Joseph Temba atajirika baada ya kupata almasi kubwa zaidi Tanzania

Mchimbaji Mdogo wa Madini Mkoani Shinyanga ameuza Almasi yake kwa Tsh. Bilioni 3. Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ashuhudia.

Chanzo cha picha, Wizara ya Madini Tanzania

Maelezo ya picha, Mchimbaji Mdogo wa Madini Mkoani Shinyanga ameuza Almasi yake kwa Tsh. Bilioni 3. Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ashuhudia.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Taifa la Tanzania limejipatia bilionea wake wa hivi karibuni baada ya mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga kuuza almasi yake kwa takriban dola milioni moja nukta nne sawa na Tsh. Bilioni 3.

Almasi hiyo yenye karati 512 ilipatikana na mchimbaji madini mdogo Joseph Temba wiki mbili zilizopita katika eneo la Maganzo huko Shinyanga.

Bwana Temba ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa Almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao uko wazi.

Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wezake kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali kwani kuna faida nyingi hivyo hawana sababu ya kukwepa Masoko hayoo.

Kulingana na naibu waziri wa madini nchini humo Stanlaus Nyongo almasi hiyo ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini humo.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Alamsi iliopatikana

Chanzo cha picha, Wizara ya Madini Tanzania

Akifichua tangazo la kupatikana kwa almasi hiyo katika mtandao wake wa Twitter bwana Nyong'o alisema kuwa serikali imejipatia shilingi milioni 238 kutokana na mauzo ya madini hayo.

Nyongo amewahimiza na kuwasisitizia wachimbaji wote na wanunuzi kote nchini kufanya shughuli hizo kwenye masoko ya madini yaliyoainishwa na kutambulika na Serikali.

Almasi ya bwana Temba ilipokuwa ikipimwa

Chanzo cha picha, Wizara ya Madini Tanzania

Amempongeza bwana Joseph Temba kwa kufuata utaratibu katika mauzo yake na kwamba Serikali itaendelea kusimamia mauzo yake mpaka hatua ya mwisho.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Almasi ya waridi

Almasi ghali zaidi duniani ni ile yenye rangi ya waridi ambayo ni adimu kupatikana iliuzwa kwa dola milioni 50 kwa karati.

Almasi hiyo na ina uzito wa chini ya karati 19.

Almasi hiyo ilinunuliwa na chapa ya Harry Winston mwenye asili ya Marekani katika mnada uliofanyika Geneva.

"Karati moja iligharimu takribani dola milioni 2.6 na bei hiyo inathibitisha kuwa almasi ya rangi ya waridi ina gharama kubwa zaidi duniani", kwa mujibu wa mkuu wa nyumba ya mnada barani ulaya, Christie.

Almasi hiyo ilikadiriwa kuwa na thamani ya kati ya dola milioni 30 mpaka dola milioni 50 baada ya kuuzwa kwenye mnada ndani ya dakika tano.

Wachimba migodi wadogo

Chanzo cha picha, OLIVIA ACLAND

Almasi kubwa zaidi yenye karati 476 ilipatikana na wachimba migodi nchini Sierra Leone ikiwa ya 29 kuwai kupatikana duniani.

Hatua hiyo inajiri miezi minane baada ya almasi ya zaidi ya karati 700 kupatikana ambayo ni kabwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leone kwa nusu karne.