Virusi vya corona: Je roboti zinatumika vipi kwenye vituo vya Covid-19 Rwanda?

Zitasaidia kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa wa Covid19 zikisaidiana na wauguzi na madaktari

Chanzo cha picha, Wizara ya Afya Rwanda/ twitter

Maelezo ya picha, Zitasaidia kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa wa Covid19 zikisaidiana na wauguzi na madaktari
Muda wa kusoma: Dakika 2

Rwanda imesema kuwa tayari inatumia roboti katika kuzuwia maambukizi ya virusi vya corona kwenye vituo vya ugonjwa huo.

Hatua hii inakuja baada ya taifa hilo kulegeza masharti ya sheria ya kutotoka nyumbani.

Zitasaidia kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa wa Covid19 zikisaidiana na wauguzi na madaktari'', alisema Waziri wa Afya Dkt Daniel Ngamije.

'' Roboti inaweza kuchukua sampuli za mgonjwa katika badala ya muuguzi. Kuna kazi nyingi ambazo roboti zinaweza kufanya kuhudumia wagonjwa wa covid19, si kwamba wauguzi ama madaktari wameshindwa la hasha, ni kama kuwasaidia kupumua na pengine kuwapa nafasi kufanya mambo mengine ya kuwahudumia wagonjwa ipasavyo'' , anasema Dkt. Ngamije.

Roboti hizo mbazo zimepewa majina ya Kinyarwanda zinatarajiwa kusaidia katika huduma zinazotolewa na madaktari kwa wagonjwa na hivyo kupunguza hatari za usambazaji wa virusi baina ya wagonjwa wa Covid-19 na wahudumu wa afya, alisema Waziri wa afya awali katika mahojiano na Radio Rwanda.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Pamoja na kuwapelekea dawa wagonjwa, roboti pia zitatumika kupima viwango vya joto vya wagonjwa, katika maeneo mengine ya umma kama vile vituo vya mabasi pamoja na kwenye milango ya kuingia katika maduka ya jumla ya bidhaa alisema.

Tangu ulipotokea mlipuko wa COVID-19, Rwanda imekua ikitumia mfumo wa ndege ndogo zisio na rubani (drones) kuwasiliana na umma katika kuupa uelewa juu ya ugonjwa huo hatari.

Je hali ikoke kuhusu maambukizi?

Kufikia Jana Jumapili Rwanda ilikua na jumla ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona -284, waliopona 140, bila vifo.

Wakati huo huo watu 42,425 tayari wamefanyiwa vipimo vya Covid-19.

Chati inayoonyesha maendeleo ya ugonjwa wa Covid-19 nchini Rwanda

Chanzo cha picha, Wizara ya Afya Rwanda/ twitter

Maelezo ya picha, Chati inayoonyesha maendeleo ya ugonjwa wa Covid-19 nchini Rwanda

Wizara ya afya ya nchi hiyo imetangaza kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yanaonekana tu upande wa madereva wa magari makubwa yanayoingiza mizigo kutoka nchi jirani na Rwanda.

"Wagonjwa wapya tulio nao tangu wiki mbili zilizopita ni madereva wa magari makubwa ya mizigo. Madereva hao wana uraia mbali mbali wakiwemo pia Wanyarwanda. Ni kundi tunalofuatilia kwa namna ya pekee tangu tarehe 20 mwezi uliopita.wanapoingia tunachukua sampuli na kuwasindikiza hadi wanaposhusha mizigo...madereva wa kigeni wanarudia nchini mwao lakini tukataarifu nchi zao '', amesema Bwana Ngamije.

Waziri wa afya amesema nchi haijapata maambukizi mapya ya ndani ya nchi licha ya kwamba ililegeza vizuizi vya kutotoka nje kwa kufungua baadhi ya shughuli zikiwemo pia biashara.

Awali Rwanda ilitangaza mpango wa kupima virusi vya Corona kwa kutumia maabara ambayo kawaida hutumiwa kupima virusi vya ukimwi ukiwa ni mpango wa kupima idadi kubwa ya watu.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?