Mamia waandamana kupinga ufisadi serikalini Kenya

Rais Kenyatta
Maelezo ya picha, Wanaharakati wanamtaka Rais Kenyatta achukue hatua

Mamia ya watu wamekusanyika eneo la Freedom Corner katika Uwanja wa Uhuru Park, katikati mwa jiji la Nairobi, kuandamana kulalamikia wanachosema ni ongezeko la visa vya ufisadi serikalini.

Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari zinazodai jumla ya dola 50 milioni za Marekani katika wizara ya afya zilitumiwa vibaya au zikaporwa.

Serikali imekanusha madai hayo.

Wanaharakati walioandaa maandamano ya leo wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua la sivyo ajiuzulu.

Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.

Polisi wa kupambana na fujo wakiwa uwanja wa Uhuru Park
Maelezo ya picha, Polisi wa kupambana na fujo wakiwa uwanja wa Uhuru Park
Baadhi ya waandamanaji wamejifunga minyororo mikononi
Maelezo ya picha, Baadhi ya waandamanaji wamejifunga minyororo mikononi
Rais Uhuru komesha ufisadi au jiuzulu, yanasema baadhi ya mabango
Maelezo ya picha, Rais Uhuru komesha ufisadi au jiuzulu, yanasema baadhi ya mabango
Maandamano Nairobi