Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Ibrahim Boubacar Keïta: Maelfu ya waandamanaji watoa wito kwa rais wa Mali kujiuzulu
Maelfu ya waandamanaji nchini Mali wamekusanyika katika mji mkuu wa Bamako, wakitaka rais ajiuzulu.
Umati huo ukiongozwa na imam Mahmoud Dicko na muungano wa makundi ya upinzani unataka mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa.
Wanataka kujiuzulu kwa rais Ibrahim Boubacar Keïta kutokana na kuongezeka kwa makundi ya kijihadi na ghasia za wenyewe kwa wenyewe.
Rais alihaidi kuunda serikali mpya ikiwa na wanachama wa upinzani.
Lakini licha ya makubaliano hayo ya pande mbili , mapema wiki hii , maandamano hayo yamefanyika kama yalivyopangwa.
Siku ya Ijumaa, makundi ya watu yalikusanyika katika bustani ya uhuru iliopo Bamako, wakiimba nyimbo dhidi ya serikali na kubeba mabango yalioandikwa jumbe dhidi ya serikali . Barua imetumwa kwa rais na makundi ya upinzani wakitaka ajiuzu.
Bwana Dicko aliongoza maombi wakati wa mkutano huo wa hadhara. Mwanasiasa wa upinzani Cheick Oumar Sissoko alitoa hotuba kwa kuwataka raia kutotii hadi bwana Keïta atakapoachia ngazi, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters.
Mkusanyiko wa namna hiyo ulitokea Juni 5, ambao uliandaliwa na makundi hayo hayo. Kundi hilo ambalo limepata jina la Movement of 5 June - Rally of Patriotic Forces".{ Vuguvugu la juni 5 - mkutano wa vikosi vya kizalendo.
Bwana Keïta, ambaye ana umri wa miaka 75 na anajulikana kama IBK, alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa katika mataifa ya magharibi mwa Afrika mwaka 2013. Na akarejea kwenye wadhifa huo katika uchaguzi wa muhula wa pili wa miaka mitano mwaka 2018.
Lakini amepata shinikizo kali sihaba kutokana na uchumi wa Mali kushuka, janga la virusi vya corona na mgomo wa walimu.
Mvutano wa kisiasa pia umeongezeka kufuatia uchaguzi wa ubunge uliozongwa na utata mnamo mwezi Machi pamoja na kuwepo kwa madai ya rushwa.
Mali limezongwa na ukosefu wa utulivu tangu mwaka 2012, wakati ambapo makundi ya Kiislamu ambayo yanachochewa na waandamanaji wa Tuareg kuvamia ukanda wa kaskazini. Lakini mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali na walinda Amani wa Umoja wa mataifa yanaendelea.
Siku za hivi karibuni, rais alikubaliana na makundi ya upinzani kuongeza fedha kwa ajili ya walimu wa shule za umma kufuatia mgomo waliouanzisha kutokana na malipo.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Ecowas ya ukanda wa mataifa ya magharibi umetaka pande hizo mbili kuafikia maridhiano.
Lakini waandamanaji wanasema , hakuna kilichofanywa kukabiliana na rushwa na kuanguka kwa uchumi.