Watu wanaokata tamaa hukimbilia wapi? Nchi hizi zinasimulia hali ya wakimbizi mwaka 2018

Chanzo cha picha, AFP
Watu huenda wapi maisha yao yanapotishiwa na mapigano, mateso au njaa?
Takribani asilimia 80 ya watu hawaondoki nchini mwao, na wale wanaoondoka, takribani asilimia 80 huenda nchi jirani, si zaidi ya hapo.
Katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani, tunatazama nchi sita ambazo zilikua na idadi kubwa ya wakimbizi mwaka 2018
Uturuki
Uturuki inahifadhi wakimbizi wengi kuliko nchi nyingine yeyote-matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, tangu mwaka 2011
Idadi kubwa pia inasafiri kutoka Afghanistan.
Uturuki inahifadhi karibu mmoja kati ya wakimbizi watano chini ya shirika la wakimbizi duniani UNHCR.
Peru
Peru ni ya pili kupokea wakimbizi mwaka 2018 wengi kutoka Venezuela, kutokana na kuporomoka kwa uchumi.
Watu milioni nne wamekimbia Venezuela tangu mwaka 2015,wengi wakienda nchi jirani,kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa
Juma lililopita Peru iliweka sheria kali za uhamiaji kudhibiti kasi ya wakimbizi kuingia nchini humo.

Chanzo cha picha, AFP
Sudan
Wakimbizi wengi waliowasili Sudan mwaka 2018 walikua wakikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudani Kusini.
Wengine wengi waliingia wakitoka mbali zaidi-Sudan ni ya tatu kwa kupokea wakimbizi kutoka Syria nje ya Mashariki ya Kati.
Lakini Sudan yenyewe ni chanzo cha wakimbizi-Watu 724,800 waliondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka 2018
Uganda
Uganda ilipokea wakimbizi kutoka nchi mbili za jirani waliokimbia nchi zao kutokana na migogoro ya ndani:Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakimbizi karibu 120,000 na Susdani kusini.
Pia ilipokea idadi kubwa ya watoto waliokimbia wenyewe bila wazazi na waliotenganishwa mwaka 2018.
Lakini wakimbizi 83,600 walikua wamerejea nchini Sudani Kusini wakitokea Uganda ilipofika mwishoni mwa mwaka 2018.

Chanzo cha picha, Reuters
Marekani
Pamoja na Marekani kuweka msimamo wake kuhusu masuala ya uhamiaji tangu Rais Trump kuingia madarakani, nchi hiyo bado ilikua ina idadi kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi mwaka 2018, na ilikua na maombi mengi ya watu wanaotafuta hifadhi kuliko nchi nyingine yeyote mwaka huo.
Wakimbizi wa nchini Marekani walitoka katika nchi 166-lakini zaidi ya nusu wametoka katika nchi za Amerika ya Kati au Mexico.
Idadi ya watu walioomba uhifadhi ilikua ndogo kuliko idadi ya 331,700 miaka ya nyuma.
Ujerumani
Ujerumani inahifadhi wakimbizi zaidi ya milioni moja-zaidi ya nusu yao kutoka Syria (532,000 mwishoni mwa mwaka 2018).
Nchi hiyo bado ilikua chanzo cha idadi kubwa ya wakimbizi kuingia nchini Ujerumani mwaka 2018, lakini idadi nyingine kubwa iliingia kutoka nchini Iraq
Lakini ingawa Ujerumani inashika nafasi ya tatu duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya maombi ya uhamiaji, idadi imepungua kutoka 722,000 mwaka 2016.
Idadi ya watu wanaoomba hifadhi ilishuka kwa asilimia 14 mwaka 2018 pekee.
Makala haya yanatoka kwenye ripoti ya Shirika la wakimbizi duniani.












