Uchaguzi Marekani 2020: Saa za lala salama za Trump na Biden

Joe Biden, left, and Donald Trump, right

Chanzo cha picha, Getty/EPA

Rais wa Marekani Donald Trump na mpinzani wake wa Democratic Joe Biden wametumia saa zao za mwisho za mbio za kuelekea Ikulu katika majimbo magumu.

Bwana Biden alifanya kampeni Pennsylvania na Ohio, wakati Bwana Trump akiwa Winsconsin, Michigan, North Carolina na Pennsylvania.

Zaidi ya watu milioni 98 wamepiga kura za mapema, na kuashiria kuwa ni uchaguzi ambao idadi kubwa zaidi kushiriki kuwahi kutokea katika kipindi cha karne moja

Katika uchaguzi wa Marekani, wapigakura huchagua katika ngazi ya majimbo kuliko uchaguzi wa jumla wa kitaifa.

Kuchaguliwa kuwa rais, mgombea anapaswa kushinda takribani kura 270 katika uchaguzi wa mapema kila jimbo nchini Marekani hupata kura fulani kutegemea na idadi ya watu ndani ya jimbo na kuna jumla ya kura 538 za kunyakua.

Mfumo huu unaeleza ni kwa namna gani inavyowezekana kwa mgombea kushinda kwa kura nyingi kwa ngazi ya taifa- kama Hillary Clinton alivyofanya mwaka 2016-lakini bado alipoteza katika uchaguzi huo.

Kura za siku ya jumanne zinakuja wakati taifa hilolikikabiliana na janga la virusi vya corona.

Marekani imerekodi idadi zaidi ya watu walioambukizwa na hata vifo kuliko nchi nyingine yoyote ulimwenguni, ikiripoti maambukizi mapya kwa watu 81,000 siku ya Jumapili pekee.

Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza nchini humo, Dkt Anthony Fauci amekosoa vikali utawala wa Trump namna unavyoshughulikia janga hilo.

Businesses in New York City are boarding up their shop fronts in case of post-election unrest

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati taifa linapohesabu saa za kupiga kura, kuna hofu kwamba vurugu za baada ya uchaguzi zinaweza kutokea.

Wafanyabiashara katika mji mkuu wa taifa hilo, Washington DC, na katika Jiji la New York wameonekana kuimarisha usalama katika majengo yao kutokana na wasiwasi kuhusu vurugu.

Wakati huo huo shirika la upelelezi, FBI limesema linafanya uchubguzi baada ya msafara wa magari yenye bendera za Trump kuzunguka basi lililowabeba wafanyakazi wa kampeni za Biden mjini Texas juma lililopita.

Mr Trump addressed a re-scheduled campaign rally in Fayetteville Regional Airport, North Carolina

Chanzo cha picha, Getty Images

Kampeni za mwisho za Biden na Trump

Baada ya ratiba ya mikutani katika majimbo sita siku ya Jumapili, Rais Trump alikuwa na kibarua kingine katika majimbo mengine manne siku ya Jumatatu.

Akiwa North Carolina, aliwaambia wafuasi kuwa ''mwakani utakuwa mwaka bora wa kiuchumi katika historia ya nchi yetu''. Mkutano uliahirishwa siku ya Alhamisi kutokana na kimbunga Zeta

Mr Biden made a last-minute campaign stop for a drive-in rally in Ohio

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mr Biden made a last-minute campaign stop for a drive-in rally in Ohio

Wachumi wanatahadharisha kuharibiwa kwa uchumi kutokana na janga la virusi vya corona- changamoto kubwa kuikumba Marekani kwa zaidi ya miaka 80- changamoto ambayo inaweza kuchukua miaka kuikabili.

Baada ya North Carolina, Bwana Trumo alielekea Scranton, Pennsylvania, mji ambao hasimu wake alikuwa akiishi mpaka alipotimiza miaka 20. Katika mkutano aliwakumbusha wafuasi wake kuwa alishinda jimbo hilo mwaka 2016 pamoja na kuwa kura za awali zilionesha ataanguka katika uchaguzi huo.

Bwana Biden pia alikwenda Pennsylvania ambako mwanamuziki Lady Gaga alijiunga naye katika mkutano huko Pittsburgh. Mwanamuziki John Legend alihutubia wapiga kura sambamba na mgombea wa nafasi ya makamu wa rais Kamala Harris.

Katika dakika za mwisho kampeni ziligotea Ohio, Bwana Biden alirejea ujumbe wake wa msingi wa kampeni zake, akiwaeleza wapiga kura kuwa kinya'ng'anyiro hicho kinahusu uhai wa Marekani.

