Wakamatwa India kwa kumshambulia afisa mwanamke

Chanzo cha picha, BBC Telugu
Wanaume kumi na sita wamekamatwa baada ya umati wa watu kumpiga vibaya kwa fito afisa mwanamke wa misituwakatimaafisa wa polisi wakitazama katika jimbo la kusini nchini India Telangana.
Umati huo ulioongozwa na mfuasi wa chama kikuu cha kisiasa katika jimbo hilo, walikuwa wakilalamika kuhusu kampeni ya upanzi wa miti iliyoidhinishwa Jumapili.
Video ya shambulio hilo imesambaa, na chama hicoh tawala kimeshutumu shambulio hilo kwenye Twitter.
Afisa huyo wa misitu anapokea matibabu katika hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya.
Kanda hiyo ya video inaonyesha umatiukimshambulia afisa huyo kwa fito za mianzi, wakati akiwa amesimama kwenye trekta na anajaribu kuzizuia fito hizo.
Anapigwa mara kwa mara kwa fito hizo hadi maafisa wa misitu na maafisa wa polisi katika enoe hilo wanaingilia kati na kuwatawanya watu hao na kudhibiti shambulio.
Video hiyo imesambazwa nchini Indiana kuzusha hasira kote nchini.
Hatua iliyomsababisha afisa mkuu wa chama cha Telangana Rashtra Samithi (TRS) , Kalvakuntla Taraka Rama Rao, kushutumu tukio hilo kwenye mtandao wa Twitter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kiongozi wa umati huo uliomshambulia anayefahamika kama Koneru Krishna Rao, ni afisa katika eneo hilo ambaye ni kakake mbunge mmoja wa chama cha TRS . Chama hicho kimethibitisha kwamba jamaa huyo ametiwa mbaroni.
Katika kujitetea, Rao ameviambia vyombo vya habari nchini kwamba alikuwa anajaribu 'kuhakikisha wakulima wa kikabila wanapata haki wakati maafisa wa misitu wanayaharibi mimea yao'.
"Idara ya misitu inawatishia wakulima na kuwapokonya kwa nguvu ardhi zao", alituhumu, akiongeza kwamba shambulio hilo lililotokea kwa 'bahati mbaya'.
Maafisa wawili wa polisi waliokuwa katika eneo hilo wakati wa shambulio wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kumlinda afisa huyo mwanamke, BBC Telugu imethibitisha.













