Mfahamu Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza

Alipoingia kwenye ofisi ya Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza, wakosoaji wake walidai hakuwa chaguo la watu.

Boris Johnson alimrithi Theresa May kama kiongozi wa chama cha Conservative baada ya kupigiwa kura na wajumbe 160,000.

Kwa mujibu wa taratibu za demokrasia ya Uingereza, Kiongozi wa chama chenye uwakilishi mkubwa bungeni huwa waziri mkuu, na hivyo baada ya kupigiwa kura za chama, Boris akashika hatu za juu za uongozi wa Uingereza.

Lakini katika uchaguzi wa jana Alhamisi ambao matokeo yake yamewekwa bayana leo Ijumaa, wamepaza sauti zao juu ya Boris, baada ya kukipa ushindi chama cha Conservative kwenye uchaguzi mkuu wa Uingereza.

Boris ametengeneza jina lake kwa kugawa mawazo ya watu na kuchochea migongano, awali akiwa mwanahabari na baadae mwanasiasa.

Baada ya kuchukua hatamu za uongozi wa chama, wengi walimbeza kuwa hana ujuzi wa kutosha wa kukiongoza chama.

Lakini, matokeo haya sasa yanaonesha hali ya tofauti. Swali ni amefikaje hapa alipo?

Asili ya Kituruki na maisha jijini Brussels

Boris toka mwanzo alijipambanua kama mtu mwenye mashaka na Muungano wa Ulaya.

Alizaliwa jijini New York baba yake akiwa mwanadiplomasia na mama yake msanii. Babu yake mkuu alikuwa ni mwandishi wa habari wa Kituruki.

Amekulia Marekani, Uingereza na Ubelgiji kabla ya familia yake kurejea rasmi nchini Uingereza.

Amesoma Eton, shule maarufu zaidi ya wavulana nchini Uingereza, na huko ndipo dalili za tabia na mtu gani angekuwa zilianza kuonekana.

Kutoka hapo akaenda Chuo Kikuu cha Oxford, na kuchaguliwa kuwa raisi wa chama cha midahalo cha chuo hicho.

Tabia yake ya kuchochea malumbano ilionekana wazi akiwa mwandishi.

Alitimuliwa kazi katika gazeti la The Times baada ya kughushi nukuu.

Baada ya hapo akaajiriwa kama ripota wa jijini Brussels wa gazeti linaloogemea mrengo wa chama cha Conservative la The Daily Telegraph.

"Uandishi wake ulichanganya kwa umaridadi uhalisia na mabo ya kubuni dhidi ya Umoja wa Ulaya," anaeleza mhariri msaidizi wa BBC wa habari za siasa, John Pienaar.

Habari alizoandika zilizaa mjadala mkubwa na mashambulizi dhidi ya Umoja wa Ulaya ambayo baadae alikuja kuyaendeleza kama mwanasiasa.

Lakini baadhi ya waandishi wenzake walimtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu kwa taaluma yake.

Mwandishi wa maoni

Hapo awali nchini Uingereza alikuwa mwandishi wa makala katika gazeti la The Telegraph na baadae mhariri wa gazeti la mrengo wa kulia, The spectator.

Johnson alionesha mwelekeo wa kuwakosea baadhi ya wasomaji, kwa kutumia maneno ya kejeli kuwaelezea watu weusi na kuwaita watoto wanaolelewa na mama mzazi peke yake kama ''watoto ambao hawajelelewa vizuri, wajinga, wenye fujo, na wasio halali.''

Lakini aliliongezea mashabiki gazeti hilo na wasifu wake katika vyombo vya habari ukakua na akaanza kuonekana katika kipindi cha kila siku kiitwacho ''Have I Got News For You?'' ambacho washiriki hujaribu kufanya ucheshi kuhusu habari za wiki.

