Virusi vya Corona: Je, corona imedhibitiwa Afrika ama kuna walakini wa takwimu?

Medical staff at the Chandaria Health Centre try on face shields in Nairobi, Kenya - 14 May 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 9

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba karibia robo ya watu bilioni moja Afrika huenda wakaambukizwa virusi vya corona mwaka wa kwanza wa janga la corona huku kati ya watu 150,000 na 190,000 wakiaga dunia.

Afrika ina chini ya watu 100,000 walioambukizwa hadi kufikia sasa lakini watalaamu wanaamini kwamba bara hilo litakuwa na mlipuko huo kwa kipindi kirefu cha miaka kadhaa na angalizo kubwa la kudhibiti virusi kumesababisha kupuuzwa kwa matatizo mengine ya afya.

Hapa, wanahabari watano wa BBC wanagusia kile kinachotokea katika nchi zao.

Huenda Congo ilikuwa imepata virusi hivyo hata bila kujua

Short presentational grey line

'Huenda raia wa Congo walikuwa wamepata virusi hivyo hata bila kuju'

Na Emery Makumeno, Kinshasa

A staff member of the Congolese Ministry of Health prepares the sampling equipment to perform a COVID-19 test at a private residence in Goma, northeastern Democratic Republic of Congo, on March 31, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, DR Congo inapambana na mzigo mkubwa wa corona

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19 mapema Machi lakini daktari katika mji mkuu wa Kinshasa anaamini kwamba ugonjwa huo uliingia mapema kabla ya kugunduliwa.

"Desemba na Januari, siwezi kukumbuka ni wagonjwa wangapi waliokuja kupata matibabu, lakini walikuwa na matatizo ya kukohoa, homa na vichwa kuuma," amesema, akirejelelea dalili za ugonjwa wa Covid-19 zilizoorodheshwa na WHO.

"Ninaamini kwamba wahudumu wa afya tayari walikuwa wako katika hatari ya kupata maambukizi bila hata kujua," aliongeza.

Lakini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepima watu kadhaa kuangalia hali ya ugonjwa wa virusi vya corona kwasababu ya ukosefu wa vifaa vya matibabu.

Nchi zenye mikakati mizuri ya kukabiliana na virusi vya corona, Korea Kusini na Ujerumani zimefanikiwa kupima virusi vya corona kwa angalau asilimia 1 ya idadi ya watu, kulingana na Jarida la matibabu la Uingereza la The Lancet.

Ikiwa vifaa vinapatikana, mataifa mengi ya Afrika huenda yakaimarisha upimaji - zilifanya vipimo vingi vya ugonjwa wa ukimwi kati ya Oktoba mosi na Desemba 31 kuliko lengo la asilimia 1 la kupima ugonjwa wa Covid-19, jarida la Lancet limesema.

Presentational grey line
  • Vipimo vya Covid-19 vilivyofanywa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufikia Mei 18: 4,493.
  • Vipimo vinahitajika kufanywa angalau asilimia 1 ya idadi ya watu: 895,614
  • Vipimo vya ukimwi kuanzia Oktoba mosi hadi Desemba 31, 2019: 203,859

Chanzo: Africa CDC; The Lancet

Presentational grey line

Hadi kufikia sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imerekodi zaidi ya waathirika 1,600 wa virusi - nchi hiyo ikiwa ni ya tisa kati ya zile zilizo na maambukizi ya juu zaidi barani Afrika, kulingana na WHO.

Mwaathirika wa kwanza wa Covid-19 aligunduliwa huko La Gombe, eneo kubwa la kibiashara Kinshasa. Serikali hiyo ilichukua hatua haraka ya kusalia ndani lakini tangu wakati huo, virusi hivyo vimesambaa katika majimbo 7 kwenye nchi hiyo yenye majimbo 26 - ikiwemo eneo ambalo ni kitovu cha uchimbaji wa madini la Lubumbashi.

