Fatma Karume: Mwana wa Abeid Karume avuliwa uwakili Tanzania

Chanzo cha picha, fatma karume/facebook
Wakili Fatma Karume amesimamishwa kufanya kazi za Uwakili Tanzania bara,
Maamuzi hayo yametolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na katibu wa Uenezi wa chama cha ACT wazalendo Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).
Hatahivyo Fatuma Karume amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa bila yeye kusikilizwa.
Mahakama Kuu imeamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Karume amesimamishwa kazi huku sababu yake ikitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliofunguliwa na katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano katika chama cha Wazalendo, Ado Shaibu kupinga uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali Dkt Adelarus Kilangi aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli mnamo February Mosi 2018 kulingana na gazeti la Mwanachi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Shaibu amesema kwamba mawakili wa serikali walilalamikia maneno yalioandikwa na Fatma wakati walipokua wakifungua kesi hiyo mahakama kuu.
''Na nakuu gazeti la mwanachi: hata iwapo kesi hii itashindwa ataendelea kupambana nayo, rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana''.
Shaibu amenukuliwa na gazeti hilo akisema kwamba uamuzi huo umetangazwa huku madai katika kesi ya msingi yakitupiliwa mbali kwa hoja kwamba rais hawwezi kusimamishwa mahakamani.
Alipoulizwa kuhusu hatua dhidi yake, fatma amesema kuwa anakusudia kufungua kesi katika mahakama ya haki afrika mashariki EACJ kupingana kusimamishwa kwake uwakili bila kupewa nafasi ya kujieleza.
Amesema kwamba hashangai kusimamishwa kazi au kuvuliwa uwakili kwa sabbau yapo mengi yaliotokea nchini,
Mimi sishangai kuvuliwa au kusimamishwa uwakili ,pengine Mungu hataki niendelee kuwa huko , pemngine anataka niingie kwenye siasa au nifanye kingine tofauti. Nitakaa na kutfakari alinukuliwa na mwananchi akisema.
Hatahivyo amesema kwamba hatua hiyo haitabadili maisha yake bali itabadilisha uwezo wake wa kusimamia kesi za kikatiba , akibainisha kuwa bado ni wakili Zanzibar, ana ofisi na ataendelea kusimamia kesi za kikatiba.













