Coronavirus: Unachopaswa kujua kuhusu ngono na virusi vya corona

Watu wawili wakiwa na barakoa kitandani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wawili wakiwa na barakoa kitandani

Ikiwa nitafanya ngono ninaweza kupata maambukizi ya virusi vya corona? Unaweza kuona aibu kuuliza swali hili.

Kutenganisha ukweli na imani potofu, tumewasilisha maswali yako kwa wataalamu wa afya.

Alix Fox na Dr Alex George

Chanzo cha picha, Paul Cochrane/Jessie Whealey

Maelezo ya picha, Alix Fox na Dr Alex George wanajibu baadhi ya maswali yako kuhusu ngono wakati huu wa maambukizi

Je, ni salama kufanya ngono wakati wa mlipuko wa virusi vya corona?

Dr Alex George: Ikiwa uko kwenye mahusiano....ukiishi na mtu huyo katika mazingira hayo hayo, hilo lisibadili namna mnavyoishi. Hata hivyo ikiwa mmoja wenue ana dalili za virusi vya corona, basi italazimika kujitenga mbali na mtu huyo, hata kama mko nyumbani. Inashauriwa ulimwenguni kuwa kila mtu anapaswa kuwa umbali wa mita mbili na mwenzake hata kama mnaishi nyumba moja, lakini tumebaini kuwa suala hili linaweza lisiwe na uhalisia.

Alix Fox: Pia ni muhimu kutokudhani kuwa ikiwa una dalili za kuwa na virusi vya corona basi na mwenza wako atakuwa ameathirika. Hivyo, ikiwa utaonesha dalili, jaribu kukaa mbali na mpenzi wako.

Vipi kuhusu ngono na watu wengine?

Dr Alex: Hakika sitashauri kuwa na wapenzi wapya kwa sasa, kwasababu ya hatari ya maambukizi ya virusi.

Alix Fox: Usisahau pia, baadhi ya watu walio na maambukizi ya virusi hawaoneshi dalili zozote. Hivyo hata kama unajihisi vizuri... bado unaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa sababu ya kuwa naye karibu na kubusu.

Unachotakiwa kuzingatia ili kuzuia maambukizi zaidi
Maelezo ya picha, Unachotakiwa kuzingatia ili kuzuia maambukizi zaidi

Nilimbusu mtu mmoja ambaye nilikutana naye hivi karibuni, na sasa ameonesha dalili za kuwa na maambukizi. Nifanye nini?

Dr Alex: Ikiwa umemusu mtu au kuwa karibu na mtu ambaye unafikiri amepata maambukizi, hakikisha unajitenga.

Tazama kama una dalili. Ikiwa utaonesha dalili, yapaswa kuwa makini zaidi.

Alix Fox: Tunapaswa kuwajibika kwetu na kwa wenza wetu katika mahusiano yetu. Kama umepata dalili , na unajua hivi karibuni umewabusu watu, unapaswa kuwaambia. Hata kama umembusu mtu na akapata dalili nawe huoneshi dalili unapaswa kujitenga.

Sikuwa nikitumia kondomu na mpenzi wangu kabla ya mlipuko wa coronavirus, ninapaswa kuanza sasa?

Alix Fox: Jibu linategemea na sababu za kutotumia mpira hapo kabla.

Ikiwa ulikuwa hutumii mpira kwa kuwa nyote mlipima, au upo kwenye mahusiano au unatumia njia za uzazi wa mpango kuepuka mimba zisizotarajiwa, hapo ni sawa. Lakini kama ulikuwa hutumii mpira kwa kuwa ulikuwa unategemea njia nyingine ya kuhakikisha mpenzi wako yuko salama wakati wa kufanya ngono au ulikuwa hatarini kupata magonjwa ya zinaa, basi ni muhimu zaidi kutumia kondomu sasa.

Kuna wasiwasi wa kupoteza mahusiano katika kipindi hiki cha mlipuko

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna wasiwasi wa kupoteza mahusiano katika kipindi hiki cha mlipuko

Ninawezaje kuendelea na mahusiano yangu katika kipindi hiki?, sitaki kumpoteza mwenza wangu.

Alix Fox: Katika kipindi hiki cha janga watu wengi wanafikiri upya kuhusu maisha ya mahusiano ya ngono na namna ambavyo wenza wanaweza kuyafurahia kwa pamoja. Kwa mfano nimesikia watu wakiandikiana simulizi za mapenzi, na watu walio kwenye mahusiano lakini wako karantini wamekuwa wakitumia ubunifu wao wote wakati huu. Kuna namna nyingi ambazo wapenzi wanaweza kuzifurahia bila kuwa na mwenza uso kwa uso.

Je niko hatarini zaidi kupata maambukizi ya virusi vya corona kama nikiwa na virusi vya Ukimwi?

Alix Fox: Dr Michael Brady ametoa ushauri mzuri sana kuhusu hili. Ikiwa unatumia dawa za kupambana na makali ya virusi, na kuwa una kinga ya kutosha (ya kufanya chembechembe nyeupe kuweza kupambana na maambukizi) hiyo haikufanyi kuwa una mfumo dhaifu wa kinga. Inamaanisha kuwa hauko kwenye hatari ya kupata virusi vya corona. Hivyo kama ni muathirika wa virusi vya Ukimwi, endelea kutumia dawa kama kawaida. Hakikisha unafuata maelekezo kila siku kama wanavyofanya wenginekama vile kujitenga.

Presentational grey line