Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nashami Wangara: mwanamke aliyekabiliwa na uraibu wa ngono kwa miaka sita
- Author, Anne Ngugi
- Nafasi, BBC Swahili
Nashami Wangara,38, ama Florence, kama wengi wanavyomuita ni mzaliwa wa magharibi mwa Kenya ambaye ameamua kuandika kitabu kuhusu maisha yake ambacho amekipa jina "My Story for his Glory" kumaanisha (Hadithi yangu kwa Utukufu wake).
"Nilipokuwa msichana mdogo nilikuwa mnyenyekevu na sikujua mambo mengi kuhusu maisha lakini nilipofikisha miaka 18 mambo yalibadilika," anasema, Nashami.
Anaongeza kuwa wakati mwingine alikuwa Anatoroka nyumbani na kurejea asubuhi hadi wakati mmoja mama yake mzazi akamshauri kuamua ikiwa anataka kuendelea kuishi naye au kutoka.
''Niiliamua kuondoka "anasema.
Bi Nashami alianza uhusiano wake wa kimapenzi wa kwanza na mwanamume na hatimae akaanza kuishi nae alipoondoka nyumbani kwao.
Haikuchukua muda mrefu, uhusiano hu ulianza kukumbwa changamoto, hali ilisabisha waachane baada ya kushindwa kusuluhisha tofauti wao.
Hatua hiyo anasema ilimuathiri sana, ''Niliamua sitawahi kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na mtu mmoja''
Akiwa na umri wa miaka 21 akaamua kuwa kila wakati atakuwa na wapenzi zaidi ya wawili ili mmoja akimuudhi awe na wengine.
Ni hapo ndipo alianza kutekwa na uraibu wa ngono.
''Nilianza kama mchezo kwa kuwa nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume zaidi ya wawili'', Nashami alisema.
Pia anasema ilikuwa rahisi kutimiza matamanio yake kwa kuwa ni kitu alichohitajika kufanya kila wakati alipokuwa na mpenzi wake.
Kwa muda wa miaka sita mwanamke huyo alikabiliwa na hali ya kufanya ngono kama uraibu.
Ukombozi wake kwa ngono kati ya mume na mke.
Bi Nashami aliamua kuokoka baada ya kuvutiwa na huduma ya uimbaji na uadilifu wa watu walioimarisha imani yao kidini.
Lakini kwa sababu dini ya Kikristo hairuhusu ngono nje ya ndoa,alijikuta ameingilia uraibu mpya wa kupiga punyeto.
''Nilikuwa naweza kujipiga punyeto kama mngonjwa aliyeandikiwa dawa na Daktari, asubuhi mbili jioni mbili" Asema Bi Nashami.
Alikuwa mmoja ya waimbaji kwenye Kwaya kanisani na hali hiyo ilimfanya alijihisi mchafu na asiyekuwa na dhamana.
Ni tabia ambayo yeye mwenyewe hakuipenda na kila mara ilimfanya ajihisi aibu sana wa miaka kumi alikuwa mateka.
Ukombozi wake anasema ulikuja wakati ambapo alifanya maombi maalum. Pia alikuwa anaandamana na watu ambao hawakumhukumu bali walimpatia mawaidha ya jinsi ya kuondokana na hali hio.
Bi Namashi anasema kuwa sio rahisi kujiondoa katika uraibu wa ngono na Punyeto lakini inawezekana.
Kwa sasa anawahamasisha vijana kutojiingiza katika hali kama yake.
Mtazamo wa ngono na ponyeto kama uraibu kimatibabu ni upi?
Mwanasaikolojia, Cate Mathea, ambaye pia ni daktari bingwa wa uraibu wa ngono anasema njia rahisi ya kugundua kuwa mtu ametekwa na uraibu huo ni kutathmini maongezi yake.
Kichochezi kikuu anasema ni mawazo ya mtu kuwa kwenye maswala ya ngono na jinsi ya kujichua.
"Kupiga punyetosio tabia mbaya lakini mtu anapoifanya kila wakati na inapokuwa tu ndicho kitu mtu anachokifikiria kila mara kila wakati inageuka na kuwa na uraibu"
Daktari Mathea anasema kuwa punyeto hutumiwa sana na vijana wanapovunja ungo kama njia ya kuondoa ule msukumo wa kawaida wa mwili.
Homoni aina ya estrogen huwa kwa mwili wa kila binadamu, kusaidia katika shughuli za ngono kwa watu wazima, alisema.
''Homoni ya estrogeni ikiwa nyingi mwilini,mtu anakuwa na hamu ya kufanya ngono kupita kiasi''
Mtaalamu huyo anaongezea kuwa hali hiyo hudhibitiwa kwa dawa ambazo mtu hupewa ili kupunguza nguvu ya homoni ya estrogen mwilini.
Unawezaje kujiepusha na uraibu wa ngono?
Mwanasaikolojia Cate Mathea, anashauri watu kutotizama filamu za ngono kila wakati.
Pia anasema 80% ya watu wanaokabiliwa na uraibu wa ngono ni wale ambao walidhulumiwa kingoni wakiwa watoto wadogo.