Coronavirus: Mataifa ambayo utafungwa ukiuka maagizo ya kudhibiti virusi vya corona

Janga la coronavirus limeshinikiza kuchukuliwa kwa hatua ambazo hazikutarajiwa katika maeneo mbali mbali duniani.

Kuanzia Uhispania hadi Marekani, 7 serikali zinajaribu kuchukua hatua kujaribu kupunguza kuenea kwa virus hivyo.

Pamoja na kuweka ukomo wa kiwango cha safari za kimataifa, baadhi ya nchi pia zinajaribu kudhibiti matembezi ndani ya mipaka ya nchi zao na kuzuwia watu kuchangamana katika maeneo ya umma.

Sera ya afya na wataalamu wanaonya kuwa sasa nchi zinakabiliwa na ugumu wa kuwa na uwiano kati ya kulinda afya ya umma na kuingilia uhuru wa watu wa kibinafsi.

Lakini je ni vipi nchi zinatekeleza hatua mkiwemo karantini na kuzuwiwa kwa shughuli mbalimbali?

Kwa wiki kadhaa China, ambako mlipuko wa Covid-19 ulianzia, ilipata athari kubwa ya kusambaa.

Kulikua na ukosoaji mkubwa juu ya jinsi ilivyoshughulikia virusi mwanzoni mwa mlipuko, huku baadhi wakiishutumu serikali ya Beijing kwa kujaribu kutosema ukweli halisi juu ya ukubwa wa kiwango cha mlipuko.

Na hali ikawa mbaya zaidi, sharti la marufuku ya kuendeshwa kwa shughuli zenye mikusanyiko ya watu ilikua ya kwanza kutekelezwa katika mji wa Wuhan, ambao ni kitovu cha mlipuko na moja ya miji mikubwa zaidi nchini Uchina.

Safari zilipigwa marufuku hatua ambayo iliendelezwa kwingine na kuwaathiri mamilioni kwa mailioni ya watu.

Takriban waandishi wa habari walili raia wa nchi hiyo, waliojaribu kushirikisha umma juu ya mlipuko wa coronavirus kupitia mitandao ya kijamii walitoweka.

Vipimo vya joto la mwili vilikfanyika katika mitaa na baadhi waliripoti kuwaona walinzi kwenye milango ya kuingia nyumba zao ili kuhakikisha watu wanabaki ndani ya nyumba zao. Uchina ilishutumiwa kutumia mfumo wake wa upelelezi unaowahusisha watu wengi katika kusaidia kuzuwia matembezi na kufuatilia afya za watu.

Huku hali ikiwa ni ya ahueni, kuna ishara za kurejea kwa hali ya kawaida ya maisha katika baadhi ya sehemu polepole. Lakini baadhi ya makundi, kama shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, yamekua yakilikosoa jinsi Shirika la Afya Duniani (WHO) lilivyozungumzia kuhusu jinsi serikali ya Beijing ilibyoshughulikia mlipuko wa coronavirus - yakisema kuisifu serikali ya Uchina kunahatarisha kunahalalishwa ukiukaji wake wa haki za binadamu na udhibiti.

Baada ya kuongezeka kwa kwa hali mbaya ya maambukizi , Italia sasa ni nchi ya pili iliyokumbwa na mlipuko baada ya Uchina. Kumekuwa na masharti makali ya kuzuwia mikusanyiko ya umma ili kujaribu kusitisha usambaaji waq virusi.

Masharti yalitekelezwa kwa mara ya kwanza kaskazini mwa nchi, kabla hayajatekelezwa kitaifa.

Serikali imewataka watu milioni 60 wa Italia kubakia majumbani mwao pale inapowezekana.

Wakazi wanaweza kutoka nje ya nyuma zao tu pale wanapokua na hitaji la dharura, kama vile kununua bidhaa muhimu na wanatarajiwa kutembea na kibali maalum kinachoelezea sababu ya safari yao.

Wanaokiuka amri hiyo wanakabiliwa na tisho la kutozwa faini ya dola 235 kwa kuvunja sheria au hata kufungwa jela kwa muda wa miezi mitatu.

Watu nchini Uhispania wamekua pia katika kipindi cha kuzuiwa kwa maisha ya umma.

Maeneo yote yasiyo ya muhimu yamefungwa na watu wamekua wakiambiwa kutoka majumbaji mwao pale inapokua ni muhimu.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez alitangaza hali ya tahadhari, kwa mara ya pili tukatika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo, akiwaambia Wahispania kuwa wanakabiliwa na "Wiki mbili ngumu sana" ya kujitolewa smbele yao.

Kumekua na ripoti za maafisa wa usalama na wanajeshi kupelekwa katika maeneo ya umma kufuatilia na kuzuia mikusanyiko ya umma. Wanajeshi wenye silaha pia wameingilia kati katika kulinda watu wasio na makazi nchini humo, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo.

Baadhi ya nchi zimetishia kutoa adhabu kali kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Ufaransa imesema kuwa itatoa faini ya hadi Euro €135.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Christophe Castaner alisema kuwa maafisa wa polisi 100,000 waanasambazwa katika maeneo mbali mbali ya nchi ili kuhakikisha hatua kali mpya za kupunguza utengamano wa kijamii inatekelezwa.

Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu. Bwana Macron alisema: "Tuko vitani... hatupambani na jingine lolote lile wala nchi yetu wenyewe.

Lakini adui yuko hapa, haonekani, hawezi kuguswa ... na anasonga mbele."

Saudi Arabia inatangaza faini ya hadidola $133,000 (£110,000) kwa mtu yeyote atakayeshindwa kutangaza taarifa sahihi za kiafya zinazomuhusu pamoja na maelezo anapoingia nchini.

