Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mashtaka dhidi ya Trump: Kesi inayomkabili Trump kuanza leo
Kwa mara ya tatu katika historia, rais wa Marekani anakabiliwa na mashtaka, kesi dhidi ya rais Donald Trump itaanza kusikizwa baadae Jumanne.
Kiuhalisia kesi kama haya inaweza kumuondoa rais madarakani. Basi fuatilia hatua hii kubwa ambayo inaweza kuchukuliwa wiki hii dhidi ya rais wa Marekani.
Niko tayari - na siwajali wapinzani!
Kwanza hatuna wapinzani wowote. Kutakuwa na michezo mingi ya kuigiza katika mfululizo wa kusikiliza kesi hii.
Ingawa tunaweza kuwajibu baadhi ya wasomaji wetu baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa kila mara.
Sawa basi. Mashtaka dhidi ya rais yana maana gani?
Mashtaka dhidi ya rais yanahusisha kesi inayoweza kumuondoa rais madarakani.
Baadhi ya watu wanadhani kuwa mashtaka dhidi ya rais inamaanisha kuwa ni kumuondoa kiongozi wa nchi madarani, lakini kiuhalisia huu ni mwanzo wa hatua mbili za kisheria ambazo zinapaswa kupitishwa katika baraza la Congress.
Kwanza, baraza la wawakilishi lilikuwa linatafuta ushaidi na kuamua namna gani wanaweza kumuhukumu rais dhidi ya mashtaka dhidi yake.
Hii imeshatokea na sasa tuko kwenye hatua nyingine.
Na sasa baraza la seneta linajaribu kutafuta namna ya kumkuta na rais na hatia, na kama ataondolewa madarakani basi makamu wa rais atachukua nafasi hiyo.
Umeelewa. Ni marais wangapi wa Marekani waliwahi kushtakiwa?
Ni marais wawili tu: Andrew Johnson mwaka 1868 na Bill Clinton mwaka 1998. Wote walikabiliana na mashtaka dhidi yao ambayo yangeweza kuwaondoa madarakani lakini baadae waliweza kuokolewa katika bunge la seneta.
Mwaka 1974, Rais Richard Nixon alikutwa na madai ya kuwachunguza wapinzani wake iliyojulikana kama 'Watergate' - Yeye alijiuzuru kabla ya Congress haijatuma madai dhidi yake, jambo ambao lingeweza kumuondoa madarakani.
Kwa nini Trump ameshtakiwa?
Donald Trump anashutumiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kutumia cheo chake ili aweze kupata nafasi za kushinda uchaguzi wa urais mwezi Novemba.
Katika mawasiliano ya simu, Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndiye mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.
Uchunguzi unataka kubaini ikiwa Bwana Trump alitumia kitisho kuzuia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae.
Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni "hila".
Je, Trump alivunja sheria?
Si kila mtu alikubali kuwa Trump alipaswa kushtakiwa kwa sababu ya kumuomba kiongozi wa nchi nyingine kumfanya hila kwa mpinzani wake.
Trump alisema kuwa hajafanya kosa lolote ambalo lilihitaji zoezi lote hili. Ikulu pia ilionyesha kutoonyesha ushirikiano katika hilo.
Lakini kesi imekuwa ikichochewa na watoa taarifa kulalamikia simu aliyompigiwa Zelensky tarehe 25 Julai mwaka jana.
Trump alisitisha misaada ya mamilioni ya dola pamoja na usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine, na maafisa wa juu walisema kuwa hawatatoa misaada hiyo mpaka mamlaka ya taifa la Ukrain kuanza uchunguzi dhidi ya mpinzani wa Trump.
Ikulu ya Marekani ilikanusha madai hayo.
Nini kitatokea?
Baraza la wawakilishi lilifanya uchunguzi. Bunge likapiga kura ili madai ya Trump yafikishwe kwa seneta.
Na sasa kesi hiyo iko chini ya seneta, ambapo tayari wawakilishi 100 wa seneti wameapa katika kitabu cha utawala kinachojulikana kama Oath.
Huku Mwendesha mashitaka mkuu akifuatilia kesi hiyo.
Watu wawili wataamua kesi hiyo itasikilizwaje: Mitch McConnell, kiongozi wa Republican katika Seneti, na mpinzani wake wa Democratic , Chuck Schumer.
Wote watakubaliana miongozo ya kusikiliza kesi hiyo kuanzia kwenye ushaidi, mashaidi, muda na majadiliano.
Lakini kwa sababu Republicans ndio wanaongoza bunge la seneti Senate, bwana McConnell atakuwa na maamuzi ya mwishi kuhusu mfumo wa uendeshwaji wa kesi hiyo.
Ingawa tayari bwana McConnell alisema kabwa kuwa: "Nitaenda kuchukua maelezo yangu kutoka kwa wakili wa rais, wote mnafahamu nini kinaenda kutokea."
"Rais anaweza kuondolewa madarakani."
Hivyo tunajua nini kinaweza kutokea?
Republicans wanaweza kumuokoa Trump kutoondolewa madarakani kwa sababu wana idadi ya kutosha ya kuweza kumkingia kifua.
Mbili ya Tatu ya viti vya bunge la seneti ni upande wa rais , hivyo kati ya viti 100- maseneti, 67 wanahitaji kupiga kura ili Trump aweze kupata ushindi.
Lakini kuna viti 45 vya Democrats , wawili hawana chama na Republican 53, rais ana nafasi kubwa ya kushinda.
Hatua hii haimuweki Trump katika hatari ya kuondolewa madarakani, lakini akiondolewa madarakani basi makamu Mike Pence ndio ataapishwa kuwa rais.
Kuna maana gani kama ni ngumu kutolewa - au huu ni mchezo wa kuigiza tu?
Wanaomuunga mkono Trump wanasema kuwa wanaamini kuwa wapinzani wanajaribu kumuharibia Trump katika uchaguzi ujao.
Kesi hii inaweza kuleta picha itakayoweza kuharibu sifa za rais.
Lakini spika Nancy Pelosy,anasema hali hii sio nzuri.Anadhani kuwa ikulu inapaswa kuonesha ushirikiano.
Bilionea aliyegeuka kuwa mwanasiasa mwenye masuala ya utata, swali ni je, kweli atang'oka madarakani au la.