Hedhi inastahili kuwa suala la faragha lakini sio siri

Amika George

Chanzo cha picha, The Pink Protest

Maelezo ya picha, Amika George alianzisha kampeini kuhusu umasikini unaotokana na hedhi akiwa na miaka 17
Muda wa kusoma: Dakika 3

Wanawake wa matabaka mbali mbali wamekua wakisimulia masuala ya hedhi katika mitandao ya kijamii.

Hii ni sehemu ya mkakati wa kuhamasisha umuhimu wa kuzungumzia wazi wazi masuala ya hedhi matandaoni kwa kutumia hashtag #FreePeriodStories, ambayo wanaharakati wanaamini itasaidia kukabiliana na unyanyapaa unaozunguka suala hilo.

Watu wanazungumzia nini na kwanini mjadala huu ni muhimu?

Kwa wengine ni hadithi za kuchekesha na za kuabisha.

Emma aliwasilisha ujumbe huu kwa Twitter:

"Tafakari wakati unapomuelekeza rafiki yako jinsi ya kutumia tampon au taulo ya hedhi kwa mara ya kwanza, ukiwa umesimama nje ya choo, anatoka njee akionekana kuwa na wasi wasi, unamuangalia tena na kugundua bwanawee... nilitumia maneno ya kuaibisha... ndio hali ilivyo #freeperiodstories."

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kwa wengine, kama Natasha, inamaanisha kuangazia suala hili kwa wanaume:

"Siku moja niliangusha mkoba wangu kwa bahati mbaya tampons saba zikatapakaa kwenye sakafu. Mpenzi wangu alipoinama kunisadia kuokota vitu vyangu vilivyomwagika, nakumbuka nilishtuka na kusema kwa sauti 'SI ZANGU!' Hadidhi yako ni gani#freeperiodstories?"

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Kando na simulizi za kuchekesha baadhi ya simulizi hizo ziliangazia jinsi hali hizo zinaweza kuchangia kitu kinachohitaji kushughulikiwa kwa dharura.

Alice aliandika kuhusu jinsi alivyokabiliwa na maradhi ya endometriosis (kuumwa na tumbo kupita kiasi wakati mtu anapopata hedhi) hatua iliyovutia simulizi zaidi kuhusu hali hiyo:

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

'Tunashughulikia suala hili peke yetu'

Hashtag hiyo ilizinduliwa na wasichana nchini Uingereza chini ya usimamizi wamwanaharakati Amika George.

Mwaka huu alifanikiwa kuongoza kampeini hiyo nchini Uingereza kwa kutoa bure taulo za hedhi katika shule za msingi na sekondari.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Anasema alianza mkakati huo kwasababu mdahalo kuhusu masuala ya hedhi "lazima iendelee" ili kufikia malengo yao.

"Kuanzia tukiwa wasichana wadogo, tulifunzwa kunong'onezana tunapozungumzia hedhi, au kutoangazia kabisa suala hilo mbele ya watu au hata kwa marafiki. ''Tunashughulikia suala hili peke yetu," alisema.

"Tunahitaji kubadilisha dhana kwamba hedhi sio swala linalostahili kujadiliwa hadharani."

Anaongeza kuwa unyanyapaa unaozunguka masuala ya hedhi ulimfanya kusalia "kimya" siku zilizopita.

"Nimekutana na watu wanaotoa visababu na kubadilisha mkondo wa mazungumzo punde ninapoanza kuzungumzia umasikini unaochangiwa na hedhi," anasema

'Tunahitaji kujua ukweli tangu tukiwa wadogo'

Kwa Celia Hodson, ambaye ni mwanzilishi wa mkakati unaofahamikakama Hey Girls, nchini Uskochi anasema kusimulia hadihi kuhusu hedhi kunaweza kusaidia kukabiliana na unyanyapaa.

Celia Hodson

Chanzo cha picha, Celia Hodson

"Msichana mmoja alitueleza kuwa rafiki yake wa kiume alimuuliza kwa nini hakusubiri hadi afike nyumbani ndio apate hedhi," anasema.

Utafiti uliofanywa na Hey Girls, unaashiria kuwa 48% ya wsichana na wanawake wanaona haya kuzungumzia masuala ya hedhi.

Anadhani mabadiliko hayo yanaweza kufikiwa kupitia elimu.

Ucheshi unavyoweza kusaidia

Gabby Edlin, Mwanzilishi wa mradi wa kuhamasisha masuala ya hedhi unaofahamika kama Bloody Good Period, anasema kicheko kinachohusiana na hedhi kinaweza kuchangia mazungumzo yenye tija.

Anaongeza kutokua na na uwezo wa kununu atau li za hedhi sio tatizo pekee - kutozungumzia hedhi pia kunaweza kuwa na madhara.

"Ikiwa mwiko huo utavunjwa, ni kumaanisha tunaweza kuangazia masuala ya hedhi magazetini bila kupepesa macho, lakini unyanyapaa unamaanisha watu bado wanaathiriwa,"alisema.

"Kuanzia hali ya mtu kutoweza kwenda msalani kwasababu mwalimu darasani amekuzuia na huwezi kusema unataka kwenda kubadilisha taulo ya hedhi'."

Chella Quint

Chanzo cha picha, Chella Quint

Hedhi inastahili kuwa suala la faragha lakini sio siri

Affi Parvizi-Wayne, mwanaharakati na mwanzilishi wa kampuni ya Freda inayotengeneza bidhaa za kujisitiri wakati wa hedhi, anahoji baadhi ya majina yanayotumiwa kuangazia hedhi.

"Hedhi kama kazi yoyote ya mwili ni ya faragha, sio ya siri,".

Anasema wawekezaji watarajiwa katika kampuni yake walionesha ukosefu wa "ufahamu wa kimsingi", walipohoji kwanini biashara yake inajumuisha siku za likizo na wikendi.

Affi Parvizi-Wayne

Chanzo cha picha, Affi Parvizi-Wayne

"Ilinibidi nielezee kwamba hedhi haijali kama mtu yuko likizo au la!"

"Mjadala kuhusu hedhi unastahili kuendelezwa hadi pale taulo za hedhi zitakuwa jambo la kawaidi," anasema.

Mabadiliko ya kweli anasema, yatafikiwa kupitia ''upatikanaji wa taulo za hedhi kila sehemu".