Paul Whelan: Askari wa zamani wa Marekani anadai ametumiwa katika kesi ya ujasusi ya Urusi

Paul Whelan in a defendant's cage in Moscow's court. Photo: August 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Paul Whelan was held in December after taking a group on a tour of the Kremlin museums
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mwanajeshi wa zaman wa kikosi cha majini cha Marekani Paul Whelan, ameishutumu Urusi kwa kufanya upelelezi wa kijasusi na akasema yeye sio jasusi ila alipangiwa njama na rafiki yake Mrusi.

Akizungumza na BBC, Bwana Mr Whelan, ambaye pia ni raia wa Uingereza, Canada na Ireland, amesema kuwa rafiki yake alikuwa amemuwekea kifaa cha kunasa sauti kwenye mfuko wake bila yeye kujua.

Kesi ya rufaa ya Whelan mwenye umri wa miaka 48- ya kupinga kufungwa kwake mahabusu ilikataliwa na mahakama ya Moscow.

Waendesha mashtaka walisema kuwa ''alikamatwa akifanya ufasusi '' na maafisa wa ujasusi wa taifa la Urusi mwaka jana.

Uchunguzi sasa umemalizika, na mawakili wa Bwana Whelan wameanza kuchunguza ushahidi dhidi ya mteja wao.

Kwasababu ni kesi ya ujasusi, taarifa zote kuhus mashtaka yanayomkabili zinafichwa.

Balozi wa Marekani mjini ambassador ametoa wito kwa Urusi kuacha "kufanya mzaha " na kesi .

Paul Whelan amesema nini?

Bwana Whelan ana uraia wa Marekani , Uingereza, Canada na Ireland
Maelezo ya picha, Bwana Whelan ana uraia wa Marekani , Uingereza, Canada na Ireland

Katika mazungumzo ya muda mfupi kupitia vioo vya kizimbani alipokuw amahakamani, Bwana Whelan alielezea hadithi yake kwa mara ya kwanza. Mwandishi wa BBC mjini Moscow Sarah Rainsford anasema

Alimwambia kuwa alikuwa amefanyiwa hila , na kwamba hakutekeleza uhalifu wowote .

"Mtu alikuja katika chumba changu cha hoteli na kuweka kitu ndani ya mfuko wangu, halafu nikakamatwa " Alisema Bwana Mr Whelan.

"Mtu huyo alikuwa ni afisa wa huduma za usalama za Urusi FSB . Mtu ambae nilimfahamu kwa miaka 10. Hapakuwa na sababu kabisa ya mtu yule kuwepo chumbani kwangu . Hakuna sababu ya wao kunipatia kifaa hicho(flash drive)."

Alipoulizwa na BBC ikiwa kulikuwa na siri za taifa kwenye kifaa hicho , kama waendeshamashtaka walivyosisitiza , Bwana Whelan alisema kuwa "hakufahamu ".

"Sikukiangalia kifaa chenyewe . Sikujua kuwa nilikuwa nacho mpaka nilipokamatwa . Huu ni uchokozi asilimia 100% na ni mbaya sana ," alisema.

Wakili mtetezi wa mshtakiwa ladimir Zherebenkov pia aliielezea kesi hiyo kama ''uchokozi'' , na kuongeza kuwa hakuona ushahidi hadi sasa wa kumweka mteja wake hatiani

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Bwana Whelan ameendelea kupata mkanganyiko na ni wazi kuwa amekanganyikiwa , anasema mwandishi wa BBC

Jaji alirejea kusoma hukumu dhidi yake - na kusema kuwa anapaswa kuwekwa mahabusu, kabla ya kufanyika kwa kesi dhidi yake na ndipo Bwana Whelanalipopaza sauti kupinga kesi yake akiitaja kama "takataka".

Bwana Whelan, ambaye amesema kuwa aliumizwa na daktari na kukataa matibabu , pia amezitaka serikali zote za mataifa yake kumsaidia.

Ni kwanini alikamatwa ?

Bwana Whelan aliwasili Urusitarehe 22 Disemba kuhudhuria harusi na alikuwa na mpango wa kutembelea St Petersburg pamoja na Moscow kabla ya kurejea nyumbani tarehe 6 Januari, kulinga na maelezo yaliyotolewa na kaka yake alipozungumza na BBC.

Akikamatwa mjini Moscow baada ya kuchukua kikundi cha wageni waliokuwa wakihudhuria harusi katika matembezi kwenye makumbusho ya Kremlin

Maafisa wa huduma za ujasusi za Urusi FSB wanasema alikamatwa "wakati alipokuwa akifanya kitendo cha uchunguzi wa ujasusi ".

Whelan ni nani ?

Bwana Whelan alizaliwa nchini Canada na wazazi wake walikuwa Waingereza lakini akahamia Marekani alipokuwa mtoto . Kwa sasa ni Mkuu wa usalama wa kampuni ya Michigan automotive components supplier BorgWarner.

Kaka yake anasema Bwana Whelan amekuwa akitembelea Urusi kwa shughuli za kibiashara na za burudani tangu mwaka 2007.

Bwana Whelan alijiunga na kikosi cha wanamaji cha Marekani mwaka 1994 na kupanda hadi cheo cha Sajenti mwama 2004. Alihudumu nchini Iraq kwa miezi kadhaa katika miaka ya 2004 na 2006.