Angola yawafukuza wachimbaji haramu

Ramani ya Angola

Chanzo cha picha, Atlas

Maelezo ya picha, Ramani ya Angola

Wahamiaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaokimbia kutoka kaskazini mashariki mwa Angola wanasema kuwa wachimbaji wadogo wa madini ya almasi wanafanyiwa vitendo vya ukatili.

Mashuhuda wanaokimbia maeneo hayo wameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba Majeshi ya Ulinzi ya Angola yameua watu kadhaa, kuchoma nyumba na kupora mali.

Madai ambayo yamekanushwa na mamlaka nchini Angola.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita makumi kwa maelfu ya watu wengi wao asilia yao ikiwa ni Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamekimbilia katika mpaka wa Congo baada ya kulazimishwa kuikimbia Angola.

Mamia ya wakongo ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo wa madini ya almasi, wameamua kurejea nyumbani kuepuka kuvamiwa, kutokana na kwamba Angola hivi karibuni kutangaza kuvunja shughuli za uchimbaji haramu wa madini hayo, baada ya nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini, kufanya mabadiliko katika sekta ya madini ya almasi kwa lengo la kuongeza mapato yake.

Mashuhuda wameiambia Reuters kuwa wameshuhudia vikosi vya jeshi la Angola likifanya uvamizi katika mji wa LUCAPA na kuua idadi kubwa ya watu pamoja na kuchoma nyumba na kisha kupora mali.

Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Angola amekanusha madai yote ya ukiukwajhi wa haki za binadamu.