Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simba mlinda nyumba karibu na shule akamatwa Nigeria
Hebu tafakari hili, unatembea mjini halafu upite karibu na nyumba inayolindwa na simba wala sio mbwa.
Hiyo ndio hali waliokumbana nayo wakazi mjini Lagos, Nigeria baada ya mmiliki wa nyumba moja kuamua kutumia simba kama mlinzi.
Simba huyo wa miaka miwili aliripotiwa kuonekana katika nyumba moja ya makazi iliyo karibu na shule na kundi la jopokazi siku ya Ijumaa.
Simba huyo alikamatwa na kuhamishiwa katika hifadhi ya wanyama ya Bogije Omu mjini Lekki, mkuu wa jopo kazi hilo aliiambia BBC.
Mmiliki wa mnyama huyo ameamriwa kufika katika kituo cha polisi mara moja la sivyo akamatwe.
Kundi hilo linalojihusisha na masuala ya usafi wa mazingira na kitengo cha upambana na uhalifu mjini Lagos liliingilia suala hilo baada ya wakazi kuwasilisha ripoti kwa wizara ya mazingira.
Msimamizi wa shule hiyo amesema kuwa walitilia maanani usalama wa watoto.
Inaaminika kuwa simba huyo aliletwa katika nyumba hiyo miezi miwili iliopita.
Pia unaweza kusoma