Mlipuko huo unawadia wakati ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - ambayo ina mfumo dhaifu wa afya pia imekumbwa na migogoro upande wa mashariki mwa nchi hiyo kwa miongo kadhaa - na inapitia wakati mgumu kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 2000 tangu 2018.

Shirika la Umoja wa Mataifa, Unicef, pia limeonyesha wasiwasi wake kuhusu kupungua kwa kiwango cha chanjo inayotolewa, likisema kwamba faida zinazotokana na chanjo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita huenda ikapotea.

Children wait to be registered before a measles vaccination at a centre in Mbata-Siala, near Seke Banza, western DR Congo on March 3, 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images

Shirika la Unicef limesema, chanjo zinazotolewa zilikuwa tayari zimeanza kupungua kuanzia mwanzoni mwa mwaka na athari ya virusi vya corona huenda kukafanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi.

Mamia na maelfu ya watoto bado hawajapokea chanjo ya ugonjwa wa kupooza yaani polio, ukambi au surua, homa ya njano na chacho zenginezo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda ikapoteza ile hadhi yake ya kutokuwa na ugonjwa wa kupooza na kuchipuka kwa magonjwa mengine hatari.

Wafanyakazi wa afya wanakosa vifaa vya kujikinga wenyewe au watoto wao kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na wazazi wana hofu ya kuwapeleka katika vituo vya chanjo.

Short presentational grey line

Hospitali za Kenya zina wagonjwa wachache lakini maiti ni nyingi'

Na Mercy Juma, Nairobi

A barber tends to a client while wearing personal protective equipment (PPE) donated by a local youth group comprised of some entrepreneurs who have lost their livelihoods due to the economic slump caused by countrywide restrictions imposed on movement of people and goods, in a bid to curb the spread of the COVID-19 coronavirus, who manufacture personal protective equipment (PPE) in a shed in Waithaka, a suburb of Nairobi on May 14, 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kufunika uso limekuwa jambo la kawaida sasa Kenya

Hospitali kuu ya umma nchini Kenya katika mji mkuu Nairobi, imekuwa na ongezeko la maambukizi kwa karibu asilimia 40 kwa magonjwa wenye matatizo ya kupumua kama vile kifua kikuu, homa ya mapafu na asthma kati ya Desemba na mapema Machi, daktari mmoja amezungumza na BBC.

Hata hivyo, visa hivyo vimepungua sana tangu katikati ya Machi, kulingana na daktari huyo aliyezungumza na BBC kwa masharti ya kuficha jina lake kwasababu hana mamkala ya kuzungumza na vyombo vya habari, aliongeza.

Moja ya sababu ni kwamba serikali ilikuwa imeweka marufuku ya kutotoka nje kuanzia usiku hadi asubuhi ili kudhibiti usambaaji wa maambukizi ya virusi vya corona.

Hilo limechangia kupungua kwa idadi ya watu wanaolazwa hospitali usiku lakini idadi ya wanaokufa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti imeongezeka, daktari huyo amesema.

Someone in quarantine in Kenya holding up a "Please help us" sign - April 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu walihangaika sana kutaka kutoka karantini

Pia inaonekana watu wanaogopa kwenda hospitali kwa hofu ya kupimwa ugonjwa wa Covid -19 na kupelekwa katika vituo vya karantini, alisema.

Hii ni kwasababu kuwekwa karantini ni jambo ambalo nchini Kenya limezua utata, huku serikali ikilazimisha wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na Covid -19 kujilipia gharama zao.

Gharama hiyo ni kati ya $20 (£16) hadi $100 kwa usiku mmoja, kulingana na kituo ulichopelekwa ingawa sasa hivi serikali imeahidi kusimamia gharama kwa watakaokuwa katika vituo vya karantini vya umma.

