Mwanamume akaa siku tano na kichwa chake kikiwa kimekwama kwenye ngazi

Hili halikuwa katika muogozo wa ukarabati: mwanamume aliyekuwa anajaribu kukarabati na kulirembesha bafu lake huko mashariki mwa Ufaransa aliteleza akaanguka na kukwamisha kichwa chake kwenye ngazi ...kwa siku tano.

Vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa, mwanamume aliye katika miaka ya 60 alikuwa amepotewa na fahamu wakati wahudumu w aafya walipowasili .

Waliarifiwa na dadake , aliyemtembelea siku ya Ijumaa.

Kichwa chake , kilichokwama katikati ya ngazi , kilifura katika siku hizo tano na alishindwa kuifikia simu yake kuomba usaidizi.

Msukumo wa damu kichwani mwake ulipungua, na anafanyiwa ukaguzi hospitalini.

Jamaa huyo anayetoka Mattaincourt karibu na Épinal, ambaye jina lake halikuwekwa wazi alipatikana akiwa hana maji mwilini.

Huenda pia ukavutiwa na hii: