Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kwanini uhalifu hauishi katika mji wa Capetown ?
Maafisa nchini Afrika Kusini wamepeleka wanajeshi katika katika mji wa mwambao wa Cape Town kukabiliana na ghasia za magenge ya uhalifu.
Waziri wa polisi Bheki Cele amesema kuwa wanajeshi watashirikiana na polisi katika operesheni ya polisi kwa ajili ya kufichua mihadarati na silaha
Takriban watu 14 waliuawa katika kipindi cha saa 24 lmwishoni mwa juma katika eneo moja la mji wa Cape Town lililokumbwa na ghasia za silaha.
Tatizo la magenge ya uhalifu mjini Cape Town limekuwepo kwa miongo kadhaa .
Taarifa zinasema kuwa mashambulio ya silaha ya hivi karibuni yametokana na vita vikubwa baina ya magenge mawili hasimu , na yalichochewa na mashambulio ya ulipizaji kisasi.
Ripoti zinasema kuwa Tidadi kubwa ya polisi wamekita kambi katika vitongoji vya Bonteheuwel, Delft, Hanover Park na Philippi vilivyopo mashariki wa Capetown.
Bwana Cele amesema kuwa kupelekwa kwa wanajeshi na polisi kwenye eneo hilo ni sehemu ya hatua ''zisizo za kawaida'' ambazo zilizoilazimu serikali kuchukua ili kuhakikisha usalama wa raia unakuwepo.
"Tutakwenda mlango hadi mlango, tutakusanya kila bunduki inayomilikiwa kwa njia haramu, tutawakusanya wahalifu wote ambao walipewa dhamana na hilo litafanyika kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi ," Amewaambiwa waandishi wa habari Bwana Waziri wa polisi.
Uvamizi unalenga "kuonyesha mamlaka ya taifa ",alisema waziri Cele.
Alitetea hatua ya kuwapeleka wanajeshi, akisema kuwa kuwa wanajeshi watakuwa ''wanaongozwa na kupata maagizo'' kutoka kwa polisi - na pia walitumiwa katika kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi wa Mei.
Wanajeshi watakuwa katika operesheni hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu na wanaweza kuongezewa muda . "Baada ya hapo, kuna haja ya kuwepo kwa usalama wa kudumu ," alisema katika taarifa ya kituo cha habari cha News24.
Kwa mara ya mwisho jeshi lilipelekwa kukabiliana na uhalifu mjini Cape Town mwaka 2017.
Suluhu ya jeshi kwa tatizo la kiuchumi
Tatizo la magenge ya uhalifu mjini Cape Town ni ishara ya ukosefu wa usawa katika jamii, ambapo kuna pengo kubwa baina ya wale wenye uwezo wa kufikia raslimali na kupata maisha mazuri na wale wasio nacho.
Katika baadhi ya maeneo ya mji huo kama vile Cape Flats, maelfu ya watu wanaishi katika vitongoji duni wengi wao wakiwa ni maskini bila ajira.
Hizi ni jamii ambazo zinaona kuwa zimesahauliaka.
Kwa vijana wengi wasio na ajira, magenge ni mahala pa kukimbilia kwa ajili ya kujikimu kimaisha, kwani ni nujia rahisi ya kupata pesa .
Kuna hisia mchanganyiko juu ya uwepo wa wanajeshi katika mji wa Cape Town - kwa wakazi wa eneo hilo wanaohisi kuwa hawana msaada wa kukabiliana na uhalifu wa magenge hatua hiyo imepokelewa vema.
Lakini baadhi wanahofu juu ya uingiliaji kati wa jeshi.
Huku uwepo wa jeshi na polisi unaweza kumaliza mashambulio kwa muda, hauwezi kufanya lolote kutatua sababu zinazochochea uwepo wa magenge mjini humo.
Labda hii inaelezea wazi ni kwanini licha ya kupelekwa mara kadhaa kwa polisi na wanajeshi Cape Flats bado ni kitovu cha magenge ya uhalifu.
Unaweza pia kutazama:
Labda hii inaelezea wazi ni kwanini licha ya kupelekwa mara kadhaa kwa polisi na wanajeshi Cape Flats bado ni kitovu cha magenge ya uhalifu.