Davos: Trump amewashutumu wanamazingira aliowaita "manabii wa kutabiri mabaya"

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Donald Trump wa Marekani amewashutumu wanamazingira kama "manabii wa kutabiri mabaya" kwenye hotuba aliyoitoa katika jukwaa la Kiuchumi Duniani, huko Davos ambapo maudhui ni Uendelevu.
Alitoa wito wa kutupiliwa mbali kwa utabiri alioufananisha na ufunuo wa Apokalipsi, na kusema Marekani itatetea uchumi.
Bwana Trump hakumtaja moja kwa moja mwanaharakati Greta Thunberg, ambaye alikuwa miongoni mwa waliokusanyika.
Baadaye akalaumu viongozi wa kisiasa na kusema "iwapo hamkua mnalifahamu, kwa sasa dunia ipo pa baya".
Uharibifu wa mazingira kwa sasa ndiyo ajenda kuu ya mkutano huo unaofanyika kila mwaka ambao mwaka huu uko eneo la kitalii la Swiss ski.
Katika hotuba yake, bwana Trump amesema kwamba ni wakati wa kuwa na matumaini wala siyo kutazamia mabaya, kweye hotuba ambayo imesifu mafanikio ya kiuchumi katika utawala wake na sekta ya nishati ya Marekai ambayo imeimarika.
Akizungumzia wanaharakati wa mazingira, amesema: "Wazushi hawa kila wakati hutaka yale yale - nguvu ya kutawala, mabadiliko na kudhibiti kila sehemu ya maisha yetu."
Walikuwa, amesema, "wabashiri wa matukio ya jana yasiyokuwa na maana"
Alikuwa akizungumza saa kadhaa kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili dhidi ya utumiaji mbaya wa madaraka ambayo ipo kwenye bunge la Seneti.
Bi.Thunberg azungumza

Chanzo cha picha, AFP
Baada tu kumaliza kuzungumza, Bi. Thunberg, mwanaharakati wa mazingira wa Sweden mwenye umri wa 17 ambaye amekuwa akiongoza vuguvugu linalotoa wito kwa wanafunzi kuandamana kote duniani wakitoa wito wa hatua haraka kuchukuliwa dhidi ya uharibifu wa mazingira, kufungua kikao kilichofahamika kama ''Kuepuka mazingira ya Apokalipsi".
Alijizuia kumtaja Trump lakini akatoa onyo hili kwa viongozi wa dunia.
"Sijui ni sababu gani mtakayotoa kwa watoto wenu kwamba kilikuwa chanzo cha kero za mabadiliko ya tabia nchi ambazo nyinyi mmezileta? ambacho kilionekana kuwa kibaya zaidi kwa uchumi kiasi cha kuamua kuachana na wazo la kuhakikisha mnatengeneza mazingira mazuri ya baadaye?
"bado nyumba yetu inaungua. Kutochukua hatua kwenu kunachochea zaidi moto huo kila baada ya saa, na kile tunachowaambia ni kwamba, mchukue hatua zinazoonesha kuwa mnajali watoto wenu."
Alishutumu wanasiasa na wafanyabiashara kwa kile alichokitaja kuwa ni ni maneno matupu yasiyokuwa na ukomo".
"Munasema: 'Tutafanya munayotaka. Musiwe watu wa kutazamia mabaya.' Na baada ya hapo, munanyamaza."

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani inajiondoa katika Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya hali ya hewa ambayo Trump amesema kwamba hayafai. Kujiondoa huko kutaanza kutekelezwa baada ya uchaguzi wa urais wa Marekani 2020 - tukifikiria kwamba Trump atakuwa amechaguliwa tena.