Presentational grey line
  • Idadi ya waliopimwa Covid-19 nchini Kenya kufikia Mei 18: 44,851
  • Idadi ya waliopimwa inahitajika kuwa asilimia 1 ya idadi ya watu: 537,713
  • Waliopimwa ukimwi kuwanzia Oktoba mosi hadi Desemba 31, 2019: 2, 177,170

Chanzo: Africa CDC; The Lancet

Presentational grey line

Mabweni shuleni na vyuo vikuu pamoja na hoteli za kibinafsi vimekuwa vikitumika kama vituo vya karantini.

Mwezi uliopita, kuna video iliyosambaa mtandaoni ikonesha vile watu kadhaa wanavyoruka ukuta kutoroka kituo cha karantini mjini Nairobi.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational grey line

Walio kwenye karantini wamelalamika kwamba baadhi ya vituo ni kheri magereza kwasababu ya usafi duni na mrundiko wa watu na kufanya iwe vigumu kutekeleza hatua ya kutokaribiana.

Short presentational grey line

'Wagonjwa wengi na maiti nyingi'M kaskazini mwa Nigeria

Na Ishaq Khalid, Abuja

A patient who is suspected of suffering from COVID-19 coronavirus undergoes testing at the University of Maiduguri Teaching Hospital isolation centre on May 10, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Upimaji wa corona unafanyika kwa kiwango duni Nigeria

Kumekuwa na taarifa za watu wengi zaidi kuugua na kufa katika jimbo la Kano lenye watu wengi nchini Nigeria tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona karibia miezi mitatu iliyopita.

Kwahiyo si jambo la kushangaza kuona Rais Muhammadu Buhari akiendeleza hatua ya kusalia ndani kwenye jimbo hilo la kaskazini hadi mwisho wa mwezi huu.

Mchimbaji makaburi katika makaburi ya Abattoir kwenye mji mkuu ambako pia kunafahamika kama Kano, aliiambia BBC: "Hatujawahi kushuhudia vifo vingi kiasi hichi tangu kutokea kwa mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa kipindu pindu tulikoelezewa na wazazi wetu. Hiyo ilikuwa ni miaka 60 iliyopita."

Profesa Musa Baba-Shani - mkuu wa idara ya matibabu katika hospitali ya chuo cha Aminu Kano, hospitali kuu kweye jimbo hilo - ameiambia BBC kwamba wamekuwa wakitibu wagonjwa zaidi wenye magonjwa yanaofungamana na asthama, homa ya mapafu na kifua kikuu pamoja na maumivu ya kifua na koo.

Profesa ambaye anafanyakazi katika kitengo cha magonjwa ya kupumua kwenye hospitali hiyo alisema kumekuwa na ongezeko la kati ya asilimia 40 na 45 kwa idadi ya visa vya magonjwa ya kupumua mwezi uliopita.

Taxi in Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kujitenga kati ya mtu na mtu pia bado ni changamoto kwa Nigeria

Pia alizungumzia kufungwa kwa hospitali nyingi katika jimbo hilo hasa kliniki za kibinafsi kwasababu ya ukosefu wa nguo za kujikinga kwa wahudumu wa afya. Hilo limesababisha wagonjwa zaidi kutafuta matibabu katika hospitali ya Aminu Kano.

Profesa Baba-Shani alisema baadhi ya wenye matatizo ya kupumua walipatikana na ugonjwa wa virusi vya corona na kupelekwa katika vituo vilivyotengewa wagonjwa wa Covid-19.

Profesa huyo pia alikosoa kasi ya chini ya upimaji virusi vya corona katika nchi hiyo ya Afrika yenye idadi kubwa ya watu ambao ni karibia milioni 200. Itakuwa vizuri kwa wagonjwa na hospitali ikiwa kasi ya upimaji ingeongezeka, alisema.

