Uganda kusitisha hukumu ya kifo: Ni mataifa gani bado yanaitekeleza?

Uganda
Maelezo ya picha, Je, rais Yoweri Museveni atasitisha hukumu ya kifo Uganda?

Bunge la Uganda limepitisha sheria inayopinga hukumu ya adhabu ya kifo kwa baadhi ya uhalifu, na kufanya marekebisho katika sheria nne tofauti ikiwemo sheria ya kupambana na ugaidi.

Kama sheria hiyo itasainiwa na rais Yoweri Museveni , marekebisho hayo yatasitisha hukumu ya kifo kwa uhalifu mkubwa zaidi, kwa maelekezo ya jaji.

Watunga sheria wanasema kuwa hii ni hatua kubwa inayoweza kutokomeza hukumu hiyo, jambo ambalo mahakama iliwahi kupigia kelele.

Kuna wafungwa 133 ambao wamehukumiwa kunyongwa lakini sasa imepita miaka 20 tangu wahukumiwe.

Kumekuwa na kampeni mbalimali za kutokomeza hukumu hilo, kufuatia hukumu ya mwaka 2009 ya mfungwa Susan Kigula ambaye alihoji juu ya hukumu ya kifo kuwa kinyume na katiba.

Mahakama baadae ilitaka hukumu ya kifo isiwe lazima kwa kesi za mauaji, na kuwasisitiza watu kuwa mtu hapaswi kuwekwa jela kwa miaka mitatu wakati amehukumiwa kunyongwa muda huo ukipita mfungwa huyo ni sawa kuwa amepewa hukumu ya kifungo cha maisha.

Mara ya mwisho Museveni kudihinisha hukumu ya kifo itekelezwe ilikuwa mwaka 1999 na watu 27 katika gereza la Luzira hapa mjini Kampala.

Kadhalika, aliidhinisha mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya kifo mwaka 2005.

gereza

Makubaliano ya kusitisha sera au utekelezaji

Ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu hukumu ya kifo imewasilishwa katika tume ya haki za binadamu mwezi Septemba mwaka huu na kusema kuwa kuna mataifa 170 wameachana na adhabu hiyo ya kifo kisheria na utekelezaji au hajauliwa mtu kwa zaidi ya miaka 10.

Umoja wa mataifa ambayo ina wanachama 193, hivyo ni mataifa 23 tu ndio ambayo inawezekana walitoa hata hukumu moja ya kifo katika muongo uliopita.

Kwa kihistoria, Kanisa limekuwa likizuia adhabu ya kifo, ikiwa ni pamoja na katika karne ya 20.

Hukumu ya kifo Afrika mashariki

Nchini Kenya wahalifu wamekuwa wakihukumiwa kifo Kenya lakini hakuna aliyewahi kuuawa tangu miaka ya 1980.

Watetezi wa haki wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa hukumu hiyo.

Baadhi ya wafungwa hata hivyo wamekuwa wakilalamika kwamba hakuna tofauti ya hukumu ya kifo na maisha jela kwani mfungwa huwa anaishi jela hadi kifo chake.

Nchini Tanzania, takriban wafungwa 500 wapo katika jela za Tanzania wanakabiliwa na hukumu hiyo.

Rais wa Tanzania, John Magufuli amekwisha weka wazi msimamo wake juu ya utekelezaji wa hukumu ya kifo kuwa hawezi kusaini mfungwa yeyote aliyehukumiwa adhabu hiyo kwenda kunyongwa.

Mara ya mwisho kwa mfungwa kunyongwa nchini ilikuwa mwaka 1994, enzi za utawala wa Rais wa awamu ya pili wa nchi hiyo, Ally Hassan Mwinyi.

kunyongwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaharakati wa haki za binadamu walifungulia kesi serikali ya Tanzania mwezi Julai na hukumu ilisalia vilevile bila mabadiliko

Hukumu ya kifo duniani

Nchi 106 hukumu ya kifo haikubaliki kisheria

Nchi 7 zinaruhusu hukumu ya kifo lakini kwa uhalifu mkubwa ambapo pia huwa inategemea na mazingira yenyewe kama wale ambao waliofanya uhalifu wakati wa vita.

Nchi 29 ambazo sheria yao inaruhusu adhabu ya kifo lakini hakuna aliyeuliwa takribani miaka 10 na hazaijasema rasmi kuwa zitaachana na adhabu hiyo au kuwa na sera inayopinga

Nchi 56 ambazo zinatekeleza hukumu ya kifo na sheria na mamlaka hayajaweka tamko rasmi ya kuachana na adhabu hiyo

Kwa mujibu wa shirika la kmataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International mpaka kufikia 2017 nchi 142 zimeacha kutoa hukumu ya kifo kisheria na/au kiutekelezaji.

Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa nchi 170 zimeachana na adhabu hiyo kwa nman moja au nyengine.

UN ina wanachama 193, hivyo ni mataifa 23 tu ndio ambayo inawezekana walitoa hata hukumu moja ya kifo katika muongo uliopita.

Idadi ya nchi ambazo rasmi zimeachana na hukumu ya kifo zinaongezeka kutoka 48 mwaka 1991 mpaka 106 mwaka 2017.

Hivi karibuni, baadhi ya nchi ambazo zimetekeleza hukumu hiyo zimekataa kuhusika.

kifo

Mataifa ambayo yametekeleza hukumu ya kifo kati ya mwaka 2013 na 2017

Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Belarus, Botswana, Chad, China, Egypt, Equatorial Guinea, India, Indonesia, Iran, Iraq, Japan, Jordan, Kuwait, Malaysia, Nigeria, Korea Kaskazini, Oman, Pakistan, Palestina,

Saudi Arabia, Singapore, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Taiwan, Thailand, United Arab Emirates, Marekani, Vietnam na Yemen.

Nchi ambazo hazijatekeleza adhabu hiyo licha kuwepo kisheria kati ya 2013 na 2017

Nchi nyengine zinazofanya hivyo ni pamoja na Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Comoros, Cuba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Dominica, Ethiopia, Gambia, Guyana, Jamaica, Lebanon, Lesotho, Qatar, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Trinidad na Tobago, Uganda na Zimbabwe.

Nchi 21 ambazo hazijatekeleza hukumu ya kifo katika miaka hiyo licha ya kuwa hazijaachana na adhabu hiyo

Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Comoros, Cuba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Dominica, Ethiopia, Gambia, Guyana, Jamaica, Lebanon, Lesotho, Qatar,

Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Trinidad na Tobago, Uganda na Zimbabwe.