Bibi harusi akiuka mila na tamaduni za ndoa nchini Bangladesh

Khadiza Khushi bibi harusi mwenye umri wa miaka 19 ameamua kukiuka tamaduni ya jadi ya jamii yake kuwa bwana harusi hutoka kwao kwenda kwa nyumbani kwa bibi harusi na kumchukuwa.Bibi harusi huyo ameandamana na familia yake na kwenda kwa mumewe na kusema hii ni njia tu ya kupigania haki za wanawake.