Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afa kwenye Ndege kwa kumeza dawa za kulevya
Mwanaume mmoja raia wa Japan, amepoteza maisha ndani ya Ndege akitokea Mexico City baada ya kumeza kete 246 za Cocaine.
Ndege hiyo, iliyokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita nchini Japan ililazimika kutua kwa dharura katika jimbo la Sonora nchini Mexico mwanaume huyo alipoanza kupoteza fahamu.
Mamlaka zimesema mtu huyo aliyejulikana kwa jini la Udo N, alipoteza maisha baada ya ubongo wake kujaa maji kutokana na matumizi ya madawa kupita kiasi.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria mkuu wa jimbo la Sonora, Kete zilizokua na urefu wa sentimita 2.5 na upana wa sentimita 1 zilikutwa tumboni na kwenye utumbo wakati wa uchunguzi.
Abiria wengine 198 waliobaki waliendelea na safari baada ya kutua kwa dharura katika mji wa Hermosillo.
Mamlaka za Mexico zimesema zitaendelea na uchunguzi.