Coronavirus: Je kujitenga na watu ni kupi na kunasaidia vipi kujikinga na virusi vya corona?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mataifa mengi duniani yamewataka wananchi wao kutokufanya safari ambazo si za lazima, japo watu wanaweza kutoka alimradi wajitenge na wengine kwa mita mbili au zaidi.
Migahawa, vilabu, kumbi za starehe na mazoezi zinafungwa kila uchao.
Yote hayo ni baadhi ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa wale ambao wanatakiwa kujitenga ama kujiweka karantini.
Lakini je, kuna mambo gani ya msingi kuzingatia?
Je, unaweza kutembea/kuota jua?
Ndio. Taasisi ya Afya ya Jamii ya England inasema: "Unaweza kutembea ama kufanya mazoezi nje ya nyumba yako lakini inapaswa uache nafasi ya mita mbili ama zaidi baina yako na wengine."
Lakini katika maeneo mengi ya wazi ama ama katika usafiri wa umma itakuwa ni vigumu kuhakikisha nafasi hiyo inapatikana.
Dkt Robin Thompson, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford anasema: "Kitu cha msingi zaidi ni kuhakikisha kuwa unapunguza kukutana na watu. Chagua sehemu ambazo hazina mkusanyiko mkubwa wa watu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa nini ni muhimu kujitenga?
Kujitenga ni muhimu kwa kuwa virusi vinasambaa haraka pale mtu mwenye mambukizi anapopiga chafya ama kukuhoa na kuwaambukiza wengine endapo watakuwa karibu naye na kusambaza virusi hewani na kwenye vitu vya karibu.
Maambukizi hutokea pale watu hao wa karibu watakaposhika nyuso zao hususani mdomo, macho na pua.
Pale watu watakapotangamana kwa muda mchache, ndio uwezekano wa maambukizi huwa mdogo zaidi.
Kujitenga ni muhimu zaidi kwa watu ambao wapo zaidi ya miaka 70 na wajawazito.

Unawezaje kujitenga
- Fanya kazi nyumbani kila inapowezekana
- Jizuie kusafiri kama si muhimu
- Epuka maeneo ya watu wwengi
- Epuka mikutano ya marafiki na familia kila inapowezekana
Mambo unayoruhusiwa kufanya ukiwa umejitenga
- Unaweza kuiona familia na ndugu pale kwenye umuhimu
- Unaweza kunyoosha miguu
- Unaweza kuhudumia ndugu wazee pale inapobidi na majirani pale ambapo hawaoneshi dalili.
- Unaweza kwenda dukani kununua chakula na mahitaji muhimu.


Je kujiweka karantini ni nini?
Kujiweka karantini ni pale ambapo mtu anaonesha dalili za ugonjwa na inabidi ajitenge pekee ili kuangalia hali yake.
Kama inawezekana, inashauriwa kuwa hawatakiwi hata kutoka nje na kununua chakula na mambo mengine ya msingi.
Na ikitokea umetoka nje basi hakikisha haukutani kabisa na watu.
Nani ajiweke Karantini?
Yoyote yule ambaye ataonesha dalili za virusi vya corona - homa inayoambatana na joto la zaidi ya 37.8C, kikohozi kikavu na shida ya kupumua. Pia watu ambao wanaishi nyumba moja ama jengo moja na mtu mwenye dalili za maambukizi.
Kama unaishi mwenyewe, hakikisha hautoki ndani kwa siku saba toka dalili zilipoanza.
Kama wewe, ama mtu unayoishi naye ataonesha dalili, nyuma nzima itatakiwa kujitenga kwa siku 14 ili kuangalia dalili za corona.

Kama mtu ataumwa katika kipindi hicho, siku zao saba zitaanza siku hiyo.
Maana yake kama ataumwa siku ya tatu basia atatakiwa kujitenga kwa siku saba zaidi na kwwnda mpaka siku ya 10.
Lakini kwa yeyote atakayeumwa siku ya 13 basi siku zake saba za kujitenga ili apone zitaanza siku hiyo - maana yake watatumia siku 20 nyumbani.
Watu hao wanatakiwa kukaa kwenye chumba chenye hewa na mwanga wa kutosha. Madirisha yanaweza kufunguliwa na watu wengine hawatatakiwa kukaribia.














