Mashtaka dhidi yaTrump : Kila kitu unachohitaji kujua kuhusu kesi hii

Hii ni mara ya tatu katika historia, ambapo rais wa Marekani anakabiliwa na kesi ya kutumia madaraka vibaya kwa maslahi yake binafsi.
Mashitaka ambayo yanaweza kumpelekea rais Donald Trump kuondolewa madarakani.
Leo ni siku ya pili tangu bunge la seneta wameanza kusikiliza kesi ya rais Trump.
Matokeo yake yanaweza kuleta mshuko mkubwa na tutaeleza sababu zake , lakini kwanza ni vvyema kuelewa maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na watu wengi.
1) Mashitaka dhidi ya rais ni yapi?
Mashitaka haya huwa yanatokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kiongozi kama Jaji, rais na wabunge, kutumia wadhifa wake kwa ajili ya manufaa yake binafsi.
Makosa haya yanajumuisha rushwa,ufisadi,uhaini na uhalifu mwingine.
Baada ya kiongozi kushtakiwa, kesi yake huwa inapelekwa kwenye bunge la seneta na wawakilishi wa baraza huwa wanaamua kama ana hatia au la.Huwa ni kesi ambayo inatatuliwa kisiasa na sio kihalifu.
2) Trump anashutumiwa kwa kosa gani?
Trump anakabiliwa na mashtaka mawili.
Kwanza, anashutumiwa kwa kuomba msaada kwa serikali ya Ukraine kumsaidia achaguliwe tena mwezi Novemba.
Anashutumiwa kwa kusitisha kutoa misaada ya mamilioni ya fedha pamoja na msaada wa kijeshi kwa Ukraine mpaka rais wa nchi hiyo afanye uchunguzi dhidi mpinzani wake.
Pili , Ikulu ya Marekani kutoruhusu wafanyakazi wake wote kutoa ushaidi dhidi ya Trump wakati kesi ya rais huyo iliposikilizwa wa mara ya kwanza mwaka jana.
Bwana Trump alikanusha kuhusika na makosa yote na kikosi chake cha sheria na kudai kuwa madai haya ni hatari sana na huo ni upotoshaji wa katiba.
Ilikuwa sawa kuwa madai haya hayana uhusiano na uchunguzi wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Mwaka 2016.
3) Kwa nini kuna kesi?
Hatua kadhaa zilipita ili madai haya kuitwa kesi:
- Agosti 2019: Watu walitoa madai dhidi ya rais Trump
- Oktoba - Disemba: Uchunguzi ulifanyika , licha ya chama cha Trump kuwa na viti vingi zaidi ya wapinzani wake.
- Disemba:Kiongozi wa Democratic alipiga kura kumshtaki rais Trump
- Januari 2020: Kesi ilifikishwa kwa seneta
4) Seneta itazingatia nini?
Katiba ya Marekani iko wazi ikija kwenye upande wa mashtaka ya uongozi.
Ingawa kuna utaratibu wa kiujumla ambao ulianza kutumika tangu rais Andrew Johnson aliposhtakiwa 1868.
Vilevile wakati ambao rais Bill Clinton ialipokabiliwa na mashtaka dhidi yake mwaka 1999. Ingawa yeye pia alinusurika kukutwa hatiani.
Watu wawili wataamua kesi hiyo itasikilizwaje: Mitch McConnell, kiongozi wa Republican katika Seneti, na mpinzani wake wa Democratic , Chuck Schumer.
Wote watakubaliana miongozo ya kusikiliza kesi hiyo kuanzia kwenye ushaidi, mashaidi, muda na majadiliano.
Lakini kwa sababu Republicans ndio wanaongoza bunge la seneti Senate, bwana McConnell atakuwa na maamuzi ya mwishi kuhusu mfumo wa uendeshwaji wa kesi hiyo.
Ingawa tayari bwana McConnell alisema kabwa kuwa: "Nitaenda kuchukua maelezo yangu kutoka kwa wakili wa rais, wote mnafahamu nini kinaenda kutokea."

Chanzo cha picha, Getty Images
Seneta atasikiliza pande zote mbili-mwendesha mashtaka kutoka wawakilishi wa baraza pamoja na mawakili kutoka ikulu pamoja na mashaidi wowote.
Baada ya hapo , maseneta watapewa siku nzima kujiandaa kwa ajili ya kupiga kura ya kumuondoa Trump.
Republicans wanaweza kumuokoa Trump kutoondolewa madarakani kwa sababu wana idadi ya kutosha ya kuweza kumkingia kifua.
Mbili ya Tatu ya viti vya bunge la seneti ni upande wa rais , hivyo kati ya viti 100- maseneti, 67 wanahitaji kupiga kura ili Trump aweze kupata ushindi.
Lakini kuna viti 45 vya Democrats , wawili hawana chama na Republican 53, rais ana nafasi kubwa ya kushinda.
5) Mhusika mkuu ni nani?
Kila seneta akiwemo bwana McConnell, ambaye tayari a mekabidhi kitabu cha hati ya mashtaka kinachofahamika kama 'oath'.
Lakini bwana McConnell - na viongozi wa ngazi za juu wa Republican katika Senate - mwezi uliopita walisema kuwa watashirikiana na Ikulu kukabiliana na kesi hii.
"Kila kitu ambacho ninakifanya wakati huu, ninaratibu ikulu," alikiambia chombo cha habari cha Fox pamoja wawakilishi wa juu wa Democrats.
6) Je, Trump atatoa ushaidi?
Ni maamuzi yake Trump kufika katika bunge la seneta au la, lakini wakili wake ndio watakuepo ambamo ni bwana Cipollone na bwana Sekulow, na kuongea kwa niaba yake.
Mawakili wake watakuwa kama mameneja wa mashtaka hayo, wataweza kuuliza maswali kwa mashaidi na kuwasilisha taarifa mwanzo mpaka mwisho.
Bwana Trump anatamani sana bwana Biden atoe ushaidi pamoja na watu waliotoa taarifa.
Democrats wawataka maafisa wa ngazi za juu kutoka ikulu kutoa ushaidi wao, akiwemo mshauri wa zamani wa usalama John Bolton.
Lakini labda hakutakuwa na mashaidi wowote kutoka kama Republicans wakiamua kuwa ni vyema kufupisha mlolongo wa kesi hiyo.
Ingawa wakati wa kesi ya Clinton, rais huyo hakuwa na mashaidi.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
7) Kesi hii itaisha lini?
Baada ya mashtaka haya kuwasilishwa kwa seneti, kesi hiyo itachukua siku tatu wakati wa kesi ya Clinton, maseneta wanapaswa kuhudhuria siku zote za kesi hiyo isipokuwa jumapili mpaka maamuzi ya mwisho yatolewe.
Hii inamaanisha kuwa maseneta wanne wanaowania urais - Bernie Sanders, Elizabeth Warren, Amy Klobuchar na Michael Bennet - wanapaswa kuacha kufanya kampeni zao kwa muda wakati kesi hiyo ikiendelea.
Kesi inaweza kuchukua wiki kadhaa ingawa ya Clinton ilichukua karibu mwezi.
Democrats wanatarajia kesi hii kumalizika mwezi Februari na kuanza uchaguzi wa awali wa mwaka 2020 na kuamua nani atapambana na Trump katika uchaguzi ujao.