Badhi ya mataifa yameweka marufuku unapowasili, kufunga mipaka yao ya anga na ardhini.

Wengine wameweka amri ya kuwekwa karantini kwa muda wa siku 14 kwa watu wote wanaosafiri kwa ndege kuingia nchini mwao, mkiwemo amri inayomtaka mtu kujitenga binafsi katika makazi binafsi kama vile kwenye hoteli.

Yeote ambaye haheshimu sheria mpya nchini Australia atakabiliwa na tisho la faini nzito na hata kifungo cha jela katika baadhi ya maeneo ya nchi. Faini kubwa zaidi iliyowekwa Magharibi mwa Australia ambako wale wanaokiuka amri hiyo wanakabiliwa na kulipa faini ya hadi dola za Australia- A$50,000 (£25,000).

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameonya kwamba wasafiri wanaoshindwa kuheshimu sheria za kujitenga wanaweza kukabiliwa na faini na kufukuzwa .

"Iwapo utakuja hapa na hauna nia ya kufuata maombi yetu ya kujitenga binafsi, kusema kweli haukaribishwi na unapaswa kutoka nchini kabla hatujakurejesha ulikotoka ," alisema.

Nchini Marekani kituo cha udhibiti na tiba ya magonjwa-Disease Control and Prevention (CDC) chenye mamlaka ya kuzuwia kuingia na kusambaa kwa magonjwa yanayoambukizwa ndani ya nchi na nje ya kiliimarishwa zaidi wakati Wamarekani walipoejeshwa kwa ndege kutoka Wuhan walipowekea karantini katika ngome ya kijeshi ya California mara walipokua wakirejea.

Kumekua na visa vilivyotengwa ambako uvunjaji wa sheria umekua ni tatizo.

Katika Kentucky mmoja wa wakazi alikataa kujitenga hadi polisi ofisa aliwekwanje ya nyumba yake ili kumlazimisha kubakia ndani, kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo.

Nchi za Africa Mashariki pia zimechukua hatua za kudhibiti maambukizi ya coronavirus.

Tanzania imetangaza Jumanne kuwa imekuwa na kisa cha kwanza cha coronavirus. Miongoni mwa maelekezo yaliyotolewa na waziri wa Afya nchini Tanzania ni pamoja na kuwataka Watanzania wasiokuwa na safari za lazima wanashauriwa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi.

Unaweza pia kutazama:

Taasisi zote zikiwemo shule, hoteli, maduka ya biashara, nyumba za kulala wageni, makanisa, misikiti, ofisi za umma na binafsi, vituo vya kutolea huduma za afya, taasisi za fedha, vyombo vya usafiri pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya michezo na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni au maji yenye dawa kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono.

Kuweka maji yenye dawa ya chroline katika mageti ya kuingia katika hifadhi zote kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza wageni.

Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono.

Kukumbatiana , kubusu, kuepuka kushika pua, mdomo na macho.

Hospitali zote nchini za serikali na zisizo za serikali kuweka zuio la idadi ya watu ambao wanakwenda kuwaona ndugu zao. Kwa maelekezo ya waziri ni kwamba wageni wa kumuona mgonjwa wasizidi wawili kwa siku kwa kila mgonjwa mmoja.

Wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa vituo vya afya iwapo watamuona na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Covid- 19.

Hata hivyo baadhi ya Watanzania katika mitandao ya kijamii wanasema hatua hizo hazitoshi ikizingatiwa kuwa baadhi ya raia hawana uwezo wa kununua kemikali za kuua vimelea (hand sanitizer) na baadhi hawana hata maji ya kunawa mara kwa mara mikono.

Rwanda ambayo ni nchi iliyoripoti visa vingi zaidi ya mataifa mengine jirani, ikiwa na wagonjwa saba imekua mstari wa mbele katika uhamasishaji wa watu kunawa mikono na kukanyaga katika maji yaliyowekwa kemikali ya kuua vijidudu hata kabla ya kuripoti visa hivyo pia imeweka sheria ya watu kuacha kufanya mikutano ya umma.

Maafisa wamefunga shule na taasisi zote za umma pamoja na maeneo ya kuabudu katika jitihada za kuzuwia kusambaa kwa coronavirus. Wafanyakazi wa umma na pia wa kibinafsi wameruhusiwa kufanyakazi kutoka majumbani kwao isipokua wafanyakazi wa muhimu zaidi.

Wakati huo huo serikali imetoa huduma ya kemikali ya kuua vimelea mikononi kwenyemasoko ya bidhaa.

Katika taifa la Kenya ambako visa vitatu vya coronavirus vimetangazwa hadi sasa, rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta Jumapili alitoa maagizo juu ya udhibiti wa kuenea zaidi kwa virusi hivyo mkiwemo kufungwa kwa Shule za msingi na sekondari kuanzia Jumatatu na za bweni zitafungwa ifikapo Jumatano, hatua ambazo zimekwishaanza kutekelezwa.

Vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu zitafungwa ifikapo Ijumaa na pale inapowezekana alisema waajiriwa wanapaswa kuruhusiwa kufanya kazi majumbani kwao ili kuepukana na maambukizi ya coronavirus.

Shughuli za kidini zinazowakutanisha watu wengi pia zimezuwiwa huku wenye maduka ya jumla wakiripotiwa kuanza kutekeleza amri ya rais ya kuweka kwenye milango yao kemikali za kuua vimelea kwenye mikoni( hand sanitizer).

Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wa hatua za kukabiliana na kuenea kwa coronavirus nchini Kenya wanadai baadhi ya raia hawana taarifa za kutosha kuhusu virusi hivyo na hivyo kuwepo kwa hatari ya kupuuzwa kwa maagizo yaliyotolewa na rais juu ya udhibiti wa coronavirus.