Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Brexit: Je ni kipi kinachotarajiwa ?
Chama cha Conservative kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Uingereza .
Je matokeo hayo yanmaanisha nini kuhusiana na Brexit?
Tarahe ya Brexit - wakati Uingreza itakapoondoka katika muungano wa Ulaya - inatarajiwa kuwa Januari 31 2020.
Waziri mkuu Boris Johnson aliweka makubaliano na EU lakini ni lazima yapitie bungeni. Hatahivyo iwapo makubaliano hayo hayataidhinishwa na bunge basi Uingereza itajiondoa bila mkataba wowote na EU.
Conservative imepata ushindi mkubwa- Je itapitisha Brexit bungeni?
Huku kikiwa na uwakilishi mkubwa bungeni , chama cha Conservative huenda kikaidhinisha makubaliano hayo ya bwana Johnson ya Brexit.
Inadaiwa kwamba kuna uwezekano itawasilisha upya muswada wa makubaliano ya kujiondoa - kifungu cha sheria kinachotoa msingi wa Brexit kufanikishwa - wiki ijayo. Lengo litakuwa kuhakikisha kuwa Brexit inafanyika tarehe 31 Januari.
Je ni nini kitafanyika baada ya Brexit?
Iwapo Uingereza itajiondoa katika muungano wa EU mnamo tarehe 31 mwezi Januari , hiyo itakuwa hatua moja katika mchakato mgumu sana.
Hatua ya kwanza itakuwa kuanza majadiliano ya makubaliano na Muungano wa Ulaya . Uingereza inapendelea sana kuweza kuuza bidhaa zake katika soko la Ulaya.
Lakini chama cha Conservative kimeweka wazi kwamba Uingereza lazima iachane na umoja wa forodha , soko moja la Ulaya na kumaliza utawala wake katika mahakama ya Ulaya ya Haki.
Muda ni mfupi . Muungano wa Ulaya unaweza kuchukua wiki kadhaa kuingia katika mkataba rasmi - huku wanachama 27 wa muungano huo waliosalia wote wakikubaliana.
Hiyo inamaanisha kwamba mazungumzo rasmi yataanza mwezi Machi. Mazungumzo hayo yatahitaji kutoa makubaliano ya mwishio kufikia mwezi Juni .
Huo ndio wakati ambapo Uingereza itaamua iwapo itaongeza muda wa mpito kwa mwaka mmoja lakini bwana Johnson amekataa nyongeza yoyote.
Iwapo itakuwa hakuna makubaliano yoyote ya kibiashara ambayo yatakuwa yameafikiwa kufikia mwisho wa mwezi Juni, basi Uingereza itakabiliwa na uwezekano wa kuondoka bila makubaliano yoyote mwisho wa mwezi Disemba 2020.
Iwapo makubaliano yataafikiwa , pia lazima yaidhinishwe kabla ya kuanza kutumika na huo ni mchakato ambao unaweza kuchukua miezi kadhaa.
Hakuna mkataba wowote wa kiabiashara wa kiwango kama hiki ambao umewahi kuafikiwa kati ya EU na taifa jingine la nje kwa haraka kama ilivyopangwa wakati huu.
Bwana Johnson amesema kwamba kwa vile Uingereza inafuata sheria za EU , majadiliano hayo yatakuwa ya moja kwa moja .
Lakini wakosoaji wamesema kwamba Uingereza inataka kuwa na uhuru wa kujiondoa katika sheria za EU ili iweze kuingia katika makubaliano na mataifa mengine - swala litakalofanya mazungumzo kuwa magumu.
Sio tu mkataba wa kibiashara unaotarajiwa kutatauliwa. Uingereza lazima ikubali jinsi itakavyoshirikiana na Muungano wa Ulaya katika maswala ya usalama na kufuata sheria.
Uingereza inatarajiwa kuondoka katika mfumo wa agizo la mahakama la kukamatwa na itaamua kitakachochukua nafasi yake,
Pia ni sharti ifanye makubaliano katika maeneo mengi ambapo ushirikiano utahitajika.