Vijana wa Afrika wanakabiliwa na uwezekano wa kutoa hongo zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Vijana wa Afrika wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutoa hongo kuliko waafrika wenye wakubwa wao.
Shirika la kukabiliana na ufisadi la kimataifa Transparency International linasema vijana wa Afrika wenye umri wa kati ya miaka 18-34, wana uwezekano mkubwa wa kutoa rushwa kuliko watu wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 55.
Katika kipimo chake cha kiwango cha Ufisadi duniani cha mwaka 2019, shirika hilo limeseam kuwa utafiti wake pia umefichua kwamba watu maskini zaidi wana uwezekano mara mbili zaidi wa kutoa rushwa - na wanauwezekano mkubwa pia wa kuwa waathiriwa wa hongo inayosababishwa na tabia ya urasimu kuliko matajiri.
Utafiti huo wa kila mwaka ambao ni wa mwaka wa 10, unasema kuwa barani Afrika ni wa kiwango cha juu zaidi katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambapo asilimia "75% ya wale ambao wanakabiliwa na ufisadi waliwalipa polisi hongo".

Chanzo cha picha, Transparency International
Ripoti hiyo pia inasema kuwa raia wa kigeni pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuchochea na kushiriki ufisadi katika bara la Afrika , "na hivyo kuhujumu cmaendeleo ya kudumu ya kikanda".
Transparency International linasema kuwa makampuni hutoa hongo ili kupata mikataba kama vile ya haki ya uchimbaji wa madini , mikataba ya ujenzi wa miradi mikubwa na mikataba mingine.
Transparency International linasema pia kwamba matokeo ya utafiti wake yametokana na mahojiano ya ana kwa ana kati ya Septemba 2016 na Septemba 2018, yaliyofanyika kwa ushirikiano na taasisi ya utafiti wa kimaendeleo barani Afrika-Afrobarometer.