Alisema ni muda wa Trumo '' kufungasha virago'', alisema ''tumechoshwa na machapisho yake ya mtamdao wa twitter, hasira, chuki na kushindwa, kushindwa kuwajibika''.

Joe Biden in Pennsylvania

Chanzo cha picha, Reuters

Mbio hizi ni ngumu sana katika jimbo la Ohio. Mwaka 2016, Trump alishinda kwa zaidi ya alama nane-kwa sasa ana 0.2% akiongoza dhidi ya Biden, kwa mujibu wa RealClear Politics.

Pia siku ya Jumatatu Trump alifanya mikutano mji wa Traverse, Michigan na Kenosha, Wisconsin. Kenosha ulikumbwa na maandamano mwezi Agosti baada ya polisi kumfyatulia risasi mwanaume mweusi.

Mjini Traverse aliomba kura kwa wa wapigakura weusi.

Mkutano wake wa mwisho utafanyika Grand Rapids, Michigan, kabla ya saa sita usiku.

Siku ya Jumapili wagombea hao walishambuliana kuhusu masuala muhimu katika kampeni hizo- Covid -19 na masuala ya rangi.

Rais na kampeni yake wakati huo huo wameonesha watashtaki kuzuia jimbo muhimu la Pennsylvania kuhesabu kura za posta zilizopokelewa siku tatu baada ya uchaguzi.

Korti Kuu ya Marekani iliruhusu uamuzi wa mahakama ya chini kutoa muda zaidi, lakini majaji kadhaa wa kihafidhina walionesha kwamba wangekuwa tayari kutazama tena suala hilo baada ya kupiga kura.

Bwana Trump aliandika katika mtandao wa twitter kuwa uamuzi wa mahakama ya juu kuruhusu kura kupokelewa siku tatu baada ya uchaguzi ni ''suala la hatari''

Donald Trump in Michigan ahead of the election

Chanzo cha picha, EPA

"Itaruhusu udanganyifu uliokithiri na usiodhibitiwa na itadhoofisha mifumo yetu yote ya sheria. Pia itasababisha vurugu mitaani. Kitu lazima kifanyike!" Twitter iliongeza ujumbe wa onyo kuwa ujumbe huo unaweza kuwa na habari "za kupotosha".

Mapigano ya kisheria kuhusu kura pia yamekuwa yakijitokeza huko Minnesota, North Carolina na Texas.

Bwana Biden tayari ameapa kumzuia Rais Trump "kuiba" uchaguzi huo.

Rais Trump anatarajiwa kuhodhi sherehe ya usiku wa uchaguzi ndani ya ikulu, wageni karibu 400 wakiwa wamealikwa.

Karibu waandamanaji 10,000 wanatarajiwa kukutana katika jengo la Black Lives Matter na eneo la bustani si mbali na ikulu, kwa mujibu wa CBS News.

Bwana Biden na Bi Harris wataangalia usiku wa uchaguzi katika mji wa makamu wa zamani wa rais wa Wilmington, Delaware.

Presentational white space

Wagombea hawa wanatofautiana kwenye masuala yapi na wameahidi nini?

Mahasimu hawa wana sera tofauti katika masuala muhimu.

Kuhusu mlipuko wa virusi vya corona, Trump aliunda kikosi kazi mwezi Januari ambacho amesema sasa kimebadilisha uelekeo '' kwenye usalama na kufungua uchumi wa Marekani''.

Rais pia ameweka kipaumbele jitihada za kupata tiba na chanjo ya Covid, akitenga kiasi cha dola bilioni 10 kwa ajili ya miradi hiyo.

Bwana Biden anataka kutengeneza mfumo wa kuwatafuta watu waliokutana na watu waliopata maambukizi, kuanzisha takribani vituo kumi vya kufanya vipimo kila jimbo, na kutoa huduma za kupima virusi vya corona bure kwa wote.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Trump amesisitiza kuondoka katika mkataba wa Paris.

Biden amesema yeye atarejea katika mkataba wa Paris na pia anataka Marekani kuondoka katika orodha ya wachangiaji katika utoaji wa hewa chafu ifikapo mwaka 2050.

Kuhusu uchumi, Trump ameahidi kubuni ajira milioni 10 katika kipindi cha miezi 10, pia biashara ndogondogo milioni moja.

Bwana Biden anataka kuongeza kodi kwa wale wanaopata zaidi kulipia uwekezaji kwenye huduma za Umma , lakini amesema kuwa ongezeko hilo litawahusu wale wanaopata zaidi ya dola 400,000 kwa mwaka.

Footer - Blue