Kama maneno na maoni yake yalivutia ukosoaji, basi pia yalimfanya awe mtu maarufu katika siasa, kulingana na maneno ya watoa maoni wengi akiwemo aliyemwandikia historia ya maisha yake, Sonia Purnell. Na hiki ndicho kilichomsaidia kwenye mwanzo wake katika siasa.

Mwaka 2001, Johnson alikuwa Mbunge, akikiwakilisha chama cha Conservative katika wilaya ya Henley-on-Thames, karibu na Oxford.

Katika uchaguzi wa mwaka 2007 kama meya wa London ndio uliompaisha kwa kasi kubwa katika jukwaa linalojulikana ulimwenguni.

Wakati macho yote duniani yakiiangalia mji ambao ulikuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2012, Jonson alikuwa balozi wa michezo hiyo, ingawaje hayakuandaliawa na City Hall.

Moja ya programu zake maarufu za usafiri alizozianzisha ni uliojulikana kama mpango wa kuendesha baiskeli ''Boris Bike'', na ulianzishwa mwezi July mwaka 2010.

Ni ushahidi tosha wa nafasi yake iliyochangyika siasa na umaarufu wake, ambao umemfanya ajulikane kama Boris.

Siku zote Johnson alipigia debe baiskeli hizo kwa kuziendesha yeye mwenyewe, huku mara moja alionekana akiwa na muigizaji mkongwe wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger.

Wakosoaji wanadai haukuwa mpango wake ila mpango wa meya aliyopita.

Lakini Johnson alikumbana na ukosoaji mkali.

Malengo makubwa ya kutaka kutengeneza daraja la bustani juu ya mto Thames ikiwa kama kumbukumbu ya binti wa kifalme Diana, yalifutwa na mrithi wake, Sadiq Khan, baada ya dola milioni 70 kutumika.

Bingwa wa Brexit

Lakini wakati Johnson akiwa amerudi bungeni baada ya kushinda kiti katika uchaguzi wa mwaka 2015, na mbele ya kura za maoni za Brexit, Msimamo wa Johson katika swal hili ulikuwa bado haueleweki.

Aliandika nakala katika gazeti akiitaka Uingereza iondoke umoja wa ulaya na akaandika nakala nyingine anayoitaka Uingereza ibaki katika umoja wa ulaya.

Lakini alikuja kuamua kuunga mkono hoja ya Uingereza kutoka umoja wa ulaya, kitendo kilichomfanya kwenda kinyume na kiongozi wa chama chake, waziri mkuu David Cameron.

Baada ya ushindi wa kutaka Uingereza kutoka umoja wa ulaya na Cameron kujiuzulu, Johnson aliweka wazi malengo yake yakutaka kuchukua nafasi yake kama kiongozi wa chama cha Conservative.

Lakini Theresa May aliweza kuibuka mshindi badala yake, na wagombea wengine wote walijitoa kugombea nafasi hiyo kabla ya upigaji kura kuanza, Lakini kama shukran kwa Johnson kwaajili ya nafasi yake kama bingwa wa Brexit, akateuliwa kuwa kama katibu wa mabo ya nje.

Wakati wa kampeni za Brexit, Jina la Johnson lilihusishwa na madai kuwa kuondoka umoja wa ulaya kutaruhusu paundi milioni 350 kwaajili ya shirika la afya la taifa, kila wiki.

Hilo halikumchafua kwa watu waliounga mkono Brexit.

Johnson baadae aliamua kuondoka katika baraza la May akidai kuwa anahitaji kuwa shupavu katika mazungumzo na Brussels.

Tangu kiongozi wa chama hicho, na hata Waziri mkuu, Johnson hajawahi kukubali kuondoka umoja wa ulaya bila makubaliano yoyote.

Amesema kama Conservatives wakishinda uchaguzi mkuu, Uingereza itaondoka ifikapo tarehe 21 Januari 2020.

Katika Brexit ya Uingereza, maoni na vinaweza kuwashawishi wapiga kura.

Katika maisha yake, Johnson ameonesha uwezo wake wa kiwango cha juu.