Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus imepewa jina jipya rasmi -Covid-19, yasema WHO
Shirika la Afya Duniani WHO, linasema jina rasmi la ugonjwa unaosababisha na virusi vipya vya corona uitwe Covid-2019.
"Sasa tumeupatia jina ugonjwa na utaitwa Covid-19," Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva
Hii inakuja baada ya vifo vilivyotokana na viurusi hihvyo kufikia zaidi ya 1,000. Maelfu kwa maelfu ya watu wameambukizwa virusi hivyo.
Neno coronavirus linamaanisha aina ya kikundi cha virusi kinamotoka kirusi hicho , na wala si ugonjwa wa hivi sasa.
Watafiti wamekua wakitoa wito wa kuwepo kwa jina rasmi ili kuepuka mkanganyiko na unyanyapaa.
"Tulikua hatujapata jina ambalo halitamaanisha eneo la kijiografia , mnyama, mtu au kikundi cha watu, na ambalo pia linaweza kutamkika na kuhusiana na ugonjwa ," alisema mkuu wa WHO.
Unaweza pia kusoma:
"Kuwa na jina ni jambo la maana katika kuzuwia matumizi ya majina mengine ambayo sio sahihi au unyanyapaa.
Pia inatupatia kiwango cha muundo tutakaoutumia kwa ajili ya milipuko ijayo ya Virusi vya corona"
Kuna zaidi ya visa zaidi ya 42,200 vilivyothibitishwa kote nchini Uchina. Idadi ya vifo imezi9di ile ya mlipuko wa virusi vya Sars mwaka 2003.
Jumatatu, watu wapatao 103 walikufa katika jimbo la huabei pekee, ikiwa ni idadi kubwa ya vifo kutokea kwa siku moja pekee, na idadi ya vifo kwa taifa zima imefikia 1,016 kwa sasa.
Lakini idadi ya maambukizi mapya kitaifa iko chini ya karibu 20% kuanzia siku siku moja kabla kutoka watu 3,062 hadi 2,478.
Uchina ''imewaondoa" kazini maafisa kadhaa wa ngazi ya juu kufuatia namna walivyoushughulikia mlipuko - huku idadi ya vifo ikizidi watu 1,000.
Katibu wa chama anayehusika na kamati ya afya ya Hubei , na mkuu wa kamati hiyo walikua ni miongoni mwa wale waliopoteza kazi.
Ni maafisa wa ngazi ya juu zaidi kushushwa cheo hadi sasa.
Unaweza pia kutazama: