Picha 20 za Rais Putin aliyeingia madarakani kama rais mwaka 1999

Chanzo cha picha, Getty Images
Vladimir Putin anakaribia kuadhimisha miaka 20 tangu alipochukua uongozi kama rais na waziri mkuu, Je unakumbuka nini kuhusu hatua za kisiasa alizopiga na matukio maarufu ya michezo aliyohudhuria?
Bill Clinton alikuwa katika Ikulu ya Marekani wakati aliyekuwa afisa wa usalama wa taifa anaingia madarakani kama rais Desemba 31, 1999.
Katika kipindi cha miaka 20, Marekani imefanikiwa kuwa na marais watatu huku Uingereza ikiwa na mawaziri wakuu watatu.
Kuanzia migogoro duniani, kashfa za ndani ya nchi hadi ushindi katika nyanja ya spoti na picha zinazosemekana kuwa propaganda tu, tunaangazia twasira inayomueleza Putin katika kipindi cha miaka 20 madarakani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Putin tayari alikuwa amechaguliwa kama waziri mkuu wakati Urusi ilianzisha vita vya pili vya Chechen Oktoba 1999, ikijibu msururu wa mashambulizi ya mabomu katika maeneo ya makazi.
Awali, uongozi wake ulighubikwa na mgogoro katika eneo la kusini. Vikosi vya Urusi vilizingira na kuvamia mji mkuu wa Chechen, Grozny. Mwaka 2003, Umoja wa Mataifa ukaelezea Grozny kama mji ulioharibiwa vibaya baada ya uvamizi huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa miaka mingi Urusi imekuwa ikikumbwa na mashambulio ya kijeshi mfano, 2004 shule ya Beslan ilivamiwa ambapo watu 330 walipoteza maisha yao wengi wao wakiwa watoto.
Rais Putin hakumaliza oparesheni hiyo hadi mwaka 2009.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Bwana Putin alithibitishwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa Machi 2000, na ndani ya miezi kadhaa akajikuta akiwa katika ya mgogoro wa kiuongozi.
Kukatokea janga baada ya nyambizi ya Kursk kuzama majini na kusababisha vifo vya watu 118.

Chanzo cha picha, ITAR-TASS/AFP via Getty Images
Nyambizi ya Kursk ilipozama mwaka 2000, serikali ya Urusi ilichukua muda mrefu kufahamisha jamaa za wahusika na pia rais hakurejea mara moja kama ilivyotarajiwa na wengi kutoka Bahari nyeusi alikokuwa mapumzikoni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kipindi cha miaka kumi ya kwanza madarakani, Vladimir Putin alikuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa nchi za magharibi licha ya kwamba alikosoa sana sera zao.

Chanzo cha picha, ITAR-TASS/AFP via Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi ilikuwa mwenyeji wa mkutano wake wa kwanza wa G8 mwaka 2006, na kuthibitisha uanachama wake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Chini ya katiba ya Urusi, Bwana Putin hangeweza kugombea urais kwa awamu ya tatu mfululizo, hivyo basi mwaka 2008, akawa waziri mkuu kwa kindi cha miaka minne.
Kuna wachache waliomuona Rais Dmitry Medvedev kama kibaraka wa Putin aliyefanyakazi kwa niaba ya mkuu wake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Georgia ilipotuma vikosi vyake ili kuchukua tena udhibiti wa eneo la kusini mwa Ossetia 2008, Urusi iliendelea kuvamia Georgia.
Hatua hiyo ilikwa kama onyo kwa mataifa ya magharibi lakini uamuzi wa Urusi wa kuvamia mashariki mwa Ukraine ulizidisha kuzorota kwa uhusiano kati ya Putin na viongozi wa nchi za Magharibi.
Hatua ya Urusi ya kutwa eneo la Krimea kutoka kwa Ukraine ilisababisha Umoja wa Ulaya na Marekani kuiwekea Urusi vikwazo na kusitisha uanachama wa nchi hiyo katika muungano wa G8.

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Syria ikiwa imeendelea kushuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka minne, Urusi iliingilia kati na kumuunga mkono mshirika wake, Rais Bashar al-Assad, ambaye serikali yake ilikuwa inakaribia kuanguka.
Uamuzi wa Putin wa kutuma ndege za Urusi na mavazi ya kijeshi Syria, kulibadilisha hali iliyokuwa inaendelea.

Chanzo cha picha, TASS/Getty
Baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Urais wa Marekani 2016, Idara ya ujasusi ya Marekani ilithibitisha kwamba Urusi iliingilia kampeni za uchaguzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia unaweza kusoma:
Mwaka 2018, Uingereza iliishutumu Urusi kwa kumtilia sumu afisa aliyekuwa jasusi wa nchi hiyo Sergei Skripal huko Salisbury.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kipindi chake chote madarakani, Rais wa Urusi amekuwa akijaribu kudhibiti picha zake na za Urusi kama nchi kwa ujumla. Picha kadhaa zilizotolewa na kiongozi huyo kwa miaka kadhaa zimekuwa zikijaribu kumuonesha kama kiongozi imara.

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia amejitahidi katika kuimarisha michezo nchini Urusi kwa kuwa mwenyeji wa mshindano ya Olimpiki msimu wa Baridi mwaka 2014 na mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.
Mashindano ya dunia yaliofanyika Sochi yalikuwa ya mafanikio makubwa lakini athari zake baada ya wanariadha wake kushtumiwa kwamba wametumia dawa za kuongeza nguvu bado yanaendelea kuonekana.
Shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini duniani limepiga marufuku washiriki wa Urusi kushiriki michezo yote maarufu kwa miaka minne. 2015, ripoti yao ilisema kwamba Urusi ilikuwa imetekeleza kile kinachoweza kuchukuliwa kama mpango wa serikali wa kuongeza wanariadha wake nguvu. Na mwezi huu, ilibainika kwamba Urusi imeingilia data ya maabara iliyotolewa Januari kwa ajili ya utafiti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Huku mashindano ya soka ya dunia yaliyofanyika Urusi 2018 yakichukuliwa kama mafanikio ya kimataifa, shutuma za wanariadha wake kutumia dawa za kuongeza nguvu kuna maanisha kwamba Urusi haitashiriki katika mashindano yajayo yatakayofanyika Qatar mwaka 2022.
Picha zote zina haki miliki.












