Shambulio la shule Nigeria: Majambazi waliowateka watoto Katsina 'wazingirwa'

Chanzo cha picha, AMINU BELLO MASARI/TWITTE
Gavana wa jimbo la Katsina ambako watu waliojihami kwa bunduki walivamia shule ya wavulana na kuwashikilia ,Aminu Bello Masari amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa bado hawajaweza kuwapata wanafunzi 333 waliotekwa.
Serikali ya Nigeria ilisema kuwa imewazingira majambazi waliowateka.
Karibuwanafunzi 800 wanasoma katika shule hiyo ya bweni ya wavulana katika jimbo la Katsina na karibu nusu yao hawajulikani waliko.

Chanzo cha picha, Reuters
Inaaminia kuwa washambuliaji walikuwa wanataka kulipwa kikombozi, kulingana na msemaji wa Rais Mahammadu Burari, Garba Shehu .
Serikali imetaja washambuliaji hao kuwa majambazi, jina linalotumika kuashiria genge linalohudumu katika eneo hilo.
Shirika la kutetea haki la Amnesty International linasema watu 1,100 waliuawa na majambazi kaskazini mwa Nigeria katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, lakini serikali imeshindwa kuwachukulia hatua washambuliaji hao.

Chanzo cha picha, Reuters
Mwandishi wa BBC Nigeria Mayeni Jones amesema kumekua na wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.
Eneo la kaskazini - magharibi limeathiriwa zaidi na utekaji wa kutafuta kikombozi, eneo la kaskazini mashariki linahangaishwa na wanamgambo wa Kislamu, huku eneo la kusini likikabiliwa na mashambulio kutoka kwa makundi yanayolenga viwanda vya mafuta vikitaka mgao wa mapato ya mafuta, aliongeza kusema.
Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo iliyopo eneo la Kankara, wakitoa wito kwa mamlaka kuwasaidia kuwapata watoto wao, Shirika la habari la Reuters limeripoti.
Mzazi Abubakar Lawal alinukuliwa kusema kwamba watoto wake watatu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo hawajulikani waliko.
'Majambazi watakabiliwa vikali'
Siku ya Jumamosi, jeshi la nchi hiyo lilisema limegundua maficho ya majambazi hao katika msitu mmoja na kukabiliana nao.
Katika mahojiano ya BBC, Bwana Shehu alisema wanajeshi kadhaa "wamepelekwa" katika eneo hilo kuwakomboa watoto hao.
"Makamanda wa kijeshi wanaoongoza oparesheni hiyo wana taarifa kuhusu ni wapi majambazi hao wanaaminiwa kuwa na wanawazuilia watu wangapi. Wamezingira eneo hilo lote ," aliongeza.
Rais Buhari anatoke jimbo hilo, na kwasasa yuko huko katika ziara ya kibinafsi
Amekuwa akipokea taarifa ya kila baada ya saa kuhusu tukio hilo na juhudi za kuwaokowa wanafunzi waliyotekwa, Bwana Shehu amesema.
"Magenge ya wahalifu na majambazi yatakabiliwa vikali. Yatatokomwezwa," aliongeza.
Wanafunzi wanaamini wanaamini wenzao 10 walichukuliwa na majambazi hao, lakini bado tunajitahidi kuthibitisha hilo, Bwana Shehu aliongeza kusema.
Mamlaka ya shule hiyo inazungumza na wazazi kubaini ni wanafunzi wangapi waliorudi nyumbani na ni wangapi wengine ambao bado wametawanyika katika eneo hilo baaada ya kutoroka shambulio hilo.

Chanzo cha picha, Gail Kankara
Wakazi wanaoishi karibu na shule hiyo wameambia BBC kwamba walisikia milio ya risasi katibu saa tano usiku (22:00 GMT) wa Ijumaa na kwamba mashambulio hayo yalidumu kwa zaidi ya saa moja.
Walinda usalama katika shule hiyo walijaribu kukabiliana na baadhi ya washambuliaji hao kabla ya polisi kufika, amaafisa walisema.
Polisi wanasema wakati wa makabiliano hayo baadhi ya watu hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki walilazimika kurudi nyuma. Wanafunzi walifanikiwa kuruka uwa wa shule na kukimbilia maeneo salama, walisema.

Wakazi kadhaa katika eneo hilo wameungana na polisi katika juhudi za kuwatafuta wanafunzi hao, huku baadhi ya wazazi wakiripotiwa kuwaondoa watoto wao katika shule hiyo.
"Shule imesalia mahame, wanafunzi wote wameondoka," mmoja wa mashuhuda, Nura Abdullahi, aliambia Shirika la habari la AFP.
Gavana wa Katsina, Aminu Bello Massari, ameamuru kufungwa mara moja kwa shule zote za mabweni katika jimbo hilo.












