Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbwembwe za saini ya kalamu nyingi dhidi ya Trump
Seneta wa Marekani amepokea rasmi hati ya mashitaka dhidi ya rais Donald Trump.
Utaratibu wote ulienda vizuri na kuonekana kuwa wa mvuto kwa upande wa Congress.
Spika Nancy Pelosi alitumia kalamu kadhaa kuweka sahihi yake katika hati hiyo ya mashtaka - ambayo yanawakwaza Republicans - kabla ya upande wa Democrats na House clerk kuingia rasmi katika chemba ya seneta kuwasilisha hati za mashtaka yao.
Waliingia kwa shamra shamra wakipiga kelele wakisema 'Hear ye, hear ye, hear ye' kuonyesha hasira yao dhidi ya mashitaka hayo, na watu wote waliamriwa kuwa kimya.
Hili ni tukio la kiaina yake kwa upande wa Congress kati ya maadhimisho machache ambazo zimezoeleka kufanyika katika bunge la Uingereza.
Shughuli kama hii ina maana gani na huwa inafanyikaje?
Sahihi inayoandikwa kwa kalamu nyingi
Bi.Pelosi na kikosi chake walikuwa katika tafrija ya kisheria siku ya jumatano jioni , ambapo spika alisaini hati za makosa dhidi ya rais na kukabidhi nakala kwa seneta.
Ilimchukua muda kufanya shughuli hii kwa sababu alitumia kalamu tofauti tofauti na masihala mengi ili kuonyesha namna sahihi inavyoweza kuwekwa kwa kuburudisha watu.
Waandishi walichukua picha ya kalamu zilizokuwa katika sahani, katika karatasi nane kila karatasi lilikuwa limeandikwa jina la bi.Pelosi kabla hajasaini katika shughuli hiyo.
Utamaduni huu wa kusaini kwa kalamu nyingi umekuwa wa muda mrefu nchini Marekani tangu wakati wa utawala wa rais Franklin Roosevelt, rais alikuwa na kalamu kadhaa kuweka saini katika hati mbalimbali za kisheria, hivyo ni sawa na historia kuendelea kuenziwa.
Rais Donald Trump alikejeli kuwa aliishiwa kalamu wakati akiweka sahihi yake wakati anaapishwa kuwa rais - huku rais Barack Obama alitumia kalamu 22 kuweka sahihi mkataba wa huduma ya afya nafuu.
Bi Pelosi amekosolewa kwa kutumia kalamu nyingi kwa kuweka sahihi yake katika hati ya mashtaka - Republican wanasema kuwa sio sahihi kuonekana kushangilia jambo ambalo si jema kusheherekewa.
Ofisi yake ilijibu kuwa mashitaka aliyokuwa anayasaini ni janga la kihistoria kutokea wakati katiba na utawala wenyewe unajieleza wazi.
Miaka ya 1998, Seneta wa Republican vilevile walitumia kalamu baada ya kusaini mashtaka yaliyokuwa yanamkabili rais Bill Clinton - ingawa kalamu hizo zinaelezwa kuwa zilikuwa zinaandika kimakosa.
Lakini siku ya alhamisi, seneta mkuu aliingilia kati utaratibu kwa kuwaamuru kila mtu awe kimya wakati wengine wakisikitishwa kwa kupitishwa kwa madai hayo dhidi ya rais wa Marekani Donald John Trump,
Kwa nini shughuli hii ilitakiwa kuwa rasmi sana?
Maneno mengi yaliyotumika yalikuwa yameandaliwa na seneta tangu mwaka 1868 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1986.
Katika historia ya Marekani, hii ni mara ya tatu kwa rais kukabiliwa na mashitaka nchini humo- kuna taratibu nyingi zinazopaswa kufuatwa kama zilivyopangwa kwa miongo kadhaa.
Utamaduni huu unaelezwa kuwa ni shughuli au maadhimisho yanayotakiwa kuonyesha umuhimu wa jambo fulani kwa kile ambacho kinatokea.
Kusainiwa kwa kitabu cha Oath
Sheria ambazo Seneti amezipanga katika mashtaka hayo yanaeleza wazi ni wakati gani rais au makamu wa rais anapokutana na mashtaka dhidi yake mahakama kuu inapaswa kufanya.
Mwendesha mkuu wa mashtaka anapaswa kuapa rasmi mbele ya maseneta 100 ambao watasini kitabu cha Oath ambacho ni hifadhi ya taifa.
Seneta aliweka utaratibu maalum katika mashtaka ya rais Trump, kumtaarifu mashtaka ambayo yanamkabili.