Presentational grey line
  • Idadi ya waliopata Covid -19 nchini Nigeria kufikia Mei 18: 33,970
  • Wanaohitajika kupimwa ni asilimia 1 ya idadi yote: 2,061,396
  • Vipimo vya ugonjwa wa ukimwi kuanzia Oktoba 1 hadi Desemba 31 2019: 1,160,920

Chanzo: Africa CDC; The Lancet

Presentational grey line

Daktari mwengine kutoka hospitali hiyohiyo ambaye hakutaka kutajwa kwasababu hakuwa na idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari alisema baadhi ya watu walikuwa wanakwepa kupata matibabu kwasababu wanaogopoa kupata maambukizi wakiwa hospitali.

Kaskazini mashariki mwa jimbo la Yobe, idadi isiyo ya kawaida ya watu 471 wameaga dunia katika kipindi cha wiki tano zilizopita.

Bado haijafahamika ikiwa vifo hivyo vinahusiana na virusi vya corona lakini afisa wa tume ya afya nchini humo, Dkt. Muhammad Lawan Gana ameiambia BBC kwamba uchunguzi wa awali ulibaini kuwa idadi kubwa ya waliokufa walikuwa wazee wenye matatizo mengine ya afya kama vile shinikizo la juu la damu na ugonjwa wa kisukari.

Nigeria imethibitisha zaidi ya waathirika 6,000 wa virusi vya corona ikiwa ni ya tatu kwa ukubwa Afrika.

Mji mkuu wa kibiashara wa Lagos, ndio kitovu cha mlipuko huo lakini hatua ya kusalia ndani iliyowekwa mwishoni mwa Machi imelegezwa kiasi, na kuzua hofu ya kusambaa zaidi kwa virusi.

"Ni uamuzi mgumu lakini nadhani haikuwa jambo sahihi," amesema Dkt. Andrew Iroemeh, anayefanyakazi katika kituo cha Covid-19 mjini humo.

"Inapendekezwa kwamba kwa hatua ya kusalia ndani kulegezwa tunastahili kuwa na kiwango cha chini cha maambukizi kufuatana kwa angalau siku 14. Hali hiyo bado halijashuhudiwa," aliongeza

Short presentational grey line

'Dalili chache za virusi' Ethiopia

Na Kalkidan Yibelta, Addis Ababa

Health Extension workers of the Ministry of Health measure the tempreature of a girl during a door to door screening to curb the spread of the COVID-19 coronavirus in Addis Ababa, Ethiopia, on April 20, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ethiopia imepiga marufuku mkusanyiko wowote wa zaidi ya watu wanne

Maambukizi ya mfumo wa kupumua ni jambo la kawaida nchini Ethiopia, nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani humo ikiwa na watu zaidi ya milioni 100. Utafiti unaonesha maambukizi hayo ni ya tatu kwa idadi ya vifo kila mwaka baada ya vifo vya watoto wadogo na magonjwa ya kuharisha.

Mlipuko wa virusi vya corona hauonekani kama uliosababisha wagonjwa wengi kuwa na maambukizi ya matatizo ya kupumua ambao wanalazwa hospitalini katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita.

Daktari katika mji mkuu wa Addis Ababa, ameiambia BBC kwamba alikuwa anaangalia ishara za dalili za ugonjwa wa Covid-19 lakini hakuona chochote.

Presentational grey line
  • Idadi ya waliopimwa Covid-19 nchini Ethiopia kufikia Mei 18: 59,029
  • Asilimia moja ya watu ambao wanastahili kupimwa ni: 1,149,636
  • Upimaji wa virusi vya ukimwi kuanzia Oktoba Mosi hadi Desemba 31 2019: 136,307

Chanzo: Africa CDC; The Lancet

Presentational grey line

Kwa mfano, hakukuwa na ongezeko la maambukizi kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya mapafu waliopata maambukizi makali ya virusi.

Taarifa kama hizo zilitolewa na daktari na muuguzi waliozungumza na BBC mashariki na kusini mwa Ethiopia mtawalia.

Katika siku za hivi karibuni idadi ya waathirika wanaobainika kila siku imeongezeka hadi kumi na kitu. Hilo limezua wasiwasi lakini idadi jumla bado iko chini - chini ya 400.

