Sergei Torop: Kiongozi wa madhehebu ya kidini wa Urusi akamatwa kwa tuhuma za kuwadhuru watu

Kiongozi wa madhebebu maarufu ya kidini amekamatwa na vikozi vya usalama vya Urusi katika maeneo ya vijijini ya Siberia, polisi wamesema.

Sergei Torop, ambaye anafamika miongoni mwa wafuasi wake kama Vissarion, alianzisha kanisa la Agano la Mwisho- Last Testament - katika jimbo la Siberia la Krasnoyarsk mwaka 1991.

Amekamata pamoja na viongozi wengine wawili wa kikundi hicho.

Wanashutumiwa kwa kuchukua fedha kwa nguvu na vitisho pamoja na kusababisha madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa wafuasi wao.

Bwana Torop, Vadim Redkin na Vladimir Vedernikov wanashukiwa kwa " shirika la dini ambalo shughuli zake zinahusisha ghasia dhidi ya watu binafsi na kusababisha madhara ya mwili kwa watu wawili au zaidi ," amesema msemaji wa kamati ya uchunguzi ya Urusi.

"Walitumia fedha za wafuasi wao na kuwanyanyasa kisaikolojia ," alinukuliwa akisema kwenye vyombo vya habari vya taifa.

Bwana Torop, mwenye umri wa miaka 59- zamani akiwa askari wa usalama barabrani, ameripotiwa kuwavutia maelfu ya wafuasi tangu alipoanzisha kikundi hicho cha kidini baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti . Baadhi wanasemekana kuamini kuwa kutakuwa na kuzaliwa upya kwa Yesu kristo.

Alikamatwa na vikosi vya usalama kufuatia msako maalumu uliofanyika Jumanne dhidi yake, na video iliyooneshwa kwenye televisheni ya Urusi ambayo ilionesha mwanaume aliyeonekana mchovu akiwaongoza wanaume wawili ndani ya helikopta.

Mmoja w wakati wa eneo hilo aliandika kwenye ukurasa wa Facebook kwamba helikopta nne na makumi kadhaa ya watu waliofunika nyuso zao waliwasili katika eneo hilokabla ya kuanza msako katika nyumba jirani pamoja na na majengo.

Wafuasi wa kanisa la Agano la mwisho-Last Testament walipata makazi katika mji unaoitwa City of the Sun, (mji wa Jua) katika jimbo la Kuraga la Siberia mwaka 1995. Wafuasi kadhaa wanaishi katika makazi mengine katika jimbo hilo.

MwakA2000, wizara ya sheria nchini Urusi ilisema madhehebu yake yana ufuasi wa watu 10,000 kote duniani.

Wafuasi wake hawatakiwi kuvuta sigara, kunywa pombe , kubadilisha pesa, na wanapaswa kuishi maisha ya kawaida. Wanaoamini mafundisho ya Bwana Torop hawapaswi kula nyama, kunywa kahawa, chai, sukari, mikate yenye chachu na bidhaa zote za ngano, Imeripoti Idhaa ya BBC ya lugha ya Kirusi.

Kikuni hicho kinajumuisha mafundisho ya kanisa la Kiothordox la Urusi na mada za kuzaliwa tena kwa Yesu Kristo, pamoja na maandalizi ya dhana ya misho wa dunia unaotabiriwa utakaosababisha maasi na kuangamia kwa dunia maarufu kama Marmageddon.