Bibi harusi akiuka utamaduni wa jadi kutetea haki za wanawake Bangladesh

Khadiza Khushi bibi harusi mwenye umri wa miaka 19 ameamua kukiuka utamaduni wa jadi wa ndoa katika jamii yake kutetea usawa wa kijinsia katika jamii ya Wabangladesh.

Bi harusi huyo ameandamana na familia yake na kwenda kwa mumewe kama sehemu ya kupigania haki za wanawake.

Alifanya hivyo kwa niaba ya wanawake wote wa Bangladesh ambao anatarajia wataiga mfano wake.

"Ikiwa wanaume wanafanya hivyo mbona wanawake pia wasipewe nafasi hio?" aliuliza Idhaa ya BBC ya Kibengali siku kadhaa baada ya ndoa yake na Tariqul kuzua gumzo mitandaoni.

Hatua hiyo pia imezua hisia mseto huku baadhi ya watu wakiipongeza na wengine wakielezea kughabishwa kwao na maharusi hao .

Mtu mmoja alipendekeza wanandoa hao na familia zao wanastahili kuadhibiwa vikali.

Lakini kwa Khadiza na mume wake hatua hiyo lilikua jambo la busara.

"Suala la utamaduni halina msingi wowote hapa ," aliimbia BBC. "Suala muhimu hapa ni haki za wanawake,''alisema

Kulingana na utamaduni Bwana harusi na jamaa zake wanatembea hadi nyumbani kwa kina bi harusi, ambako ndoa hufungwa na sherehe ya harusi kuandaliwa, kabla ya bi harusi kuagana na familia yake na kwenda nyumbani kwa mume.

Utamaduni huo umekua ukifanyika tangu zamani.

Lakini katika Wilaya ya Meherpur, magharibi mwa Bangladesh, kulifanyika jambo la kipekee: Bi harusi na familia yake walitembea hadi nyumbani kwa bwanaharusi kufunga ndoa na baada ya hapo bwana harusi alienda nyumbani kwa kina mke wake.

Umuhimu wa hatua hiyo haujaeleweka: kwa wanaume wengi ni kitendo cha kujidhalilisha. Baadhi ya watu walighadhabishwa na hatua hiyo.

Sio vijijini tu, jambo kama hilo halifanyika hata katika miji mikuu ya Bangladesh, bila shaka maharusi hawa wameanza maisha yao ya ndoa kwa kuonesha ujasiri wa hali ya juu.

Hata h iv yo Bangladesh imepiga hatua kubwa katika juhudi za kupigania usawa katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Jumuiya ya uchumi duniani, Taifa hilo limeorodheshwa kuwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usawa wa kijinsia Kusini mwa bara Asia.

Lakini suala kuu linasalia kuwa, kifo cha Nusrat Jahan Rafi - mwenye umri wa miaka 19, ambaye aligonga vichwa vya habari baada ya kudai kuchomwa moto hadi kufa kwasababu ya kulalamikia unyanyasaji wa kingono aliotendewa na mwalimu wake mkuu.

Huku hayo yakijiri Umoja wa Mataifa umesema kua thuluthi mbili ya wanawake walioolewa duniani watanyanyasika mikononi mwa waume zao huku nusu yao wakiripoti visa vya dhulma dhidi yao mwaka uliopita.

Japo hali ya wanawake inaendelea kuimarika katika masuala kama ya elimu, sheri aya ndoa katika nchi hiyo iliyo na idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislam limekosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu kuwa ya kibaguzi.