Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Duma wa India atembea kwa muda mrefu zaidi kutafuta 'mke'
Dumaa ametembea mwendo mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini India akisafiri urefu wa kilomita 1,300 katika kipindi cha miezi mitano.
Wataalam wanaamini kwamba mnyama huyo wa kiume anatafuta chakula ama mke.
Duma huyo ambaye amebandikwa mkufu unaoweza kuonyesha kule aliko , aliondoka eneo analoishi katika eneo moja la wanayapori katika jimbo la magharibi la Maharashtra mwezi Juni.
Baadaye alichunguzwa akirudi kupitia mashamba, majini barabarani na kufika katika jimbo jirani.
Kufikia sasa simba marara huyo amelumbana na binadamu mara moja baada ya kumjeruhi kimakosa mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa kundi ambalo lilikuwa limeingia msitu ambao mnyama huyo alikua akipumzika.
Duma huyo kwa jina C1 alikuwa miongoni mwa watoto watatu waliozaliwa na T1 , simba marara jike katika hifadhi ya wanyamapori ya Tipeshwar, ambako ni nyumbani kwa simba marara 10 katika jimbo la Maharashtra.
Aliwekewa mkufu huo wa kielektroniki mnamo mwezi Februari na akaendelea kuzurura msituni hadi wakati wa mvua za upepo mkali ili kutafuta eneo zuri la kuishi.
Mnyama huyo aliondoka katika hifadhi hiyo mwisho wa mwezi Juni, na tangu wakati huo ametembea kupitia wilaya tatu katika jimbo la Maharashtra na jimbo jirani la Telangana.
Wikendi iliopita alionekana katika hifadhi nyengine ya wanyama huko Maharashtra.
Hofu za mawasiliano
Maafisa wa wanyamapori wanasema kwamba simba marara huyo hajasafiri kwa mstari mmoja. anachunguzwa kupitia Setlaiti ya GPS kila saa na amerekodiwa katika zaidi ya maeneo 5000 katika kipindi cha miezi tisa. Simba marara huyo anatafuta eneo , chakula na mke .
Maeneo yanayopendwa sana na simba marara nchini India yamejaa hivyobasi simba marara wapya wanahitajika kutafuta maeneo mengine, alisema daktari Bilal , mwanabaiolojia mwandamizi wa taasisi ya wanyamapori India aliyzungumza BBC.
Duma huyo hujificha wakati wa mchana na hutembea wakati wa usiku , akiua nguruwe mwitu na ng'ombe kwa lengo la chakula.
Dkt. Habib alithibitisha jeraha moja alilopata mtu aliyeingia katika msitu ambapo simba marara huyo alikuwa akipumzika , lakini akasema kwamba hakujakuwa na mgogoro wowote dhidi ya bindamu.
Watu hata hawajui kwamba simba marara huyu anatembea karibu na makaazi yao.
'Hatahivyo maafisa wa wanyama pori wanasema simba marara huyo atahitaji kukamatwa na kupelekwa karibu na misitu iliopo ili kuzuia ajali zozote', maafisa wa misitu wanasema.
Pia wanahofia watapoteza mawasiliano katika siku za hivi karibuni kwa kuwa betri ya mkufu wa kielektroniki umepungua nguvu kwa asilimia 80.
'Idadi ya duma imepungua nchini Indi , lakini maeneo wanayoishi pia yamepungua na hakuna chakula' , wanasema wataalam.
Kila duma anahitaji takriban wanyama 500 katika eneo lake ili kuhakikisha kuna hifadhi ya chakula, wanasema wataalam.