Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Sudan : Jeshi na upinzani watia saini mkataba wa kihistoria wa kugawana madaraka
Bara za la jeshi lianaloongoza nchini Sudan na muungano wa upinzani wafikia mkataba wa kihistoria wa kugawana madaraka.
Makubaliano hayo yanatoa nafasi ya kubuniwa kwa baraza jipya la uongozi utakaojumuisha viongozi wa kijeshi na raia kwa kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu ambapo utawala wa kiraia utachaguliwa.
Mohamed Hamdan "Hemeti" Dagolo, ambaye anasadikiwa na wengi kuwa mwenye ushawishi mkubwa katika utawala wa nchi hiyo ameahidi kutekeleza kikamilifu mkataba huo.
Sudan imeshuhudia maandamano makali ya upinzani kufuatia utawala wa ukandamizaji wa kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir aliyeng'olewa madarakani mwezi Aprili mwaka huu.
Mkataba huo ulitiwa saini na Hemeti na Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan kwa niaba ya baraza la kijeshi na Ahmed al-Rabie kwa niaba ya vuguvugu linalounga mkono demokrasia nchini Sudan.
Mawaziri wakuu wa Ethiopia na Misri pamoja na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit walikuwa miongoni mwa viongozi wa kikanda waliohudhuria sherehe ya kutiwa saini mkataba huo mjini Khartoum.
Chini ya mkataba huo, baraza la utawala litakalojumuisha raia sita na majenerali watano wa kijeshi litabuniwa kuongoza nchi hiyo hadi uchaguzi mkuu utakapoandaliwa.
Pande hizo mbili zime kubaliana kubadilishana uwenyekiti wa baraza hilokwa zadi ya miaka mitatu.
Waziri mkuu atakayeteuliwa na raia anatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.
Hemeti alisema nini?
"Tutazingatia kila kipengele cha mkataba huu kama tulivyokubaliana," Hemeti alisema katika mahojiano na BBC kabla ya sherehe ya kutia saini mkataba huo.
"Hata bila ya makubaliano [tutafanya] kazi pamoja kwa maslahi ya nchi hii,"aliongeza. "Kwahivyo tumeamua kutekeleza makubaliano yaliomo ndani ya mkataba huu ambao tunaunga mkono kwa kauli moja."
Hemeti ni kamanda wa kikosi cha uingiliaji kati wa haraka -Rapid Support Forces (RSF), ambacho kimekuwa kikishutumiwa kwa kuwauwa waandamanaji.
Kikosi hicho sasa kitakuwa chini ya utawala wa jumla wa kijeshi , na huduma za ujasusi zitaongozwa na baraza la uongozi pamoja na baraza la mawaziri kwa ujumla.
Mkataba juu ya azimio unakuja baada ya baraza la kijeshi kutangaza kwama wanajeshi wa RSF walikuwa wamefutwa kazi na kukamatwa kuhusiana na mauaji ya waandamanaji
Mauaji yaliibua maandamano makubwa kote nchini humo na kusababisha kuchelewa kwa mazungumzo.
Tunafahamu nini juu ya kipindi cha mpito?
- Jeshi na waandamanaji wamefikia makubaliano kadhaa, huku kila upande ukiongeza maelezo zaidi huku wakijaribu kuondoa hali ya kutoaminiana na kujenga uhusiano wa kikazi.
- Hadi kufikia sasa wamekubaliana yafuatayo:
- Mgawanyo wa mamlaka utadumu kwa miezi 39
- Baraza la huru, baraza la mawaziri na bunge vitaundwa
- Jenerali ataongoza baraza kwa miezi ya kwanza 21, na raia ataongoza miezi 18 iliyosalia.
- Waziri mkuu , atakayeteuliwa na vuguvugu linalounga mkono demokrasia, ataongoza baraza la mawaziri
- Tmawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani watachaguliwa na jeshi
Kipindi kirefu cha mpito kinaonekana kama ushindi kwa vuguvugu linalounga mkono demokrasia -majenerali walikuwa wametishia kuitisha uchaguzi wa haraka baada ya kamata kama ya 3 Juni
Waandamanaji wanadai utawala wa Bwana Bashir ulikuwa umekita mizizi sana na kwamba itachukua muda kuvunja mitandao yake ya kisiasa na kufungua njia ya uchaguzi huru na wa haki.