Hiyo ni licha ya kwamba Ethiopia, tofauti na nchi zengine bado haijaanza kutekeleza hatua za kusalia ndani na kuchukua hatua kidogo kama vile kupiga marufuku michezo na mikusanyiko kwa zaidi ya watu wanne kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona.

Media captionCoronavirus: Ethiopian pop star donates house to help fight virus

Daktari mjini Adis Ababa amesema raia wa Ethiopia huenda wameepuka kupata mlipuko mbaya wa virusi hivyo kwasababu ya idadi ndogo ya raia wa kigeni nchini humo ama pengine huenda kuna sababu zingine zisizofahamika.

Alisema watu wanastahili kuchukua tahadhari kuzuia kusambaa kwa virusi kwasababu uwezekano wa kuongezeka ni jambo ambalo haliwezi kuondolewa kabisa.

Short presentational grey line

Uganda kuangazia zaidi 'uchunguzi wa maneno'

Na Catherine Byaruhanga, Kampala

Traders sleep next to items to be sold at a market following a directive from Ugandan President Yoweri Museveni that all vendors should sleep in markets for 14 days to curb the spread of the COVID-19 coronavirus at Nakasero market in Kampala, Uganda, on April 7, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Uganda ni moja ya nchi zenye masharti makali kwa Afrika Mashariki na hadi kufikia sasa ni miongoni mwa nchi zenye idadi ndogo ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwenye eneo hilo - karibia waathirika 260 na bado hakujatokea kifo chochote chenye kuhusishwa na Covid-19.

Wengi waliopimwa nchini Uganda ni madereva wa malori au wa magari ya kubeba mizigo wanaoingia nchini humo kutoka nchi jirani. Wiki jana waziri wa afya Ruth Aceng alisema watu 139 wamethibitishwa kuambukizwa, 79 wakiwa ni madereva wa malori.

Rais wa chama cha madaktari nchini Uganda, Dkt. Richard Idro, alisema madaktari kote nchini humo hawajaripoti kupata wagonjwa zaidi wa maambukizi ya matatizo ya kupumua ingawa hatua za kusalia ndani ikiwa ni pamoja na marufuku ya usafiri huenda kumechangia pakubwa kuwazuia kwenda hospitali.

Watu wenye dalili za wastani za virusi vya corona pia huenda wanasalia nyumbani na kufanya wengine wanaoathirika data zao zisichukuliwe.

Presentational grey line
  • Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini Uganda hadi kufikia Mei 18: 87,832
  • Idadi ya wanaopimwa inastahili kuwa asilimia 1 ya idadi ya watu: 457,410
  • Waliopimwa virusi vya ukimwi kufikia Oktoba mosi hadi Desemba 2019: 2,098,734

Chanzo: Serikali ya Uganda, The Lancet

Presentational grey line

Katika hotuba ya hivi karibuni, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema serikali inapanga kuanza kufuatilia chanzo cha kifo cha mgonjwa katika jamii kubaini ikiwa pengine kuna wale waliokufa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Serikali imeahidi kugawa barakoa za bure kwa raia wote wenye umri wa miaka 6 na zaidi kwa kipindi cha wiki mbili zijazo kabla ya kulegeza masharti ya kusalia ndani.

Raia wa Uganda wamekuwa na mashaka na mipango inayoendelezwa wakizungumzia kuchelewa kutolewa kwa chakula kwa watu milioni 1.5 katika mji wa Kampla baada ya kupoteza ajira zao kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19.

Ikiwa hatua ya kugawanywa kwa barakoa itafanikiwa, Bwana Museveni ameahidi kwamba maduka yatafunguliwa, usafiri wa umma utarejea barabarani lakini kwa kubeba nusu idadi ya abiria wa kawaida pamoja na wauzaji wa vyakula masokoni ambao wamekuwa wakilala kwenye vibanda vyao chini ya agizo la rais - wataruhusiwa kurejea nyumbani kila baada ya biashara zao za siku.

Coronavirus
Banner