijabadilika kwa sababu visa vya mashambulio vimeongezeka mwaka huu.

"Ongezeko la vifo kwa kiasi kikubwa linahusiana na uvamizi uliofanikiwa dhidi ya wanajeshi - Boko Haram na Iswap [kikundi kilichojitenga na kikundi cha Dola la Kiislamu], na vile vile mauaji ya raia yanyofanywa na Boko Haram, "alisema Bw Zenn.

Hata hivyo eneo la kaskazini - magharibi pia limeshuhudia ongezeka la ghasia.

Katika miaka michache iliyopita, majimbo ya Zamfara, Katsina na Kaduna yameshuhudia ongezeko la mauaji yaliyohusishwa na makundi yaliyojihami pamoja na ghasia za kisiasa.

Sababu za kukosekana kwa utulivu katika mkoa huo ni ngumu kuelewa.

How violence is increasing in northern Nigeria . Fatalities linked to political violence and armed groups . 2020 data is up until 12 December. North East includes: Adamawa, Borno, Buachi, Gombe, Taraba and Yobe. North West includes: Kaduna, Katsina, Kano, Kebbi, Jigawa, and Sokoto. .

Ripoti iliyochapishwa mwaka huu na kundi la kimataifa la kushughulikia mzozo ilisema "vurugu zimetokana na ushindani juu ya rasilimali kati ya wafugaji wa Fulani walio wengi na wakulima wa Kihausa walio wengi. Hali ambayo imechangia kuongezeka kwa uhalifu uliopangwa, pamoja na wizi wa ng'ombe, utekaji nyara kwa fidia na uvamizi wa kijiji".

Deaths linked to political violence in Katsina, Nigeria . . 2020 data is up until 12 December..

Pia inaripotiwa kuwa makundi ya kijihadi yamekuwa yakitumia nafasi ya kudorora kwa usalama kuendeleaza ajenda zao.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita kumeshuhudiwa ongezeko la makundi yanayojitangaza kuwa tiifu kwa kwa kiongozi wa Boko Haram lkutoka kaskazini- magharibi mwa Nigeria - na Shekau amekiri hilo," alisema Bw. Zenn.

Boko Haram pia iana kundi lililojitenga ambalo linahudumu katika eneo la kaskazini - magharibi, linalojulikana kama Ansaru. Kundi hilo lililo na ufungamano na al-Qaeda limejiimarisha na limefanya mashambulio kadhaa tangu lililobuniwa mwaka 2012.

Je! mkakati wa kijeshi umekuwa upi?

Jeshi la Nigeria limekuwa likijikita zaidi katika mashambulio ya angani yanayolenga ngome za wanamgambo

Akaunti rasmi ya Twitter ya jeshi mara kwa mara huweka kanda ya video na picha, ikidai kuwa imefanikiwa kutokomeza makundi ya majambazi.

Reality Check branding