Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo Mashariki ya kati: Tahadhari kuhusu usalama yatolewa
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa taarifa ya tahadhari ya kiusalama. Katika taarifa yake ambayo ipo katika mitandao ya kijamii ya ubalozi huo, Marekani imewataka raia wake wawe makini kuhusu masuala ya usalama kutokana na 'mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati'.
Taarifa imewaonya raia Wamarekani nchini Tanzania kuwa makini na mazingira waliyopo, wawe watulivu na kuzingatia kwa ukaribu hali ya usalama ya mazingira yao.
Wakati taarifa hiyo haikutaja moja kwa moja mvutano wa Marekani na Iran, taarifa hiyo inaendana na wasiwasi juu ya uwezekano wa Iran kulipiza kisasi katika maslahi na mali za Marekani barani Afrika, kufuatia kuuawa kwa jenerali mahiri wa Iran Kasim Suleimani.
Unaweza kusoma
Mwaka 1998, ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam ulilipuliwa. Wasiwasi unapozidi kuongezekana juu ya mvutano huu wengi wanadhani kwamba aidha Iran au wafuasi wake wanaweza kuchagua Afrika kama moja ya sehemu rahisi za kuidhibu Marekani.