Ukraine yapendekeza sheria itakayopiga marufuku matusi

Dr Ulana Suprun, Ukraine's health minister
Maelezo ya picha, Kaimu waziri wa afya Ukraine Ulana Suprunasema matusi ni mazuri kwa afya ya binaadamu

Pengine sote tumewahi kutukana katika maisha yetu.

Ima ni kutokana na hasira au kwa sababau yoyote ile nyingine, lakini ni sehemu nzito ya lugha inayotumika na watu katika makabila tofuati.

Nchini Ukraine, kaimu waziri wa afya Ulana Suprun amependekeza kwamba matusi ni mazuri kwa afya yako kutokana na kwamba mtu anapotusi, inaashiria uhusiano mzito ulioimarika na ni 'mawasiliano mazuri ya kihisia' baina ya watu.

Suprun alikuwa anazungumzia sheria iliyopendekezwa ya kusitisha lugha chafu katika vyombo vya habari.

Sheria hiyo inaeleza kwamba watu wanaotukana hewani na katika hotuba kwa umma, watatozwa faini ya hadi $49.

Lakini mtazamoa wa Dkt Suprun ni kwamba kutukana au matusi ni muhimu katika hali mbaya akisema "katika visa kadhaa matusi humaanisha watu wana ukaribu na kwamba kuna mawasiliano mazuri ya kihisia kati yao".

Ameongeza kwamba ni muhimu watu kushirikiana kuondosha hamaki badala ya matusi.

matusi

Chanzo cha picha, Veronique DURRUTY

'Vyumba vya kutusi'

Licha ya sheria hiyo kulengwa kwa viongozi wa umma na sio raia wa kawaida, wengi wamefanya mzaha katika mitandao ya kijamii kuhusu namna ambavyo maisha yao yatabadilika kutokana na hilo.

Mmoja kwa jina Yevhen Halahan anawaza namna raia wa Ukriane wataweza sasa kuzungumza kuhusu maisha Ukraine" iwapo sheria hiyo inayopinga matusi itapitishwa

Wengine wamewaza iwapo kutaidhinishwa sehemu maalum ambapo watakuwa wanaruhusiwa kutusi.

Huenda "vyumba vya kutusi " vikaidhinishwa, anapendekeza v na pengine kutakuwana sehemu maalum katika migahawa kwa wavutaji sigara, na wasiovuta na kadhalika kwa wanaotusi.

Na wengine wengi wamezungumzia fikra ya kupitishwa sheria hiyo ya kupiga marufuku matusi.

Sheria ya 'kuthibiti matusi' kwa sasa inakaguliwa na kamati ya bunge.